Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uislamu utakuwa ndio Mwokozi na Nguvu Kuu ya Ulimwengu Ujao

(Imetafsiriwa)

Habari:

Hotuba ya Rais wa Sri Lanka Ranil Wickramasinhe katika maadhimisho ya miaka 100 ya ACJU (All Ceylon Jameeyathul Ulama) mnamo Januari 2023.

“Mnaweza kukumbuka mwanzo wa 1922 wakati ulimwengu ulikuwa unapitia mabadiliko makubwa baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia, ambavyo vilijumuisha kuondolewa kwa Khilafah. Na nchini India kulikuwa na harakati kubwa ya kuregesha Khilafah. Lakini nchini Sri Lanka, pia mliunda ACJU wakati huo huo na kile ambacho kitakuwa fikra moja ya Waislamu na sio theolojia ambayo ndio mjadala ambao umeendelea.

Kwa hiyo leo bado munakabiliwa na baadhi ya masuala yaliyokuwepo wakati huo. Kwanza, tuko katika ulimwengu tofauti na takriban mataifa 150 ambayo hayakuwepo mwaka wa 1922. Tuko katika karne tofauti pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia na maendeleo ya haki za kisiasa. Ni kwa msingi huu ambapo inatubidi kuangalia mustakabali wa Waislamu nchini Sri Lanka.” - (Kutoka kwa Hotuba ya Rais wa Sri Lanka Ranil Wickramasinhe katika hafla ya kuadhimisha miaka 100 ya ACJU)

Maoni:

Uislamu unatengwa na kutoka kwa dhati yake ya kweli kutoka kwa wanadamu baada ya kuanguka kwa Khilafah Uthmani mwaka 1924. Tangu kuibuka kwa Mtume Muhammad (saw) kama kiongozi wa Dola ya Madina katika karne ya 7 hadi zama za dhahabu za ulimwengu hadi kwa Suleiman Mtukufu na hadi kuanguka kwa Khilafah ya Kiuthmani kwa hakika ulikuwa ni Uislamu ndio ambao ulitumika kikamilifu katika mambo ya maisha ya wanadamu kwa zaidi ya karne 13. Dhati ya kweli ya Uislamu ni itikadi yake, isemayo “Hakuna apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu na Mtume Muhammad (saw) ni mjumbe wake”. Ni kumkubali Muumba kama bwana wa ulimwengu yakiwemo mambo ya wanadamu, kwa hiyo mambo yote ya maisha ya mwanadamu (yaani matatizo) yanaweza kutatuliwa kwa kuzingatia mipaka iliyowekwa na Muumba, Mwenyezi Mungu (swt) na kuonyeshwa na kipenzi Mtume Muhammad (saw) kuitabikisha katika mambo ya wanadamu.

Baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia na kuanguka kwa Khilafah Uthmani mnamo 1924 kulibadilisha mizani ya nguvu ya ulimwengu. Haikuwa ila ni kuuondolewa Uislamu kutoka katika mambo ya maisha ya wanadamu. Huo ulikuwa ni msiba mkubwa zaidi uliotokezwa na maadui wa wanadamu. Sasa ni miaka 99 (M) tangu wakati huo. Dunia imekabiliana nao katika miaka hii 99 ambayo haikuwa imeona kabla ya 1924, wakati mlinzi wa wanadamu, Khalifa wa Waislamu, alipokuwepo duniani. Hakuna mtu anayeweza kukataa. Hakuna mtu anayeweza kukataa kile ambacho wakoloni walifanya na bado wanafanya katika ulimwengu huu, katika Afrika, Asia ya Kati, Asia na Asia ya Mashariki. Waliyakoloni (waliyafuja) mataifa haya, mali zao, rasilimali zao, watu (imani zote), na hawakuacha kiumbe chochote kwa hiari yake. Kisha wakasema wamewapa uhuru wao. Lakini wamewakoloni kwa akili zao. Kwa maana nyengine, waliwafundisha wengine kwa nguvu kufikiri kulingana na njia yao ya maisha. Walipandikiza vibaraka wao wenyewe kama watawala na kutawala kwa kile walichokifundisha kutawala.

Maombolezi ya Rais kuhusu kupotea kwa miaka 75 katika machafuko hayakuwa kazi ya Khilafah katika utendaji, bali utawala wa Marekani na Ulaya juu ya makoloni ya zamani kazini. Utawala ambao haukuzaa amani wala ustawi popote, achilia mbali Sri Lanka. Leo hii wanadamu kwa jumla kwa thamani yoyote ya kidini iliyoachwa nyuma wanatishiwa na Ubepari wa Magharibi na sio Uislamu. Miaka 100 ya dunia inayoongozwa na Ubepari wa Magharibi imemimina utajiri wa dunia kwa idadi ya watu ambayo ni chini ya 1% ya watu wote, zaidi ya watu 25,000 wanakufa kwa njaa kila siku, vifo na kuhama (kutokana na vita) ambapo haikufanyika katika miaka elfu chache iliyopita ikiunganishwa kwa pamoja, kuvunjika kwa maadili ya kijamii, kuvunjika kwa utukufu wa ndoa kati ya mwanamume na mwanamke kunakosababisha kuendelea kwa wanadamu. Kadi ya ripoti ya ubepari unaoongozwa na Magharibi iko wazi sana kwa mtu wa hadhi kama hiyo kuikosa! Ni kweli, dini inaweza kuwa imekuwa chombo katika baadhi ya matukio ya kukiuka mambo yasiyoweza kukiukwa, lakini mtu anapaswa kukwaruza tu uso wa matukio kama hayo ili kutambua kwamba nyuma ya matukio hayo kulikuwa na 'nguvu za kidemokrasia' zenye kucheza na benki za kura, kama mpumbavu anayecheza na moto.

‘Usekula’ huonekana na hutoa wito wa kuchora mstari wa usawa katika dini zote kwa kuweka thamani zote za kidini nje ya mambo ya maisha. Unachukua msingi wa kimaadili kuweka mipaka kwa wanadamu kupitia sheria ya walio wengi, ingawa mara nyingi inachongwa na maslahi ya kisiasa ambayo yanawakilisha mabepari, washawishi au benki za kura. Kutokuwa na uwezo wa kushughulika na mipaka kwa ajili ya wanadamu kumechukua msingi huo wenye kasoro wa kimaadili kwa ‘usekula’. Matokeo ya dhana hii sio lazima yatabiriwe kwa siku zijazo, lakini inaweza kutazamwa nyuma miaka 50 hadi 100. Ni kweli, kukosekana kwa mfumo wa utawala wa Khilafah katika ulimwengu wa Kiislamu kumemaanisha kwamba fisi wako tayari kula.

Mfumo wa utawala wa Khilafah, ambao uliondolewa kwa uchungu na Mustafa Kemal unasadifiana na kongamano la hivi majuzi. Waislamu lazima watambue kwamba mfumo wa utawala wa Khilafah kamwe haufai kulinganishwa na mfumo wowote wa tawala duniani bila kujali ni wa Kidemokrasia, Udikteta, Ufalme au mengineyo. Wajibu wa Waislamu kumteua Khalifa kuwa mrithi wa Mtume (saw) katika utawala, ni kuhakikisha kwamba mipaka ya Mwenyezi Mungu (swt) inawekwa juu kabisa ya raia wa dola ya Khilafah (Waislamu na wengineo) na kama kinara wa sheria zinazoleta ustawi duniani na Akhera. Yule (Muislamu) anayeiamini na kuishi chini ya Shariah anapata amani na utulivu wa dunia na Akhera. Yule asiyeiamini lakini anaishi chini ya Shariah angalau atafurahia amani na utulivu wa dunia hii na ataipoteza Akhera – kama jambo la hiari yao, baada ya kulipa Jizya. Hakika yule, awe Muislamu au la, ambaye anatamani kuishi chini ya ‘usekula’ hupoteza amani na utulivu katika dunia na Akhera chini ya mangati ya uhuru.

Enyi Waislamu wa Umma Mtukufu, harakisheni juhudi zenu za kurudisha mfumo wa utawala wa Khilafah katika ulimwengu wa Kiislamu ili fisi wa dunia hii wafungiwe na kupunguzwa kutokana na kuila amani. Mfumo wa Khilafah wakati fulani ulikuwa ni mwenge wa amani, ustawi na maendeleo kwa kuwa ulitafuta kutabikisha nidhamu za Mwenyezi Mungu (swt) duniani. Je, haustahili kurudi tena kwa wanadamu?

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abdallah Afwas

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu