Jumatano, 04 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Serikali ya Uturuki Yafanya Kazi kwa Bidii ili Kuung’arisha Utawala wa Kihalifu nchini Syria

(Imetafsiriwa)

Habari:

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Cavusoglu amekutana na Salem Al Meslet, Rais wa Muungano wa Kitaifa wa Vikosi vya Mapinduzi na Upinzani vya Syria, Bader Jamous, Rais wa Tume ya Majadiliano ya Syria na Abdurrahman Mustafa, Mkuu wa Serikali ya Muda ya Syria jijini Ankara. Cavusoglu alisema “Tunashukuru na kuunga mkono mchango wa upinzani katika mchakato wa kisiasa ndani ya muundo wa Azimio 2254 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.” (Yeni Safak 24.08.2022)

Maoni:

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut anafanya kazi katika kuusafisha uhalifu wa utawala wa Assad, ambao ni mojawapo ya tawala ovu na katili zaidi. Zaidi ya hayo, wiki mbili zilizopita, baada ya XIII, katika Kongamano la Mabalozi jijini Ankara, alisema kuwa kupatanisha utawala wa mauaji na watu wa Syria ndio suluhisho - bila kuonyesha dalili yoyote ya aibu.

Tunapotazama nyuma katika uasi wa Syria ulioanza miaka 11 iliyopita, itaeleweka kwa motisha gani Uturuki na watendaji wengine wametenda.

Burhan Ghalioun, ambaye Cavusoglu alisimama pamoja naye kwa kuwachukua wawakilishi wake kulia na kushoto, alikuwa amesema, "Tatizo halisi nchini Syria ni kwamba watu wanapinga chochote isipokuwa utawala wa Kiislamu". Katika kipindi hicho hicho, mmoja wa waandamanaji katika mitaa ya Syria alisema, "Tutaupindua utawala kwanza, kisha Muungano wa Kitaifa." Huu ndio uhalisia ulio nyuma ya sera za njama zinazofanywa na dola za kiulimwengu na kikanda juu ya Syria.

Uhalisia huu uliofichuliwa na Waislamu wa Syria kwa mapenzi ya Kiislamu na kujitoa muhanga kukubwa umewafanya mabeberu makafiri kukosa usingizi.

Kwa sababu dhalimu Bashar al-Assad ameuona ukweli huu, aliwaita mabwana zake wa Magharibi kwa kusema "Mimi ndio ngome ya mwisho ya usekula katika eneo la Mashariki ya Kati na kama nitaanguka, siasa mpya za eneo hili zitaibuka kuanzia Morocco hadi Indonesia".

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria, Walid Muallem, aliashiria ukubwa wa ukweli huo kwa kusema, "Tunapigana sio tu kuulinda utawala wa Syria, bali pia kuzilinda Lebanon, Jordan na Uturuki dhidi ya wale wanaolingania kuwepo kwa Khilafah ya Kiislamu."

Amerika, ambayo ndiye mmiliki wa utawala wa Assad, alipanga azimio la Umoja wa Mataifa Na. 2254 ambalo linalichukua suluhisho la kisekula la Syria kama msingi na haimchukulii Bashar al-Assad kuwa mwenye hatia na kuufanya ulimwengu kulikubali na kugawanya dori na watendaji kulingana na uhalisia huu.

Iran na wanamgambo wake waliingia vitani na Waislamu nchini Syria kulingana na uhalisia huu. Urusi iliingia Syria na kufanya mauaji ya kikatili ili kutokumbana na uhalisia huu, ambao pia unatishia eneo lake la ndani. Daesh na PKK waliletwa nchini Syria ili kuharibu uhalisia huu na kuwa mamlaka.

Kwa kuzingatia ukweli huu, Uturuki ilitumia vibaya hisia za Wasyria wanaodhulumiwa kwa kufungua milango yake, kuwakaribisha na kuandaa upinzani nchini Uturuki ili kuwaingiza usekula, na kusaidia kuiregesha miji iliyokombolewa kama vile Aleppo mikononi mwa utawala kupitia kuyaondoa makundi ya mujahidina kutoka maeneo yao pamoja na operesheni ilizozipanga dhidi ya kile kinachoitwa ugaidi, hasa 'Ngao ya Furaat'. Aliileta utawala kwenye miguu ambapo ulikuwa karibu kuporomoka.

Pamoja na Mikutano ya Astana na Sochi, mazungumzo ya Kikatiba jijini Geneva yalifanyika na yangali yanafanyika ili kugeuza ulisia huu.

Huu ni ukweli ambao Waziri wa Mambo ya Nje wa zamani wa Marekani, Hillary Clinton alisema kuuhusu, "Naingiwa na kichaa kwa sababu ya mgogoro wa Syria." Obama alisema suala la Syria lilitia mvi nywele zake. Kwa mara nyengine, huu ni ukweli ambao umewafichulia watu imani na upotovu.

Sasa, ili kuangamiza kikamili ulisia huu (kukabiliana na pigo la mauti pindi dhurufu zinazofaa zitakapotokea), majaribio maovu yanafanywa chini ya usimamizi wa serikali ya Uturuki, ambapo udhaifu wa kiuchumi na sera za wakimbizi zisizo na uaminifu ilizozipitia zimegeuka kuwa nyenzo za uchaguzi dhidi yake yenyewe, chini ya usukani wa Amerika, iliyouacha mzozo wa Syria utulie kwa muda. Wanataka kuwakabidhi watu wa Syria kwa muuaji wao kwa jina la "amani"                                                                                                              

Hata hivyo, kwa kumiminika viwanjani, Waislamu wa Syria walionyesha kuwa hili sio rahisi hivyo. Waliweka upya kiapo chao kwamba kamwe hawatawahi kufanya amani na utawala huo wa kihalifu, lakini wataendeleza na mapambano hadi watakapoupindua. Kwa sababu ukweli unatokana na mawazo, na ukishatulia moyoni, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, uwongo hauwezi kuushinda!

Maadamu Waislamu wa Syria watakata uhusiano wao wote na nchi kama Uturuki, ambazo nia zao mbaya zimefichuliwa, msiwape imani wanamapinduzi wa hoteli wanaokimbilia kuuza mapinduzi yao leo kama walivyofanya jana, wakining’inia kwenye uzi wa imani, rudini kwenye misimamo mikali ya mapinduzi ili kuifanya Damascus kuwa kitovu cha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume pambizoni mwa uongozi makini wa kisiasa, na mukitaraji msaada kutoka kwa Mwenyezi Mungu Peke Yake!

(اِنَّ اللّٰهَ يُدَافِعُ عَنِ الَّذ۪ينَ اٰمَنُواۜ اِنَّ اللّٰهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ خَوَّانٍ كَفُورٍ۟)

“Hakika Mwenyezi Mungu huwakinga walio amini. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila khaini mwingi wa kukanya mema.” [Surah Al-Hajj 38]

 

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Muhammed Emin Yildirim

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu