Jumatano, 04 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Je, Uislamu Unaweza Kuwepo bila ya Qur’an na Sunnah Ewe Erdoğan?

(Imetafsiriwa)

Habari:

Akizungumza katika Mkutano wa Baraza Pana la Ushauri Mkoa wa Istanbul la Chama cha AK uliofanyika katika Haliç Congress Center, Rais Recep Tayyip Erdoğan alisema, “Hakuwezi kuwa na fikra ya Alevi bila ya Mwenyezi Mungu, Muhammad na Ali. Hakuna ubinadamu kwa wale waliojengwa juu ya uchochezi mpotovu.” (03.09.2022 Yeni Şafak)

Maoni:

Erdoğan, ambaye hajatawa kwa mujibu wa Qur'an na Sunnah tangu aingie madarakani mwaka wa 2002, ana ufahamu wa kiroho kuhusu Uislamu na mtu kuwa Muislamu. Erdoğan, ambaye anawatawala watu wa Uturuki kwa mujibu wa mfumo wa kirasilimali katika uchumi, utawala, elimu, jamii na nyanja nyingine za maisha, anaweka mipaka ya Uislamu na mtu kuwa Muislamu kwa ibada na maadili pekee. Kwa maana nyengine, kwa mujibu wa Erdoğan, Uislamu na mtu kuwa Muislamu ni dini ya kiroho ambayo hudhibiti mahusiano kati ya Muumba na mja. Haina athari juu ya uhusiano wa mwanadamu na watu wengine. Ingawa hakiri hili kwa ulimi wake, matendo yake ni ushahidi wa hili.

Tunauliza yafuatayo: “Ikiwa hakuna fikra ya Alevi bila Mwenyezi Mungu, Muhammad, na Ali”, je kutakuwa na Uislamu bila ya Qur’an na Sunnah? Je, utaitwa ni Uislamu ikiwa uchumi, utawala, siasa na sera za nje, yaani hukmu na nidhamu, zinachukuliwa kutoka katika mfumo ya kirasilimali ulioingizwa kutoka Magharibi huku ibada zikichukuliwa kutoka katika Qur’an na Sunnah? Je, itaitwa ni Uislamu kutabanni, kubeba na kutekeleza fikra za kisekula za kirasilimali huku baadhi ya hisia ni za Kiislamu?

Uislamu sio kama Uyahudi na Ukristo. Dini hizi hazina kanuni kuhusiana na kila nyanja ya maisha. Zimefungika tu na kipengee cha kiroho pekee. Lakini Uislamu hauko hivyo. Uislamu ni mfumo mithili ya urasilimali na ukomunisti. Una kanuni kuhusiana na kila nyanja ya maisha, kuanzia ibada yake hadi uchumi wake, utawala, elimu na sera yake ya kigeni. Kwa kifupi, ni dini ya kisiasa. Kuufunga Uislamu kwenye kipengee chake cha kiroho, kama vile Ukristo, na kuacha kipengee chake cha kisiasa, ina maana ya kutumikia maslahi ya makafiri, kuwa watumwa wao na kubakia watumwa wao. Kwa sababu kuufahamu Uislamu kiroho pekee hakutokamani na Uislamu. Uislamu uko mbali na ufahamu huu. Ufahamu huu ni ufahamu ambao kafiri mkoloni Magharibi waliuingiza ndani ya Waislamu, na ili kudumisha utawala wake, watawala vibaraka waliwekwa juu ya Waislamu kama walinzi. Mwenyezi Mungu (swt) amesema kuhusu watu kama hao:

(اَفَتُؤْمِنُونَ بِبَعْضِ الْكِتَابِ وَتَكْفُرُونَ بِبَعْضٍۚ)

 “Je! Mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakataa baadhi yake? [Surah Al-Baqarah 85]. Kwa mujibu wa aya hii, je, wale ambao, kama wanasiasa wa leo, wangeitii Qur'an katika ibada, hawangefuata mfumo wa kirasilimali badala ya Qur'an katika nyanja kama vile uchumi, utawala na mfumo wa kuadhibu, na kuichukua Magharibi kama Kibla, wanakanusha baadhi ya aya za Mwenyezi Mungu (swt)? Ijapokuwa hawakanushi waziwazi kwa ndimi zao kwa sababu wanaogopa rai jumla ya Waislamu, bali wanakanusha kwa vitendo vyao.

Katika Qur’an na Sunnah, kuna ahkaam zinazohusiana na ununuzi, biashara, sera za kigeni, adhabu na mfumo wa kijamii pamoja na ahkaam kuhusu ibada. Kusema kuwa kuna nass (andiko) ya wazi kuhusu riba, huku ukikosa kuharamisha riba katika nyanja zote za maisha, kutotawala kwa yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu ijapokuwa anasema anaamini na kumtegemea Mwenyezi Mungu, kutofunga na kuruhusu viwanda vinavyozalisha pombe ijapokuwa anataka vijana wa dini wajue kuwa pombe ni haram si chochote ila manufaa ya kisiasa, unyonyaji na kuwa mtumwa wa mfumo wa kirasilimali na Magharibi.

Muislamu ni mtu aliye na mshikamano katika vitendo na mazungumzo. Kitendo na mazungumzo yake haviwezi kutofautiana. Hata hivyo, inawezekana kukutana na tofauti za vitendo na mazungumzo ya watawala vibaraka katika nchi zetu, ambayo ni zao na ujenzi wa mfumo wa kirasilimali katika nyanja zote za maisha kama katika mifano ya hapo juu ya riba, pombe na mifano mingine isiyo na idadi. Qur’an wanayoisoma haiendi zaidi ya koo zao. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema katika moja Hadith:

«يقرأون القرآن لا يجاوز حناجرهم»

Wanaisoma Qur’an. Lakini haiendi zaidi ya koo zao.” [Tirmidhi]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ercan Tekinbaş

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu