Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Urusi iko Mbioni Kutafuta Upendeleo kwa Amerika

Wakati Huu Barani Afrika

 (Imetafsiriwa)

Habari:

Katika mji mkuu wa Mali, Bamako, mamia ya raia walifanya maandamano wakitaka kikosi cha jeshi la Ufaransa kuondoka katika ardhi ya nchi hiyo.

Waandamanaji walikusanyika karibu na Mnara wa Afrika, moja ya alama za Bamako, na kuimba miito ya kutaka kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa walioko nchini Mali tangu 2014 kama sehemu ya Operesheni Barkhane.

Mahusiano kati ya nchi hizo mbili yamezorota baada ya madai kuwa wanajeshi wa Wagner PMC watawekwa nchini Mali, hali hiyo imeongezeka hata zaidi huku kukiwa na maneno makali kutoka kwa maafisa.

Ufaransa mnamo Januari 12 iliwasilisha rasimu ya azimio kuhusu vikwazo dhidi ya Mali kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UNSC). Hati hiyo ilizuiwa kwa sababu ya kura ya turufu ya China na Urusi.

Maoni:

Operesheni Barchan ya kijeshi ya Ufaransa nchini Mali kwa hakika ni mwendelezo wa Operesheni Serval iliyoanzishwa na Ufaransa mwaka 2013 ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya kisiasa katika koloni yake ya zamani. Tofauti pekee ni kwamba pamoja na Mali, wigo wa utekelezaji wake ulienea hadi mataifa manne jirani - Mauritania, Burkina Faso, Niger na Chad.

Kama tunavyojua, tangu mwisho wa karne ya 19, baada ya miongo kadhaa ya upinzani mkali wa Waislamu, eneo la Mali ya sasa, kama nchi zengine za Afrika Magharibi, lilitawaliwa na Ufaransa. Katika miaka ya 60 ya karne ya 20, ilipata uhuru kama sehemu ya sera ya kuondoa ukoloni chini ya mwamvuli wa UN, kama utekelezaji wa Mkataba wa Atlantiki wa 1941, ambayo kwa mujibu wake, kwa kuunga mkono Vita vya Pili vya Dunia, Wazungu waliiahidi Amerika mwanya sawa wa unyonyaji na uporaji wa makoloni yao.

Baada ya kupata uhuru rasmi, Mali iliondoka katika Jumuiya ya Kifaransa, ambayo ilitumika kama urithi wa kikoloni wa Ufaransa barani Afrika. Hata hivyo, baada ya mapinduzi ya kijeshi ya 1968, Ufaransa ilifanikiwa kuregesha ushawishi wake na kuirudisha Mali katika duara lake la maslahi ndani ya muundo wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS). Amerika iliendelea kufanya kazi ya kunyakua utawala katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na kuunda matatizo ya kiuchumi, kisiasa na kikabila.

Mnamo mwaka 2012, Watuareg wanaoishi kaskazini mwa Mali, wakiwa wamekamata silaha zinazodaiwa kuwalenga waasi nchini Libya, wakiungwa mkono na baadhi ya makundi ya kijihadi, waliasi na kutangaza kuundwa kwa taifa huru la Azawad.

Jeshi, likimtuhumu rais kwa kushindwa kuzima ghasia, lilifanya mapinduzi. Katika hali hiyo, Ufaransa ilituma kikosi chake cha kijeshi nchini Mali, kwa kisingizio cha kuwalinda raia wake, kulinda hadhi ya ardhi ya nchi hiyo na kuikomboa kutoka kwa wanamgabo wa Kiislamu.

Makubaliano kati ya jeshi la junta la Mali linalotawala na PMC Wagner yanatoa ushuhuda wa nia ya kulibadilisha jeshi la Ufaransa kwa mamluki wa Urusi. Na, licha ya Moscow kukataa uhusiano wake na Wagnerites, kila kitu kinaashiria ukweli kwamba, kama ilivyokuwa kwa Syria na Libya, Urusi nchini Mali yakubali kutumikia kwa bidii maslahi ya Amerika.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Abu Ibrahim Bilal
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu