Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Wanawake wa Kiislamu Nchini India Watolewa Ofa ya Kuuzwa na Mabaniani Wenye Misimamo Mikali Kama Sehemu ya Muendelezo wa Utesaji Waislamu Nchini Humo

 (Imetafsiriwa)

Habari:

Katika wiki za hivi karibuni, kumekuwa na ghadhabu iliyoonyeshwa kwenye programu iliyoundwa na Mabaniani wenye misimamo mikali nchini India ambayo iliwaweka zaidi ya wanawake mia moja wa Kiislamu "katika mauzo" katika "mnada" ghushi. Programu hiyo, inayoitwa "Bulli Bai", neno la dharau linalotumiwa na Mabaniani wengi wa mrengo wa kulia kuwaelezea wanawake wa Kiislamu, ilitoa picha za wanawake wa Kiislamu na kuzipakia katika mazingira machafu na kuziweka kwa "mauzo". Wengi wa wanawake hao walikuwa wanaharakati, waandishi wa habari, mawakili na watu wengine wenye ushawishi mkubwa ambao wamekuwa wakipinga unyanyasaji wa Waislamu nchini India. Mmoja wa wahasiriwa wa uhalifu huu wa kuchukiza wa chuki alikuwa Fatima Nafees, mama mwenye umri wa miaka 65 wa mwanafunzi aliyetoweka Najeeb Ahmed ambaye alitoweka katika chumba chake cha kulala cha chuo kikuu miaka 5 iliyopita chini ya hali ya kutatanisha baada ya kushambuliwa usiku uliotangulia na wanachama wa chama cha wanafunzi cha utaifa wa Kibaniani cha ABVP. Programu hiyo ya Bulli Bai imekuja miezi sita baada ya programu kama hiyo iitwayo “Sulli Deals” ambayo ilipakia picha za wanawake zaidi ya 80 wa Kiislamu wa Kihindi na kuziweka kwa mauzo, na kuwapa wanaozuru programu hiyo fursa ya kudai wanawake hao, na kuwaita "dili za siku".

Neeraj Bishnoi, mshukiwa mkuu katika programu ya Bulli Bai inayotumiwa na watu wenye misimamo mikali wa mrengo wa kulia 'kuwapiga mnada' wanawake wa Kiislamu - ametishia kujiua akiwa chini ya ulinzi wa polisi wa Delhi, aliarifu DCP wa kitengo maalum cha Intelligence Fusion and Strategic Operations (IFSO) KPS Malhotra. "Mshukiwa amekiri kuwa anawafahamu waundaji wa 'Sulli Deal', programu ambayo wanawake wa Kiislamu walipigwa mnada. Pia amekubali kuwa ana akaunti ya mtumizi ya Sweta Singh, ambaye amekamatwa na polisi wa Mumbai", alisema Bwana Malhotra. (NDTV)

Mnada wa mtandaoni mithili ya huo wa wanawake wa Kiislamu nchini India pia ulifanyika wakati wa Eid al-Fitr mwaka jana, ambapo chaneli ya You-tube inayoendeshwa na "Liberal Doge Live" ilichapisha video ya ngono iliyokuwa na picha za wanawake wa Kiislamu, ikiiita "Eid Maalum”.

Maoni:

Programu hizi za kinyama zinalenga kushusha hadhi, kudhalilisha, kufedhehesha, kutishia na kunyamazisha wanawake wa Kiislamu nchini India kwa uhalifu wa utawala wa Kibaniani wa BJP na wafuasi wengine wa imani ya Hinduvta ambayo inapigia debe dola ya kabila la Kibaniani nchini humo. Huu ni mkono mwingine tu wa muendelezo wa unyanyasaji na kuteswa kwa Waislamu nchini India ambao wahalifu wake, mara nyingi zaidi, wanaruhusiwa kutekeleza uhalifu wao bila kuadhibiwa. Mnamo mwezi Disemba mwaka jana, mkusanyiko ulifanyika huko Haridwar, kaskazini mwa jimbo la Uttarakhand, ambapo viongozi wa kidini wa Kibaniani walitoa wito hadharani wa mauaji ya halaiki ya Waislamu nchini India, wakienda sambamba na vitendo vya mauaji ya jeshi la Myanmar dhidi ya Waislamu wa Rohingya. Serikali ya BJP ilishindwa kutoa hata tamko moja la kulaani dhidi ya maandamano na hotuba za uchochezi. Kwa kweli, iliripotiwa kwamba mkutano huo ulihudhuriwa na angalau mwanachama mmoja wa chama tawala cha Waziri Mkuu Narendra Modi. Mwaka jana, zaidi ya misikiti kumi na mbili katika jimbo la Tripura kaskazini mashariki mwa India iliharibiwa na umati wa Mabaniani. Wakati huo huo, vurugu na mateso ya kimpangilio dhidi ya Waislamu huko Assam na mamlaka ya Kibaniani, ikiwa ni pamoja na kufukuzwa kwa lazima kutoka kwa nyumba zao, sasa imethibitishwa vyema. Na kwa miezi kadhaa sasa, makundi ya Kibaniani yamejaribu kutatiza swala za Jummah zinazoswaliwa katika maeneo ya umma huko Gurgaon karibu na New Delhi. Na bado, hakuna uongozi hata mmoja, mtawala hata mmoja, dola hata moja ulimwenguni leo inayokuja kuwasaidia ndugu na dada zetu Waislamu wanaokandamizwa. Hakika kukosekana kwa dola ya kutetea maslahi ya waumini na Dini yetu ndiko kunakowapa ujasiri maadui wa Uislamu kuwalenga Waislamu na kutekeleza jinai zao za kinyama na chafu, zikiwemo dhidi ya heshima ya dada zetu bila ya kuhofu matokeo.

Hinduvta hawa wenye misimamo mikali wanapaswa kujua kwamba heshima ya dada zetu ni takatifu katika Uislamu. Ulinzi wake umewekwa katika kiwango cha kulinda maisha yenyewe. Kwa hakika, Qur’an inafafanua kutamka hata neno moja la kashfa dhidi ya sifa ya mwanamke msafi kuwa ni jinai kubwa inayostahiki adhabu kali. Mtume (saw) alilifukuza kabila zima la Kiyahudi, Banu Qaynuqa, kutoka katika Dola ya Kiislamu mjini Madina kutokana na unyanyasaji wao dhidi ya mwanamke mmoja wa Kiislamu. Karne ya 9 Khalifah, al-Mu’tassim, alituma jeshi kubwa kumuokoa mwanamke mmoja Muislamu aliyekuwa ametekwa nyara na Warumi. Khalifah wa karne ya 8, al-Walid bin Abdul Malik alikusanya jeshi la kutisha, likiongozwa na jenerali mkubwa wa Kiislamu Muhammad ibn Qasim, kuokoa kundi la wanawake na watoto wa Kiislamu waliokuwa wamefungwa na Mfalme dhalimu wa Kibaniani wa India, Raja Dahir, na kuiweka Sind chini ya utawala wa Uislamu katika mchakato. Mtume (saw) na viongozi wa kweli wa Uislamu walionyesha ukali wa mwitikio unaohitajika katika Uislamu pale hadhi ya wanawake wa Kiislamu inapochafuliwa. Kwa hivyo vipi urithi wao utafuatwaje leo wakati heshima ya dada zetu nchini India na ulimwenguni kote inanajisiwa? Je, haihitaji kusimamishwa kwa dola ambayo kwa hakika inathamini hadhi yao kwa namna ambayo Qur’an na Sunnah imefafanua? Je, haihitaji uongozi wa kweli wa Kiislamu unaokumbatia kwa bidii wajibu wake wa Kiislamu wa kulinda heshima yao? Je, haihitaji mtawala wa Kiislamu mwenye ikhlasi ambaye atakusanya jeshi lake bila ya kusita kuwalinda, kama vile Khulafaa’ (makhalifa) wa zamani? Hakuna dola nyingine ambayo chini yake yote haya yatatokea zaidi ya Khilafah kwa njia ya Utume. Hivyo tunawalingania Waislamu wa India na duniani kote kujiunga na kazi muhimu mno ya Kiislamu ya Hizb ut Tahrir katika kusimamisha dola hii tukufu kwa dharura; dola ambayo itaregesha usalama kwa Ummah huu, kuukomboa kutokana na ukandamizwaji wake na kutovumilia unyanyasaji wa mwanamke hata mmoja wa Kiislamu mikononi mwa maadui wa Uislamu!

 [وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَى لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُم مِّن بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا وَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ فَأُوْلَئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyo wapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [An-Nur: 55]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya f Hizb ut Tahrir na

Dkt. Nazreen Nawaz
Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu