Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mkutano wa OIC jijini Islamabad ni wa Kuwafanya Waislamu wa Afghanistan Waipigie Magoti Amerika

(Imetafsiriwa)

Habari:

Waziri wa Mambo ya Nje Shah Mahmood Qureshi mnamo siku ya Alhamisi, tarehe 16 Disemba 2021, alisema kuwa pamoja na wanachama wa jumuiya ya kimataifa na Taliban kuwepo kwenye jukwaa moja, mkutano wa Disemba 19 wa OIC jijini Islamabad utathibitisha kuwa ni ngazi ya kutafuta suluhisho la janga la kibinadamu nchini Afghanistan. Waziri huyo wa mambo ya nje alisema, kwa kuandaa hafla hiyo, Pakistan ilikuwa inacheza dori chanya kwa kuziba pengo la mawasiliano kati ya ulimwengu na Taliban.

Maoni:

Tangu kuondoka kwa fedheha kwa Biden kutoka Afghanistan, Amerika inajaribu kuifanya serikali ya Taliban ifeli kupitia kuanzisha majanga ya chakula na ukosefu wa ajira. Afghanistan ni nchi isiyo na bahari, inayohitaji usaidizi wa majirani zake kwa ajili ya biashara. Kati ya nchi sita jirani, Pakistan, Iran, Turkmenistan, Uzbekistan, Tajikistan, na China, ni Pakistan pekee ambayo inaweza kumaliza majanga haya kupitia kufungua mpaka wake. Hata hivyo watawala wa Pakistan wanafuata maagizo ya Washington ya kukataa kuutambua utawala mpya wa Kabul hadi utakapopiga magoti mbele ya Jumuiya ya Kimataifa.

Madhumuni ya Mkutano wa OIC ni kuwasilisha ujumbe wa Biden kwa Taliban ya Afghanistan kwamba watawala wote wa nchi za Kiislamu wanasimama kidete na mabwana zao wa Magharibi. Ni kutuma ujumbe kwamba ili kupata uwezeshaji wa kusuluhisha migogoro, Taliban lazima itulize moyo wa Jumuiya ya Kimataifa kwa kuachana na kuhukumu kwa Shariah ya Kiislamu kwa namna yoyote ile.

Kama watawala wa nchi za Kiislamu wangekuwa na ikhlasi kwa Waislamu wa Afghanistan, wangalitangaza tu uungaji mkono kamili badala ya kukusanyika pamoja Islamabad kwa ajili ya Biden. Hakuna hata dola moja ya Kimagharibi, ikiwemo Amerika, itakuwa katika nafasi ya kuwazuia lau kama wangefanya hivyo. Watawala wanafanya kazi kuifanya Taliban ipige magoti licha ya kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), iliyopokelewa na Abdullah bin Umar kwamba,

«الْمُسْلِمُ أَخُو الْمُسْلِمِ، لاَ يَظْلِمُهُ وَلاَ يُسْلِمُهُ» “Muislamu ni ndugu ya Muislamu mwengine, hamdhulumu wala hamsalimishi (kwa adui).” (Bukhari and Muslim). Hata hivyo, watawala hawa watawaruhusu watoto na wanawake wa Afghanistan kufa njaa na kuganda wakati wa baridi hadi Taliban isalimu amri kwa Magharibi na ukafiri wake. Mwenyezi Mungu (swt) awakamate na kuwamaliza watawala hawa waovu hivi karibuni.

Suluhu pekee ya kumaliza mateso ya Waislamu wa Afghanistan ni kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume, ili Pakistan, Afghanistan na dola za Asia ya Kati ziwe kitu kimoja. Dola hii ya Khilafah haitakuwa tegemezi kwa dola za kikafiri, kwani itakuwa tajiri na inayojitosheleza kwa nishati, madini na kilimo, pamoja na kuwa na jeshi imara lenye silaha za nyuklia. Hakika Khilafah ni hitajio la wakati.

 Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Shahzad Shaikh
Naibu wa Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu