Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kupungua kwa Idadi ya Watu Kwaipa Tumbojoto Singapore

(Imetafsiriwa)

Habari:

Ripoti ya kila mwaka ya Idadi ya Watu kwa Ufupi ilionyesha idadi jumla ya watu kufikia Juni ilipungua kwa mwaka wa pili mfululizo, hadi milioni 5.45 - ikishuka kwa asilimia 4.1 punguo kubwa zaidi la mwaka kwa mwaka tangu 1950. Idadi ya watu wasio wakaazi ilipungua kwa asilimia 10.7 hadi milioni 1.47. Na kwa mara ya kwanza tangu 1970, idadi ya raia na wakaazi ilisajili kupungua mwaka hadi mwaka. Idadi ya ndoa za raia mwaka jana - 19,430 - ilikuwa ni ya chini zaidi tangu 1986, na kiwango cha raia wa kimataifa kilipungua hadi asilimia 30, ambayo ni ya chini zaidi tangu 1997.

Ambako kulikuwa na ongezeko, na kwa kasi zaidi kuliko hapo awali, ni hisa ya raia wenye umri wa miaka 65 na zaidi. Hii iliongezeka hadi asilimia 17.6 kufikia Juni, kutoka asilimia 16.8 mwaka jana na asilimia 10.4 mwaka 2011. Idadi ya wazee inatarajiwa kufikia asilimia 23.8 mwaka 2030. Idadi ya watu waliozeeka na wasiojizalisha inaweka mapengo katika soko la ajira, ambalo tangu jadi Singapore imekuwa iking'ang'ana na vyombo vya sera za uhamiaji na uagizaji wa wafanyikazi wahamiaji kutoka nje. Mwaka huu, kupungua kukubwa kwa sehemu ya wasio wakaazi kulisukumwa pakubwa na wamiliki wa vibali vya kazi katika ujenzi, uwanja wa meli za baharini na sekta za utengezaji, ambazo huunda asilimia 20 ya wageni hapa, ambao hufanya kazi ambazo watu wa Singapore huzikimbia.

Mazungumzo juu ya kupunguza utegemezi wa Singapore kwa wafanyikazi wa kigeni ni ya muda mrefu. Mawazo na mipango ambayo imekuwa ikijadiliwa juu ya uwekezaji anuwai kuanzia mitambo na teknolojia kwa sekta za mishahara ya chini, hadi kukuza na kuelimisha katikati ya kushindania dori za kitaalam, usimamizi na dori za kiutendaji. (Strait Times)

Maoni:

Singapore imekuwa ikikabiliwa na changamoto za muundo wa idadi ya watu tangu miaka iliyotangulia. Hii sio tu athari ya janga lakini janga hili huongeza tu tatizo hili zaidi na zaidi kwa machoni.

Ni jambo lisilowezeka kukataliwa kuwa Singapore inakabiliwa na janga la idadi ya watu wanaozeeka, ambalo ndilo haswa lililotokea katika nchi za Ulaya, Japan na Korea Kusini; kwa sababu ya hulka yao ya huria na ya kibepari ambayo imedhoofisha umuhimu wa kujenga familia. Huu ndio ugonjwa wazi wa jamii ya kisekula.

Utabiri wa wanadiplomasia tangu 2015 umesema kuwa Asia Mashariki itakabiliwa na tishio kubwa zaidi la idadi ya watu, ambayo ni: kutoweka. Korea Kusini, Japan, Taiwan na Singapore wanajitahidi kufadhili mzigo wa manufaa ya kijamii kwa idadi yao ya wazee inayoendelea kukua.

Ni dhahiri Urasilimali umeharibu ujenzi wa familia na jamii na kulemaza uhai wa taifa. Je! Mwenyezi Mungu Aliyetukuka hakutuuliza ndani ya Qur'an tuchukue mafunzo kutoka kwa hadithi za uharibifu wa mataifa juu ya mgogo wa ardhi?

 [قُلْ سِيْرُوْا فِى الْاَرْضِ فَانْظُرُوْا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الَّذِيْنَ مِنْ قَبْلُۗ كَانَ اَكْثَرُهُمْ مُّشْرِكِيْنَ]

“Sema: Safirini duniani muangalie ulikuwaje mwisho wa walio tangulia. Wengi wao walikuwa washirikina.” [QS. Ar-Ruum: 42]

Kwa hivyo, tunapaswa kutafuta njia mbadala ya kimfumo inayofaa kwa jamii ya Waislamu, kuilinda kutokana na aina hii ya kudidimia kwa watu. Mfumo unaoenda sambamba na maumbile ya mwanadamu lakini pia ilio na utaratibu wa maendeleo ya hadhara. Mfumo huu sio mwengine isipokuwa ni Uislamu.

Kama nukuu inavyosema: "Ikiwa Amerika itatumia mamilioni ya dolari kwenye utafiti ili kusuluhisha matatizo ya kijamii katika jamii yake, basi Uislamu huondoa tabia ambazo zimeota mizizi katika jamii ya wajinga kwa aya chache tu za Quran" - Sayyid Qutb. Ruwaza ya Kiislamu inahakikisha kuwa mamboleo na maendeleo hayatasababisha usumbufu na uharibifu wa kijamii katika jamii; ili maendeleo ya kiteknolojia katika Uislamu yasihitaji gharama za kijamii mithili ya jamii ya kirasilimali. Kwa hivyo chukua funzo!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Fika Komara

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu