Uzbekistan na Hizb ut Tahrir
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Lau kama fikra za Hizb ut Tahrir zisingeenea sana nchini Uzbekistan, zisingekumbana na kiwango hiki cha kukamatwa na kuteswa, kwani maiti hapigwi vita.
Lau kama fikra za Hizb ut Tahrir zisingeenea sana nchini Uzbekistan, zisingekumbana na kiwango hiki cha kukamatwa na kuteswa, kwani maiti hapigwi vita.
Kenya, imekumbwa na maandamano makubwa katika masiku ya hivi majuzi baada ya bunge kupitisha mswada wa kuongeza ushuru – ikiwa ni pamoja na mahitaji ya kila siku kama vile mafuta ya kupikia, nepi, na mkate – kwa idadi ya watu ambao tayari wanakabiliwa na mfumko wa bei na viwango vya juu vya ukosefu wa ajira. Rais Ruto alikataa kutia saini mswada huo baada ya maandamano makubwa ambayo kufikia sasa watu 39 wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa.
Hali mjini Gaza inazidi kuwa mbaya. Umbile haramu la Kiyahudi linaendelea na mashambulizi yake, na kusababisha idadi ya vifo ambayo sasa imefikia 37,000, na zaidi ya 82,000 kujeruhiwa. Inajulikana sana kuwa hakuna maeneo salama kabisa yaliyosalia kwa wakaazi wa Gaza kutafuta kimbilio kutokana na mashambulizi ya umbile hilo haramu la Kiyahudi. Takriban Waislamu wote wa Gaza sasa wanalazimika kuyahama makaazi yao, wakitafuta hifadhi hadi kusini mwa Rafah, karibu na mpaka wa Misri.
Zaidi ya mahujaji Waislamu 1,300 waliripotiwa kufariki wakati wa Hija ya kila mwaka, au hija ya Makka, mwezi huu nchini Saudi Arabia, ambapo halijoto imepanda zaidi ya nyuzi joto 50 (nyuzi 122 za Fahrenheit). Mfiduo usiodhibitiwa wa joto kali unaweza kusababisha aina mbalimbali za madhara ya kiafya yanayojulikana ikiwemo kufeli kwa viungo vya mwili na hata kifo.
Mnamo tarehe 24 Mei 2024, kitengo cha habari cha jeshi la Pakistan kilisema kuwa, “Mkuu wa Majeshi yuko katika ziara rasmi katika Jamhuri ya Shirikisho ya Ujerumani... Uongozi wa Ujerumani ulitambua dori ya Jeshi la Pakistan katika mapambano dhidi ya Ugaidi.”
Ingawa vyombo vya habari vinaitwa “nguzo ya nne ya demokrasia,” vikionyesha kutoegemea upande wowote na fikra yake, kama mamlaka ya mahakama kwa mfano, uhalifu uliofanywa na serikali ya Kiyahudi huko Gaza, na katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina, ulitosha kufichua madai haya. Uhalifu huo ulifichua ukweli kuhusu vyombo vya habari na wanahabari. Jinai hizo zilionyesha wazi kwamba hakuna mamlaka ya kimaadili au uhalali, bali kwa ajili ya nguvu ya unyama, inayowakilishwa na dola za kimataifa na silaha zao duniani, ikiwemo Ulimwengu wa Kiislamu, ikiwa ni pamoja na watawala, serikali, na taasisi za vyombo vya habari.
Uongozi wa juu wa Pakistan umeidhinisha kuanzishwa kwa operesheni mpya ya kijeshi Inayoitwa Azm-e-Istehkam. Mpango huo mpya wa kijeshi unatarajiwa kuangazia vitisho vya usalama wa ndani na wapiganaji wenye silaha wanaovuka kutoka Afghanistan, huku kukiwa na taharuki inayoongezeka kati ya Islamabad na watawala wa Taliban jijini Kabul.
Gazeti la ‘The Daily Times’ liliripoti kuwa, “Sindh anasimamisha benki ya maziwa ya binadamu, inauregesha mpango huo kwa Baraza la Itikadi la Kiislamu... Benki ya kwanza ya maziwa ya binadamu nchini Pakistan iliundwa mapema mwezi huu na Taasisi ya Sindh ya Afya ya Mtoto na Matibabu ya Watoto (Neonatology)
Ufahamu wa mfumo wa mahakama wa Uturuki kuhusu uadilifu ni kuwaadhibu Waislamu wanaopinga ukatili unaofanywa dhidi ya Waislamu nchini Uturuki na duniani kote, na kuwaachilia huru wanasiasa wanaolaghai umma, na ni kuwatangaza Waislamu wenye fikra za Kiislamu, na wanaotamani maisha ya Kiislamu, ambao hawajatenda jinai yoyote, kuwa ni magaidi na kuwahukumu kwenye dhulma, mateso na kifungo.
Katika miaka michache iliyopita, siasa nchini Kyrgyzstan zimebadilika kutoka mfumo huria wa vyama vingi hadi udikteta katili kama vile Tajikistan na Kazakhstan. Ingawa hapo awali vyama vyenye maoni tofauti vilikuwepo bungeni na vilipata fursa huru ya kushindana, leo kila kitu kinaamuliwa na Rais S. Zhaparov.