Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Mtazamo kwa Ghasia za Baada ya Uchaguzi wa Msumbiji

(Imetafsiriwa)

Habari:

Kwa mujibu wa Kituo cha Demokrasia na Haki za Binadamu cha Msumbiji na shirika la Reuters, kufikia tarehe 8/11/2024, jumla ya vifo 34 viliripotiwa huku vyanzo vyengine vikisema kuwa waliouawa ni zaidi ya 50, kutokana na ghasia za baada ya uchaguzi. kutangazwa kwa mgombea wa chama tawala cha Front for Liberation of Msumbiji (Frelimo), Daniel Chapo kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika mnamo Oktoba 24 mwaka huu ambapo wapinzani walidai kuwa matokeo ya kura yaliibwa.

Maoni:

Vurugu za uchaguzi zimekuwa sehemu ya chaguzi za kidemokrasia kote duniani na hali inayojulikana katika mataifa yanayoendelea. Ripoti za kimataifa zinakadiria kuwa vurugu hutokea kwa takriban 19%, na takriban 58% ya uchaguzi barani Afrika. Mwanzoni mwa miaka ya tisiini ilifikia 86%.

Baadhi ya mifano ya ghasia za uchaguzi katika baadhi ya nchi za Afrika:

Nchini Tanzania tangu uchaguzi wa kwanza wa urais wa vyama vingi uliofanyika mwaka 1995, kuibuka tena kwa ghasia za baada ya uchaguzi kumekuwa jambo la mfululizo na lisiloisha katika kila baada ya miaka mitano.

Jambo la kuhuzunisha zaidi ni baada ya uchaguzi wa mwaka 2000 ambapo zaidi ya wafuasi 40 wa chama cha upinzani (CUF) visiwani Zanzibar (visiwa vyenye mamlaka nusu kujitawala) waliuawa kwa kupigwa risasi, zaidi ya 600 kujeruhiwa na wanaokadiriwa kufikia 2,000 walikimbilia nchi jirani ya Kenya, wakati vyombo vya dola vilipofyatua risasi kwa umati wa watu waliokuwa wakipinga matokeo ya kura.

Mnamo Disemba 2007 hadi Februari 2008 nchini Kenya zaidi ya watu 1,200 waliuawa na wengine 350,000 walikimbia makaazi yao, Côte d'Ivoire mwaka wa 2010 ambapo takriban watu 3,000 waliuawa, Senegal mwaka 2012 ambapo hadi vifo 15 na vurugu zinazoendelea sasa 2024 nchini Msumbiji ambapo zaidi ya watu 50 wameuawa, tukitaja chache.

Sababu kuu ya ghasia za uchaguzi nchini Msumbiji, Afrika na ulimwengu kwa jumla bila shaka ni maumbile ya msingi ya itikadi ya ubepari ambapo mfumo wa kisiasa wa demokrasia umechipuka. Msingi wa kibepari wa usekula unapigia debe maovu na mtazamo usio ingia akilini wa kutenganisha dini na utawala ambao unahitimisha mwanadamu kunyimwa hisia za maadili ya kiroho, na badala yake ukawasukuma kujihusisha na ulafi mwingi katika kupata mali.

Fauka ya hayo, vyama vya kisiasa katika nchi zinazoendelea vinamilikiwa na mataifa ya magharibi kwa lengo la kutumia ushawishi na maslahi yao ya kisiasa na kiuchumi kupitia ukoloni mamboleo katika nchi hizo. Kwa hivyo, katika hali zote ushindani na vurugu kati ya vyama vya kisiasa kwa maana halisi ni kati ya mataifa ya kikoloni ya kibepari kwa gharama ya watu wasio na hatia.

Bila kusahau kwamba mitazamo ya miamala ya kibepari katika siasa au kwengineko hutumia mtazamo wa Machiavelli wa kupigana kufikia lengo linalotakikana kwa mbinu na njia yoyote inayotumika.

Katika hali hii, wanasiasa wa kidemokrasia katika hali nyingi hutumia njia za kikatili kufikia mafanikio yao ya kisiasa. Kwa mfano, mnamo 1992, inaaminika kuwa Rais wa Kenya wa wakati huo Moi aliua 1,500 na kuwalazimisha takriban wakaazi 250,000 kukimbia katika Bonde la Ufa na kuwazuia kupiga kura kwa upinzani.

Hali ya sasa ya kuhuzunisha nchini Msumbiji katika hatua hii ya hatari ambayo imegharimu maisha ya wengi wakiwemo viongozi wawili wakuu wa upinzani ni miongoni mwa vurugu nyingi zinazofanywa na dola za kikoloni za kibepari zinazohalalisha kunyonya mali yake na kiasi kikubwa cha maliasili.

Inasikitisha zaidi kwamba Msumbiji iliwahi kufurahia maisha ya amani ilipopitia Uislamu pindi sehemu yake ya kaskazini ya jimbo tajiri zaidi la Cabo Delgado ilipokuwa sehemu ya jimbo kuu la Kilwa la Afrika Mashariki mnamo 1505 hadi uvamizi wa wakoloni katika miaka ya 1700. Uvamizi wa Wareno na baadaye ukoloni haukuleta chochote ila ukatili usio na mwisho unaoendelea, mauaji, unyonyaji na maovu yote kwa watu wake.

Ni wakati muafaka sasa kwa watu wa Msumbiji kuregea katika kile kilichowapa amani mara ya kwanza ambacho ni Uislamu, kwa kufanya kazi ya kusimamisha tena dola yake (Khilafah) katika ulimwengu wa Kiislamu ambayo italeta amani na ustawi, kuunganisha ardhi zote za Waislamu na kuondoa aina zote za unyonyaji na unyanyasaji wa kikoloni wa kibepari.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Said Bitomwa
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu