Alhamisi, 03 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kupigana kwa Heshima, au Kutotenda kwa Udhalilifu?!

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mnamo tarehe 30 Oktoba 2024, Naim Qassem alisema katika hotuba yake ya kwanza ya video baada ya kuapishwa kama Katibu Mkuu wa kundi linaloungwa mkono na Iran, “Tofauti kati yetu na ‘Israel’ ni kwamba tunapigana kwa heshima, tukilenga kambi, jeshi, vifaru na askari, huku wao wanaua raia na watu wasio na silaha, na kuangamiza watu na majengo ya miundombinu.” (Al-Ahed News)

Maoni:

Ulichokiita heshima, ewe Sheikh, si heshima katika kitu chochote. Ni kutotenda, udhaifu na udhalilifu. Adui anatekeleza mauaji makubwa, na kuua makumi ya maelfu ya watu wasio na hatia na walio katika hatari ya ulemavu, wanawake na watoto katika nyumba zao, vijiji na miji nchini Palestina na Lebanon, kuharibu nyumba zao, hospitali, misikiti na mahema juu ya vichwa vyao, na kugeuza miji yote na vijiji kuwa vifusi na vumbi kwa makumi ya maelfu ya makombora mazito na makubwa. Kwako wewe, unajibu haya yote kwa kutumia makombora yenye idadi na athari chache. Unaweka kikomo shabaha zako kwa jeshi na vifaa vyao. Kisha unahesabu hasara zake ndani ya mwaka mmoja na nusu kwa wapiganaji tu kadhaa na uharibifu mdogo kwa baadhi ya vituo vyake vya kijeshi. Hii sio heshima na maadili ima kutoka kwa neema au kutoka kwa Shariah au kutoka kwa Fiqh. Ni kutotenda, usaliti, udhalilifu na usaliti wenyewe.

Maneno yako, ewe Sheikh yanahusisha fahamu hatari ambazo ziko mbali na Shariah ya Mwenyezi Mungu (swt). Kama ulivyoelezwa kwamba maadui ambao wanaweza kulengwa katika vita hivi ni wapiganaji pekee, wakati wa utumishi wao wa kijeshi, katika mitambo yao ya kijeshi, kwenye vifaru vyao na kwenye mstari wa mbele pekee. Hata hivyo, je hao wengine walioko majumbani mwao, madukani, makazini na sokoni ni watu wasio na hatia na watu wanaolindwa?!

Inaonekana kana kwamba umesahau, Katibu Mkuu, hukmu ya Kiislamu iliyokubaliwa na wanazuoni wote faqhi (fuqaha), wakiwemo mafaqihi wako mwenyewe, kwamba Palestina yote ni ardhi ya Kiislamu inayokaliwa kwa mabavu na jeshi la kafiri. Yote ni uwanja wa vita. Wale wote wanaoshikilia uraia wa umbile hili la Kiyahudi, isipokuwa wakaazi asili wa ardhi hiyo, wanachukuliwa kuwa wakaliaji kimabavu, wavamizi na wapiganaji, wawe wanaume, wanawake, vijana na wazee. Hii ni iwapo wangali wanahudumu katika jeshi, au wamestaafu, au raia, kama wanavyopenda kujielezea. Wote ni shabaha halali za Shariah kwetu katika vita vya kuikomboa ardhi ya Kiislamu wanayoikalia kimabavu. Inaonekana kwamba umesahau Kauli ya Mwenyezi Mungu (swt),

[وَقَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللهِ الَّذِينَ يُقَاتِلُونَكُمْ وَلَا تَعْتَدُوا إِنَّ اللهَ لَا يُحِبُّ الْمُعْتَدِينَ * وَاقْتُلُوهُمْ حَيْثُ ثَقِفْتُمُوهُمْ وَأَخْرِجُوهُم مِّنْ حَيْثُ أَخْرَجُوكُمْ]

“Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui * Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni.” [Surah Al-Baqarah 2:190-191]. Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[مَنِ اعْتَدَى عَلَيْكُمْ فَاعْتَدُوا عَلَيْهِ بِمِثْلِ مَا اعْتَدَى عَلَيْكُمْ]

“Anaye kushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyo kushambulieni.” [Surah Al-Baqarah 2:194] Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[فَإِمَّا تَثْقَفَنَّهُمْ فِي الْحَرْبِ فَشَرِّدْ بِهِم مَّنْ خَلْفَهُمْ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ]

“Basi ukiwakuta vitani wakimbize walio nyuma yao ili wapate kukumbuka.” [Surah Al-Anfaal 8:57].

Ni kanuni ya msingi ya vita na mapigano kwamba jibu kwa uvamizi wa adui lazima lisiwe chini ya uvamizi wake. Badala yake, yule anayepigana kwa kujilinda yeye mwenyewe, ardhi yake, heshima yake na ukombozi wa ardhi yake kutoka kwa mkaliaji kimabavu, ana haki ya kutumia nguvu ya juu zaidi, na zilizo katika uwezo wake. Hata hivyo, licha ya mauaji yaliyofanywa na adui dhidi ya viongozi wenu, wapiganaji na watu, na licha ya uharibifu mkubwa wa miji na vijiji vyenu, bado mnajizuia na umbile la Kiyahudi hadi leo. Sheria zako za makabiliano zina kikomo ndani ya kikomo ambacho huzidishi!

Ahadi na vitisho vyako viko wapi, ambavyo umevirudia kwa miaka mingi, pamoja na utayari wako wa kuliangamiza umbile la Kiyahudi kwa dakika chache?! Yako wapi yale maroketi uliyowaahidi Mayahudi kuwa utaharibu uwanja wa gesi wa Karish, na kinu cha nyuklia cha Dimona?! Iko wapi ahadi yako ya kupenya katika ardhi iliyokaliwa ya Galilaya (al-Jaleel), katika vita vya kweli vijavyo?! Ziko wapi ahadi zako za kuukomboa Al-Masjid Al-Aqsa na kuswali ndani yake?! Je, bado unasubiri utekelezaji wa ahadi zote hizi utekelezwe wakati wa fursa kubwa kuliko vita hivi visivyofikirika katika uhalifu wake?!

Basi, ilikuwa wapi heshima yako hii ya kijeshi, ewe Sheikh, ulipopigana vita vyako vya kihalifu visivyo na Dini na maadili, dhidi ya wana wa Umma wa Kiislamu, walioasi dhidi ya dhalimu wao mhalifu nchini Syria?! Huko, ambapo ulipigana vita kwa amri ya mlezi wako al-Faqih, na kwa mwelekeo wa Marekani, katika kulinda mojawapo ya tawala chafu zaidi katika historia. Hili lilikuwa katika makubaliano na dola zote za kikafiri duniani ili kuepusha hatari ya kuanzisha dola halisi kwa ajili ya Umma wa Kiislamu. Katika vita vyenu hivyo vichafu, ambavyo hamjajitoa mpaka leo, mmesahau maadili na hukmu zote za kivita zinazolazimishwa na Mwenyezi Mungu (swt). Pamoja na kupigana na mujahidina waliotoka kwa ajili ya Jihad kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt), uliua nafsi zisizo na hatia, bila ya kutofautisha kati ya mwanamume au mwanamke, kati ya mpiganaji na raia, na baina ya wazee na watoto. Hapo, hukumwacha binadamu yeyote au jengo lolote la miundombinu. Mlikuwa washirika wa wale waliofeli na kuwadhalilisha katika vita vyenu chungu vya leo. Mlikuwa washirika pamoja nao katika kurusha mabomu ya kifo yaliyobomoa majengo juu ya vichwa vya watu wao, na katika kurusha aina hatari zaidi za roketi kuharibu vitongoji, vijiji na miji. Hapo ulitenda kama umbile la Kiyahudi linavyofanya sasa kwa watu wa Gaza na kwa watu wako nchini Lebanon.

Shida yako kubwa leo, ewe Sheikh, ni kwamba hupigani vita vyako mwenyewe, wala vita vya Palestina, wala vita vya Lebanon, ambavyo mamlaka yake hukuyafurahia sana miaka iliyopita. Badala yake, unapigana vita vya wakala kwa niaba ya mlezi wako wa Iran, ambaye amekufanya wewe, Lebanon, na watu wake kuwa mstari wa mbele wa ulinzi, kulinda ardhi na serikali yake yenyewe. Tatizo lako ni kwamba ulijenga jengo lako kwa mchanga, na nguzo za nyasi. lilianguka kwa kufumba na kufumbua.

Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[أَفَمَنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَى تَقْوَى مِنَ اللهِ وَرِضْوَانٍ خَيْرٌ أَمْ مَنْ أَسَّسَ بُنْيَانَهُ عَلَى شَفَا جُرُفٍ هَارٍ فَانْهَارَ بِهِ فِي نَارِ جَهَنَّمَ وَاللهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ]

“Je! Mwenye kuweka msingi wa jengo lake juu ya kumcha Mwenyezi Mungu na radhi zake ni bora au mwenye kuweka msingi wa jengo lake juu ya ukingo wa shimo linalo burugunyika, na likaburugunyika naye katika Moto wa Jahannamu? Na Mwenyezi Mungu hawaongoi watu madhaalimu.” [Surah At-Tawba 9: 109].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ahmad Al-Qasas
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu