Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia ni mwenyeji wa Kongamano la Kimataifa la Wanawake “Familia: Changamoto na Suluhisho la Kiislamu” Lililoandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya
- Imepeperushwa katika Kitengo cha Wanawake Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Mnamo Jumamosi 27 Oktoba 2018, Hizb ut Tahrir Wilayah ya Tunisia itakuwa mwenyeji wa kongamano muhimu la kimataifa la wanawake lililoandaliwa na Kitengo cha Wanawake katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kwa kichwa, “Familia: Changamoto na Suluhisho la Kiislamu” ili kutatua janga linaloathiri uwiano na umoja wa ndoa na familia katika jamii ulimwenguni, ikijumuisha ardhi za Waislamu. Tukio hili adhimu litawakusanya wanawake waliopendekezwa kutoka Tunisia na nchi nyinginezo, ambao ni viongozi mashuhuri katika jamii zao au walio na ujuzi kuhusiana na mada hii.