Ni Khilafah Pekee Ndiyo Iwezayo Kuchukua Nafasi ya Mpango wa Uchumi wa Amerika Unaosambaratika
- Imepeperushwa katika Khilafah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Katika usikilizwaji wa Kamati ya Seneti ya Benki wa tarehe 28 Septemba 2021, Waziri wa Fedha, Janet L. Yellen, aliwaonya watunga sheria wa Amerika mnamo Septemba 28 juu ya matokeo ya “msiba mkuu”, pindi Bunge la Marekani likishindwa kuongeza au kusitisha ukomo wa kisheria wa deni hadi Oktoba 18, 2021, akisema, kuchelewa kutapelekea mporomoko wa kujiumiza wenyewe wa kiuchumi na mgogoro wa kifedha.