Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 404
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Vichwa Vikuu vya Toleo 404
Vichwa Vikuu vya Toleo 404
Jumatatu tarehe 15 Agosti 2022 iliadhimisha mwaka mmoja tangu Taliban waingie Kabul na serikali ya iliyokufa ya Afghanistan iliyokuwa ikiungwa mkono na Marekani kuanguka rasmi.
Wizara ya Wanawake, Familia na Wazee inazindua kampeni ya kinidhamu ambayo kwayo ilichagua kauli mbiu ya “Kupinga Unyanyasaji dhidi ya Wanawake” ambapo kupitia kwayo inapigia debe utekelezaji wa Sheria Msingi nambari 58 ya tarehe 11/8/2017, iwe ndio mdhamini pekee wa kuweka hatua za kutokomeza aina zote za unyanyasaji dhidi ya wanawake.
Katika jibu lake kwa swali: Iwapo Rais Erdogan angekutana na Bashar al-Assad, Waziri wa Mambo ya Nje Mevlut Cavusoglu alijibu: “Hakuna mawasiliano hayo kwa sasa...Kwa muda mrefu, Putin na maafisa wa Urusi walitaka mkutano kati ya Assad na rais wetu.