Vita vya Amerika na umbile la Kiyahudi dhidi ya Iran: Kimya cha Watawala na Kujisalimisha kwa Murshed
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza makubaliano kamili kati ya Israel na Iran juu ya usitishaji kamili wa mapigano. Katika jukwaa lake la Kijamii la Truth, Trump alisema: "PONGEZI KWA KILA MTU! Imekubaliwa kikamilifu na kati ya Israel na Iran kwamba kutakuwa na Usitishaji Vita Kamili na Jumla (katika takriban saa 6 kutoka sasa, wakati Israel na Iran zitakapomaliza na kukamilisha misheni zao zinazoendelea, za mwisho!), kwa masaa 12, ambapo Vita vitazingatiwa, VIMEMALIZIKA! Trump alisifu pande zote mbili, akisema: "Misuli, Ujasiri, na Ujasusi kumaliza" mzozo na kusema kwamba ulimwengu na Mashariki ya Kati ndio "WASHINDI halisi".