Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan Mkao wa Kadhia za Ummah

Marekebisho ya Sheria ya Hivi Majuzi... Mtazamo Angavu Uliojengwa kwa Msingi wa Uislamu

Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan ilifanya Mkao wake wa Kadhia za Ummah kwa anwani: Marekebisho ya Sheria ya Hivi Majuzi... Mtazamo Angavu Uliojengwa kwa Msingi wa Uislamu.

Wazungumzaji wakuu walijumuisha Ustaadh Hatem Ja’far (wakili) – Mwanachama wa Baraza la Wilayah / Wilayah Sudan, na Ustaadh Ibrahim Othman (Abu Khalil) – Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir Wilayah Sudan, aliyezungumzia kuhusu Serikali ya Mpito kufutilia mbali idadi kadhaa ya sheria kwa kisingizio kwamba zinaufunga uhuru, na akasema: Kupitia kuliangalia Gazeti Rasmi la Serikali Na. 1904 lililo chapishwa mnamo Jumatatu 13/7/2020, tunapata kuwa marekebisho ya sheria hizi (marekebisho 35 ya sheria ya jinai, na marekebisho 3 ya sheria ya mpangilio wa jinai, Kifungu Kimoja katika Sheria ya Vyama, vifungu 5 vya Sheria ya Usalama wa Taifa, kimoja cha Sheria ya Trafiki, vifungu 3 vya Sheria ya Pasipoti na Uhamiaji, vifungu viwili katika Sheria ya Mashtaka ya Umma, na vifungu 34 katika Sheria ya Kuzuia Uhalifu wa Habari, sheria mpya inayoitwa Sheria ya Tume ya Marekebisho ya Mfumo wa Sheria na Haki ya 2020). 

Jumamosi, 27 Dhul Qi‘dah 1441 H sawia na 18/07/2020 M

Ustaadh Mohammad Jameh (Abu Ayman)

Naibu Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan

 

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoIjumaa, 24 Julai 2020 09:27

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu