- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Wilayah Sudan: Ugawanyaji Toleo la Mapambano Lenye Kutahadharisha Mdororo wa Kiuchumi na Ongezeko la Viwango vya Umasikini!
Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan iligawanya toleo la mapambano katika miji mingi ya Sudan kwa anwani "Marekebisho ya Bajeti Mwaka 2020 ni Kuendeleza Uharibifu katika uchumi wa Sudan kwa Kuutii Mfuko wa Fedha wa Kimataifa" ambapo ugawanyaji wake ulifanyika masokoni na sehemu jumla, na toleo hili lilitahadharisha matokeo ya utekelezaji marekebisho hayo na kwamba yatapelekea katika mdororo wa kiuchumi na kwamba gharama za ala za uzalishaji zitakuwa juu ambapo itapelekea wazalishaji kutoka katika soko la kazi, na Hizb ut Tahrir ikatahadharisha kutokana na ziada ya marekebisho batili na kwamba utekelezaji wa bajeti hii utazidisha hali ya umasikini na matokeo yake yatakuwa ni janga kwa watu wa nchi hii!
Ugawanyaji wa toleo hili ulikuwa mkubwa mno katika kila pembe ya nchi mashariki na magharibi, kaskazini na kusini, na toleo hili liliashiria kwamba jambo moja pekee litakaloitoa Sudan kutoka katika mgogoro wa kiuchumi ni kukata mafungamano na dola za kikoloni na kutotii sera zao zenye kuangamiza watu, na kuzifurusha taasisi za kimataifa ambazo zinapora utajiri wa watu katika nchi yetu na Hizb ut Tahrir ikatoa wito katika toleo hilo wa kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida ili kuikomboa Sudan na ulimwengu mzima kutokana na shari ya urasilimali kwani ndiyo pekee inayoweza kutatua hali ya kiuchumi ya kindani na ya kiulimwengu
Alhamisi, 23 Dhu al-Hijjah 1441 H sawia na 13 Agosti 2020 M
https://hizb-uttahrir.info/sw/index.php/dawah/sudan/1032.html#sigProId0a39d27e2c