Jumamosi, 19 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan:

Maoni ya Habari 27/11/2024 M

Maoni ya habari yaliyotolewa na Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Pakistan.

Kwa ajili ya mabadiliko ya kweli... kataa Demokrasia... simamisha Khilafah Rashida.

Ewe Mola turudishie ngao yetu, Khilafah Rashida kwa njia ya Utume...  Allahumma Amina.

#BringBackKhilafah

Jumatano, 25 Jumada al-Awwal 1446 H sawia na 27 Novemba 2024 M

Maandalizi ya Silaha ni kwa ajili ya Vita, Sio Maonyesho na Mauzo


Mnamo tarehe 19 Novemba, maonyesho makubwa ya ulinzi ya Pakistan jijini Karachi yalianza. Sasa sio wakati wa kuonyesha silaha. Ni wakati wa kutumia silaha katika vita muhimu vya kuinusuru Gaza. Kifaru aina ya Haider ni cha kuongoza mashambulizi ya kivita dhidi ya vikosi vya ardhini vya jeshi la Kiyahudi. Droni aina ya Shahpar-3 ni kwa ajili ya kugonga ngao ya ulinzi wa anga ya umbile la Kiyahudi. Amesema Mwenyezi Mungu (swt) مِّن قُوَّةٍ وَمِن رِّبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّهِ وَعَدُوَّكُمْ  “Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu.” [Surah al-Anfal 8:60]. Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Ipeni Nusrah yenu Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida, ili muweze kujitahidi kupata ushindi na shahada.

Alhamisi, 19 Jumada al-Awwal 1446 H – 21 Novemba 2024 M

Gaza ni Makaburi ya Watoto, Ilhali Watawala Wanazuia Kuhamasishwa kwa Majeshi ya Waislamu.


Mnamo tarehe 20 Novemba 2024, mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), aliandika tweet, “Gaza imekuwa makaburi ya watoto. Wanauawa, kujeruhiwa, kulazimishwa kukimbia, na kunyimwa usalama, masomo, na kucheza.” Enyi majeshi ya Pakistan, hata makafiri wanakiri kwamba ulimwengu wa kisasa haujashuhudia uhalifu mkubwa zaidi kuliko uharibifu wa Gaza. Watawala wanakuzuieni kusonga kwa ajili ya ukombozi wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Ni wakati sasa wa kutimiza wajibu wenu wa Shariah. Wang'oeni watawala hawa wasaliti na muipe Nusrah yenu Hizb ut Tahrir ili kusimamisha tena Khilafah Rashida. Khilafah itafungua njia za anga na za ardhini za mawasiliano kwa ndege zenu za kivita na vifaru, ili kwamba muhamasike kwa ajili ya ulinzi wa watoto wa Gaza.

Ijumaa, 20 Jumada al-Awwal 1446 H – 22 Novemba 2024 M

Dini yetu ni Uislamu na Kitambulisho chetu ni Uislamu


Mnamo tarehe 20 Novemba 2024, Mkuu wa Jeshi la Pakistan alisema “Hakuna kitu kikubwa kuliko nchi na hatuna kitambulisho zaidi ya Pakistan.” Amesema Mwenyezi Mungu ﷻ إِنَّ ٱلدِّينَ عِندَ ٱللَّهِ ٱلْإِسْلَـٰمُ  “Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu.” [Surah Aal-e-Imran, 3:19] na هُوَ سَمَّاكُمُ الْمُسْلِمِينَ  “Yeye (Mwenyezi Mungu) alikuiteni Waislamu” [Surah Al-Hajj, 22:78].   Mwenyezi Mungu ﷻ ameifanya Dini ya Uislamu juu ya kila kitu. Uislamu ulitangaza utaifa, uzalendo na ukabila kuwa ni batili. Uislamu haukufafanua ardhi au rangi yoyote kama msingi wa kitambulisho. Leo Mayahudi wanafanya ukatili dhidi ya Waislamu wa Palestina kwa sababu watawala hawakusanyi majeshi yetu kwa misingi ya utaifa. Khilafah Rashida inakataa mipaka yote ya utaifa na inachukulia ardhi za Waislamu kama ardhi moja.

Jumamosi, 21 Jumada al-Awwal 1446 H – 23 Novemba 2024 M

Serikali pamoja na Upinzani ni Sura Mbili za Mfumo Ule ule Uliofeli


Mji wa Rawalpindi umefungwa ili kuzuia waandamanaji kutoka kwa upinzani kuingia mji mkuu mnamo tarehe 24 Novemba 2024. Hata hivyo, hakuna tofauti kati ya wanasiasa wa mirengo tawala. Hawaondoi riba na kodi zisizo za Kiislamu. Hawatabanni dhahabu na fedha kama sarafu. Hawafanyi nguvu za umeme kuwa mali ya umma. Hawafanyi kazi ya kuunganisha ardhi za Waislamu. Hawakusanyi majeshi kwa ajili ya ukombozi wa ardhi zinazokaliwa kimabavu. Hawakati mafungamano na maadui wa Ummah. Wanashindana kuketi kwenye kiti cha khiyana cha utawala na kumuasi Mwenyezi Mungu ﷻ, wakitumikia maslahi ya mabwana zao wa Magharibi. Ni lazima tuukatae mfumo wa sasa na makundi tawala. Ni lazima tushirikiane na wanasiasa wa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida.

Jumapili, 22 Jumada al-Awwal 1446 H – 24 Novemba 2024 M

Ukoloni Unabadilisha Uchumi Kuwa Mashini ya Kulipa Pesa kwa Wale Wanaofaidika na Riba


Mnamo tarehe 21 Novemba, 2024 Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano ya Mfuko wa Fedha wa Kimataifa alisema, “juu ya uwezekano wa upungufu wa mapato, ninamaanisha, hili ni jambo ambalo timu hii itakuwa ikilikagua.” Sababu kubwa ya uhaba wa mapato ni riba. 52% ya bajeti yote ni kwa ajili ya malipo ya riba pekee. Serikali inafukuzia shabaha ya kuongeza ushuru kwa 40%, ndani ya mwaka mmoja tu. Tatizo la kiuchumi nchini Pakistan si tofauti na lile la Misri, Uturuki na Indonesia. Tiba ya tatizo sio uhamiaji kwenda Magharibi. Hiyo ni tiba ya tatizo la baadhi ya watu binafsi, sio Ummah wa bilioni mbili. Tiba hiyo ni kufutiliwa mbali kwa riba kupitia mfumo wa uchumi wa Kiislamu. Ummah na majeshi yake lazima washirikiane na Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida.

Jumatatu, 23 Jumada al-Awwal 1446 H – 25 Novemba 2024 M

Watawala Wanahusika na Kugeuza Mizozo Juu ya Ardhi kuwa Vurugu la Kijamii


Mnamo tarehe 22 Novemba 2024, katika Shirika la Parachinar na Kurram, mapigano kati ya makabila mawili yalikuwa ya umwagaji damu. Watu kadhaa wamepoteza maisha hadi sasa. Serikali imekuwa haipo kabisa katika kipindi chote. Watu wa Fitna wameruhusiwa kuwasha moto wa Fitna waziwazi. Watawala hawakusuluhisha mzozo hata mmoja wa ardhi wa kikabila kupitia kadhi wa Shariah. Hawakusimamisha mapigano kati ya makabila mawili, licha ya kuwa na amri ya mamia ya maelfu ya polisi wenye silaha na wanajeshi. Hawatoi usalama kwa Waislamu. Walakini, watawala wako tayari kila wakati kutekeleza operesheni za kijeshi, na kutumia mabilioni ya rupia, kwa maagizo ya Amerika. Watawala hawa wanastahili vipi basi kutawala? Khilafah Rashida hutoa amani na utulivu kwa Ummah, kwa kutoa utatuzi wa haraka na sahihi wa migogoro.

Jumanne, 24 Jumada al-Awwal 1446 H – 26 Novemba 2024 M

Kutoka kwenye Deni hadi Ufanisi: Kufutilia mbali Riba kwa ajili ya Mapinduzi ya Kiuchumi


Ripoti ya habari ya tarehe 25 Novemba ilifichua maendeleo makubwa ya kiuchumi. Uwiano wa uwekezaji wa amana kwa sekta ya benki nchini Pakistan (IDR) umepanda hadi 94% isiyo na kifani kufikia Juni 2024. Kiwango hiki cha juu kinatokana na benki kuelekeza mtaji mkubwa katika ukopeshaji wa serikali, huku taasisi za fedha zikiwekeza trilioni 7.6 katika mikopo hiyo. dhamana za serikali zisizo na hatari. Kitendo hiki kimeinyima sekta ya kibinafsi, ukuaji unaonyonga. Mzizi wa tatizo hili ni utegemezi wa mifumo ya fedha inayozingatia riba kwa amana, ukopaji na ukopeshaji. Suluhisho pekee ni kukomeshwa kabisa kwa Riba na kutoa mfumo wa sarafu unaotegemea dhahabu na fedha. Mabadiliko haya ya kimapinduzi yataweka mazingira thabiti zaidi ya kifedha katika Khilafah Rashida, yakitayarisha njia ya ustawi endelevu wa kiuchumi chini ya kivuli cha Uislamu.

Jumatano, 25 Jumada al-Awwal 1446 H – 27 Novemba 2024 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu