Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Hizb ut Tahrir / Indonesia:

Majadiliaono ya Habari katika Gazeti la Umat:

Mustakbali wa Ummah katika Miaka Mitano Ijayo, Indonesia una Kiza Mno.

Takriban watu 250 wameshiriki kwenye Majadiliano ya Habari katika Gazeti la Umat: Mustakbali wa Ummah katika Miaka Mitano ijayo, Alhamisi (31/10/2019) katika eneo la Gedung Joang, Jakarta. Miongoni mwa wazungumzaji ni Abdul Chair Ramadhan (Mwenyekiti wa Kituo cha Habib Rizieq Shihab), Prof. Dkt. Suteki (Profesa wa Ndaki ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Diponegoro) na Muhammad Ismail Yusanto (Msemaji wa HTI) na mzungumzaji mkuu Farid Wadjdi (Mhariri mkuu wa Gazeti la Habari la Umat).

Kwa kuwepo uongozi huu na mjumuiko wa baraza hili, Prof. Suteki alibashiri kwamba katika miaka mitano ijayo Indonesia itakuwa mbaya zaidi. “Kwa hivyo, kwa maoni yangu miaka mitano ijayo itakuwa na kiza sana. Mustakbali wenye kiza. Utakuwa na kiza iwapo suluhisho la kukabili misimamo mikali litatumia mwelekeo wa kiusalama”, alisema. Kwa mujibu wa maoni yake, mwelekeo utakaochukuliwa haupaswi kuwa wa kiusalama bali mwelekeo wa mazungumzo.

Kwa upande wake, Ismail Yusanto alieleza kwamba serikali ya Jokowi Volume II ni ya msimamo mkali kweli kweli. “Sasa, hii (serikali) (inakumbatia) mtazamo wa msimamo mkali wa kisekula, usio na urafiki, usio na kielimu wala tafakari. Usio na urafiki kwa nani? Kwa wengi wa watu. Usio na elimu? Hawana elimu kuweza kufahamu ni nini hasa hitajio la Waislamu. Hitajio la Waislamu ni kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu (swt). Kwa hiyo hawakuelimika kwa sababu ya taarifa zao za kuchekesha na za kushangaza. Moja ya hizo ni taarifa ya kupiga marufuku hijab." [Maktab Ilamy Jakarta]

Afizi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Indonesia

Alhamisi, 03 Rabi Al-Awaal 1441 H - 31 Oktoba 2019 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu