Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Ujumbe kutoka kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir kwa Wale Wanaoihami Dawah
(Imetafsiriwa)

Sifa njema zote ni kwa Mwenyezi Mungu na dua na salamu zimshukie Mtume wa Mwenyezi
Mungu na jamaa zake na maswahaba zake na wale waliokuja baada yake,
Kwa wale wote walionitumia risala kupitia ukurasa wangu wa Facebook, wakishtumu maandishi
hayo meusi kupitia mtandao…

Kwa wale wote walio niandikia, wakishtumu maandishi ya kikundi cha waasi ‘Nakithin’
(waliovunja kiapo) na wale waliotoka (chamani) na wale ambao kwa sasa wanachukuliwa hatua
za kinidhamu…

Kwa wale wote walio niandikia; wakishtumu maandishi hayo maovu ya yule aliyetekwa na kiburi
chake…
Kwa wale wote walionitumia jumbe zao, wakishangazwa ni vipi watu hawa na wafuasi wao
wanajidhalilisha kiasi hicho…

Kwenu nyote, nawasalimu kwa maamkuzi ya Kiislamu:
Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh
Kaka na Dada Zangu Wapendwa,
Haishangazi kuwepo kwa aina hiyo ya watu na wafuasi wao, maadamu wema na ubaya
ungalipo ulimwenguni… watu aina hiyo wamekuwepo tangu zamani na wangalipo mpaka leo na
wanatarajiwa kuwepo siku za usoni vile vile. Baadhi ya wanachama wa Kamati ya Uongozi wa
Hizb walikihama chama wakipinga muelekeo wa Amiri muasisi Abu Ibrahim (Mwenyezi Mungu
amuwiye radhi). Na wakati wa enzi ya Amiri wa pili Abu Yusuf (Mwenyezi Mungu amuwiye
radhi), baadhi ya wanachama wa afisi ya Amiri walivunja kiapo chao. Na leo, wanaume, walio
na usemi na uzito kwa sababu ya Hizb, wamepotea njia, wamekiangusha chama, Hizb iliwapa
hadhi lakini wakaamua kushikamana na dunia.

(وَلَكِنَّهُ أَخْلَدَ إِلَى الْأَرْضِ وَاتَّبَعَ هَوَاهُ﴿ 

“…lakini (badala yake) alishikamana na dunia na akafuata matamanio yake.” [Al-A’raf:
7:176]

Kupotea njia kwao hakukuwa tu ni kupotea njia; bali walikhini amana na kuzua urongo. Baada
ya kufanya dhambi hilo kubwa kwa kumkhini yatima mali yake, kiongozi wao asema:
nimerudisha thamani ya nyumba hii – kana kwamba ni mkweli – lakini hamwambii mwenye
nyumba, bali amwambia mtu aliyeadhibiwa na wala hayumo ndani ya Hizb! … kama ambaye
kwamba mmiliki wa nyumba hiyo hajulikani na wala hakumkabili mara kadhaa juu ya kadhia hii!
Je hili sio jambo la kushangaza mno?

Na mmoja wao akamuuliza kuwa kwani haitoshi kwa Amiri kukuomba radhi naye akamjibu kuwa haitoshi! Hivyo basi wanazidanganya nafsi zao kabla ya kumdanganya Mwenyezi Mungu; kana kwamba kuna ombi la kuomba radhi! Wanafuata barabara ya uvumi mchafu. Wamedumu katika kudanganya, kwa matarajio ya kupata watu vipofu, wasioona sasa wala mbeleni, ambao
watawaamini. Mmoja wao alisema: Amiri alituma agizo kwa wanachama kuuandikia usimamizi
wa mtandao wa Facebook ufunge ukurasa wa mtu huyo. Na mwengine wao akajibu kwa kutoa
hakikisho kubwa kwamba hili lilifanyika na ukurasa huo kufungwa. Kana kwamba Amiri
alitingishwa na ukurasa huo wa kutamausha au hata kushughulika kuufungua! Hivi ndivyo jinsi
wanavyozua.

Ama kisingizio wanacho kitumia katika ukiukaji wao na uzushi wao ni “kuuhisabu uongozi”.
Kana kwamba hili haliko wala halijaonekana wala kusikika! Mpangilio wa “kuuhisabu uongozi”
umefafanuliwa kwa kina katika faili ya idara; miongoni mwa hao waliochangia kutunga faili hiyo
ndio wanaoikiuka. Lakini kuna mwili mwengine mbali na nukta ya kuhisabu, nao ni Diwani ya
Madhalim (Bodi ya kushughulikia malalamishi), inasimamiwa na watu mukhlisina na wacha
Mungu, wasioogopa lawama ya yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt), ingawa hatumtakasi
yeyote kwa Mwenyezi Mungu. Kuhisabu na malalamishi ni mambo yaliyo thabiti, hakuna yeyote
atakaye yakataa isipokuwa muovu, na hakuna yeyote atakaye ukataa uaminifu wao isipokuwa
mashetani wa kibinadamu na wa kijini… hili wamekosa kuwa makini nalo wala kusitisha
wayafanyayo. Mtu huyu kisha akatoa vitisho: kuwa sasa anayaelekeza maneno kwa Amiri
kupitia mtandaoni (vitisho hafifu), lakini baadaye atazungumza maneno yenye cheche kali. Hii
ndio jinsi ya vitisho vyao. Amekosa kutambua kuwa watu waliokuwa na nguvu, idadi kubwa na
umoja kumshinda yeye hawakuweza kuiathiri Hizb wala mwanachama yeyote huru na mwema
ndani yake … sembuse wao…

Kaka na Dada Zangu Wapendwa,
Kama nilivyo tangulia kutaja, si ajabu kuwepo kwa watu kama hawa. Wakati wowote kunapo
kuwa na ulinganizi wa haki, huwepo watu kama hawa. Huzungumza urongo, uzushi na kudai
kuwa wanasimama msimamo wa sawa, lakini ni madai yasiokuwa na msingi. Wanapo waona
walinganizi wa haki wamesimama imara na kushikamana nayo, nyoyo zao hujaa chuki. Na
wanapoona walinganizi hawa wakiungwa mkono na kukubaliwa na Ummah, nyoyo zao hujaa
njama na vitimvi. Lakini wanapoona ukatili wa madhalimu dhidi ya walinganizi wa haki, hufurahi
na kuzidisha uzushi juu yao, wakidhani kuwa watawaathiri na kuwaweka mbali na haki wanayo
shikamana nayo.

(إِنْ تَمْسَسْكُمْ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ وَإِنْ تُصِبْكُمْ سَيِّئَةٌ يَفْرَحُوا بِهَا وَإِنْ تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا لَا يَضُرُّكُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئًا إِنَّ اللَّهَ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ)

… “Yanapokufikeni mazuri huwachukiza na yanapo kusibuni mabaya hufurahi kwayo; lakini mukisubiri na kumcha Mwenyezi Mungu, njama zao hazitawadhuruni chochote. Hakika Mwenyezi Mungu ni mtambuzi wa wayafanyayo” [Al-i-Imran: 120].

Kaka na Dada Zangu Wapendwa,
Kurasa hizi ovu hazitakoma maadamu wema na uovu ungalipo duniani kama nilivyo tangulia
kutaja juu. Watu waovu wanataka kutushughulisha na sumu yao na uzushi wao. Ikiwa
tutashughulishwa nao, watakuwa wamefaulu, na ikiwa tutazikataa kurasa zao, mithili ya kutupa
mbegu iliyooza, kutowatilia maanani, tutakuwa tumepangua vitendo vyao na watakufa na chuki
zao. Hapa, sitaki kuwazuia kushiriki na kupata ufahamu juu ya kurasa hizi ovu, hivyo basi
siwaamrishi wala siwakatazi. Lakini, ninacho waamrisha kwa mkazo ni kuwa musinitumie
kurasa yoyote katika hizo. Nataka kujishughulisha katika kheri na njia iliyo nyoka, ili msafara
huu unaobeba kurunzi ya nuru ambao wasafiri wake wataabiri chombo cha Khilafah Rashidah
kwa idhini ya Mwenyezi Mungu katika muda uliopangwa na kukadiriwa na Mwenyezi Mungu. Na kwa kila jambo lina muda wake maalumu… Namuomba Mwenyezi Mungu (swt) hili liwe karibu.

(إِنَّ اللَّهَ بَالِغُ أَمْرِهِ قَدْ جَعَلَ اللَّهُ لِكُلِّ شَيْءٍ قَدْرًا)

“Hakika, Mwenyezi Mungu atatimiza jambo lake. Hakika Mwenyezi Mungu amejaalia kwa kila kitu qadari” [At-Talaq 3]

Kutamatisha, nyinyi, kaka na dada zangu, ni kizuizi chenye kuhami dhidi ya maandishi haya
maovu na uzushi usio na msingi. Nimeambiwa kwamba nyinyi ni wanaume wa wanaume,
ambao huzidi kupata nguvu kutokana na wapinzani wenu, na hamuathiriwi na fitna na
migogoro, bali haya huzidisha ari na kujitolea kwenu … Nyinyi ni wanaume wa wanaume
ambao mithili yao ni kama wale ambao Mwenyezi Mungu (swt) amewasifu:

(الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَانًا وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ* فَانْقَلَبُوا بِنِعْمَةٍ مِنَ اللَّهِ وَفَضْلٍ لَمْ يَمْسَسْهُمْ سُوءٌ وَاتَّبَعُوا رِضْوَانَ اللَّهِ وَاللَّهُ ذُو فَضْلٍ عَظِيم)


“Wale ambao wanafiki waliwaambia, ‘Hakika watu wamekusanyika dhidi yenu, hivyo basi
waogopeni.’ Badala yake hili likawazidishia Imani na wakasema ,‘Mwenyezi Mungu
anatutosheleza, na ndiye wakili bora* Hivyo basi wakarudi na neema kutoka kwa
Mwenyezi Mungu na fadhila, huku wakiwa hawakuguswa na uovu wowote. Na wakatafuta
radhi za Mwenyezi Mungu ,na Mwenyezi Mungu ni mwingi wa fadhila” [Al-i-Imran: 173-174]

Kumalizia, ningependa kusisitiza yale niliyosema juu: Musinitumie chochote kutoka katika
kurasa hizo ovu na wala musihofu kutokana na wazushi hao, wala kutokana na kuendelea
kwao na hilo, kwa sababu Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Nguvu (Al-Qawi) na Mwingi wa Uwezo
(Al-Aziz), huwahami waja wake waaminifu kwake

(إِنَّ اللَّهَ يُدَافِعُ عَنِ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ كُلَّ خَوَّانٍ كَفُورٍ)

“Hakika Mwenyezi Mungu huwahami wale walio amini. Hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kukhini mwenye kufuru” [Al-Hajj: 38.]
Namuomba Mwenyezi Mungu (swt) atufinike hapa duniani na kivuli cha Khilafah, ili tupate kuwa
mashahidi na wanajeshi wake, na ili tubakie ndani ya kivuli chake (swt) kesho Akhera, siku
ambayo hakutakuwa na kivuli isipokuwa chake Yeye, katika kiti cha enzi karibu na Bwana,
Mwenye Uwezo Kamili, na kufaulu katika maisha yote mawili; hakika huko ndiko kufaulu
kukubwa.

Wa Assalamu Alaikum wa Rahmatullah wa Barakatuh

Ndugu Yenu,
Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatano, 29 Januari 2020 14:46

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu