Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Salamu kutoka kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah
Kwa Wanaozuru Mitandao Yake kwa Mnasaba wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan 1443 H sawia na 2022 M
(Imetafsiriwa)

Kwa Umma bora ulioletwa kwa wanadamu ... Umma wa Kiislamu ambao Mwenyezi Mungu (swt) aliukirimu kwa utiifu Kwake...

Kwa wabebaji wa Dawah ambao haiwashughulishi biashara wala mauzo kutokana na kumkumbuka Mwenyezi Mungu...

Kwa wageni waheshimiwa kurasa, wanaozuru kurasa kwa kutokana na kheri zinazoibeba ...

Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh,

Nawapa tahania kwa kuwasili mwezi huu mtukufu

(شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنْزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ)

“Mwezi wa Ramadhan ambao ndani yake imeteremshwa Qur'an, uongofu kwa watu na hoja wazi za uongofu na upambanuzi (wa haki na batili).” [Al-Baqarah: 185]

Ni mwezi ambao Mwenyezi Mungu (swt) amewabariki Waislamu kwa msamaha, kama ilivyo katika hadith ya Mtume (saw):

«مَنْ قَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ»

“Yeyote inayesimama kwa kuswali swala za usiku wakati wa Ramadhan akiwa na imani na matarajio mema kwa Mwenyezi Mungu, husamehewa madhambi yake yaliyotangulia." [Bukhari kutoka kwa Abu Huraira] ... ambao ndani yake imeteremshwa Qur’an Tukufu, na ndani yake kulikuwa na ushindi na ufunguzi muhimu ... mwezi wa kazi, juhudi na bidii, na mwezi wa ibada, subira na jihad. Enyi Waislamu, kunjeni mikono ya mashati yenu, na shindaneni katika mambo ya kheri, kwani thawabu na Mema huongezwa mara nyingi.

Na ninamuomba Mwenyezi Mungu (swt) awakubalie Waislamu wote saumu na Qiyam (swala za usiku) zao, na aufanye mwezi huu uliobarikiwa kuwa ni mwezi wa kufunguka kwa kheri na baraka, na utangulizi wa ushindi kwa kusimamisha Khilafah Rashida. Ambapo Umma utakuwa chini ya kivuli cha Rayat Al U’qab (bendera), Rayah ya La Ilaha iIla Allah, na utaregea kama ulivyokuwa mbeleni Ummah adhimu, ulioimarishwa na Mola wake Mlezi na kukirimiwa kwa Dini yake.

 (وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ)

“...Na siku hiyo waumini watafurahi * Kwa nusra ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye na Yeye ndiye mwenye nguvu mwenye kurehemu” [Ar-Rum: 4-5]

Wa Assalamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuh

Mkesha wa Jumamosi Siku ya Kwanza ya Ramadan 1443 H

01/4/2022 M

Ndugu Yenu

Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu