- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
“Mfalme” wa Kiimla wa Jordan Anashiriki kwa Shangwe katika Uuzaji wa Ardhi Iliyobarikiwa
(Imetafsiriwa)
Mtawala kiimla wa Jordan hivi majuzi aliondoka kwenye kasri lake baada ya maagizo ya Trump, akiruka kwa shauku kuelekea Ikulu ya White House kucheza dori yake katika uuzaji wa Palestina.
"Mfalme" huyo alisema wiki iliyopita tu, mnamo tarehe 5 Februari 2025, kwamba uhamisho wa Wapalestina kwenda Jordan ulikuwa "mstari mwekundu," huku uvumi ukienea kwamba kuvuka mstari mwekundu kunaweza kusababisha Jordan kutangaza vita dhidi ya "Israel". Hili limeonekana kuwa kweli kama alivyodai El-Sisi mwaka jana kuwa "Rafah" ni mstari mwekundu wa Misri.
Katika ziara yake ya White House, "mfalme" wa Jordan alikaa kimya na kwa utiifu kando ya Trump huku POTUS ikiregelea mpango wake wa kuitakasa kimbari Palestina: "Hatutalazimika kununua. Tutakuwa na Gaza. Hatuhitaji kununua. Hakuna cha kununua. Tutakuwa na Gaza,” Trump aliwaambia waandishi wa habari. "Ni eneo lenye vita. Tutalichukua, tutalishikilia, tutalithamini... Itakuwa kwa ajili ya watu wa Mashariki ya Kati. Lakini nadhani inaweza kuwa almasi.”
"Tunampongeza" "mfalme" wa Jordan kwa mafanikio yake ya wastani katika kufikia mwonekano "wa makini". Alipendekeza kwamba Misri na madikteta wa Kiarabu wangeitisha mkutano mwingine, akiahidi pendekezo ambalo liliweka akilini "maslahi bora ya Marekani" na "watu katika eneo hilo, hasa watu wangu wa Jordan".
"Maslahi bora ya Marekani", alisema, pasi na chembe ya kejeli. Kana kwamba maslahi ya watu wowote yanaweza kuwepo pamoja na ubeberu wa Marekani.
"Mfalme" huyo huyo alipigwa picha muda mfupi tu kabla, akitabasamu kutoka sikio hadi sikio alipokuwa amesimama karibu na Trump. Mwonekano wa shangwe wa mtu mwenye shauku ya kutimiza dori yake katika kuendeleza uuzaji wa Ardhi Iliyobarikiwa.
Usikosee, wakati Trump anatishia kuondoa misaada kutoka Jordan, ni kweli kwamba Jordan iko katika uhusiano wa upande mmoja na Marekani; isipokuwa inainufaisha Marekani na “Israel” kwa mizani isiyo ya usawa kwa gharama ya Umma wa Kiislamu. Jordan ina kambi za Marekani, inahakikisha usalama wa "Israel", na inasaidia kueneza hadithi ya kirongo ya kutoshindwa kwa "Israel" kwa kuangusha midoli yoyote ambayo Iran inatuma.
Vikosi vya Ulinzi vya "Israel", ambavyo vilidhalilishwa zaidi ya majeshi yote, havikuweza kuwashinda wapiganaji shupavu wa upinzani wa Palestina, ambao wanapigana kwa silaha zilizotengenezwa kwa mikono na idadi ndogo. Umbile la Kiyahudi lingekoma kuwepo ikiwa jeshi lolote la Waislamu lingejitokeza, kama vile la Syria, la Jordan, au la Misri.
Mwenyezi Mungu (swt) anayathibitisha haya katika Quran Tukufu,
[لَا يُقَاتِلُونَكُمْ جَمِيعًا إِلَّا فِي قُرًى مُّحَصَّنَةٍ أَوْ مِن وَرَاء جُدُرٍ بَأْسُهُمْ بَيْنَهُمْ شَدِيدٌ تَحْسَبُهُمْ جَمِيعًا وَقُلُوبُهُمْ شَتَّى ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَوْمٌ لَّا يَعْقِلُونَ]
“Hawatapigana nanyi kwa mkusanyiko isipo kuwa katika vijiji vilivyo zatitiwa kwa ngome, au nyuma ya kuta. Wao kwa wao vita vyao ni vikali. Utawadhania kuwa wako pamoja, kumbe nyoyo zao ni mbali mbali. Hayo ni kwa kuwa wao ni watu wasio na akili.” [Surah Al-Hashr 59:14].
Makubaliano ya hivi karibuni ya mkuu mpya wa jeshi la "Israel", Eyal Zamir, yanathibitisha msimamo dhaifu wa IDF: "Takwimu rasmi za jeshi la 'Israel' zinasema kwamba maafisa na wanajeshi 844 wa 'Israel' wameuawa huko Gaza tangu kuanza kwa vita mnamo 7 Oktoba 2023 na karibu 5,696 kujeruhiwa. Takriban 'Waisrael' 1,200 waliuawa katika mashambulizi ya Hamas ya 7 Oktoba 2023, ikiwa ni pamoja na wanajeshi 400, kulingana na data rasmi. Zamir alisema kulikuwa na angalau 5,942 "familia zilizofiwa" zilizosajiliwa tangu 7 Oktoba, huku baadhi ya zikiwa na uwezekano wa kuwa na zaidi ya mwanafamilia mmoja aliyeuawa katika vita vya Gaza. Aliongeza kuwa kuna zaidi ya askari 15,000 waliopata majeraha ya mwili na kiakili na wameingizwa kwenye mfumo wa ukarabati. (Chanzo: https://www.newarab.com/news/israeli-new-army-chief-admits-gaza-losses-higher-reported)
Huku Trump na madikteta wake watiifu wa Kiarabu wakipongeza makubaliano ya kusitisha mapigano ya Gaza kama wakati wa afueni kwa watu wa Gaza, inazidi kuwa wazi kwamba usitishaji huo wa mapigano uliipa tu "Israel" fursa ya kujipanga upya na kuelekeza juhudi zake katika kuvamia Ukingo wa Magharibi, ikisaidiwa na Mamlaka ya Palestina.
Madikteta wa Kiarabu, kwa amri ya bwana wao wa Marekani, hufunga tu mikataba inayoisaidia tu uvamizi wa Wazayuni pekee. Badala ya kutuma majeshi yao kuikomboa Ardhi Iliyobarikiwa, wanaipatia “Israel” mboga, mafuta, hifadhi ya kidiplomasia, likizo jijini Dubai, ushirikiano wa kijeshi, na ahadi ya kuhalalisha zaidi mahusiano.
Kwa hivyo, huku Trump akiongeza maradufu mpango wake wa kuitakasa kimbari Palestina, madikteta hao wa Kiarabu wanajihusisha tu na ukumbi ili kuwahadaa watu wao, kwani wanaogopa maasi. Maasi kama yale yaliyowafanya Bashar Al-Assad na Sheikh Hasina kukimbia kwa kushindwa na kwa udhalilifu. Dikteta wa Jordan ana hamu sana ya kumfurahisha Trump hivi kwamba aliachana na usanii wowote haraka zaidi kuliko El-Sisi wa Misri.
El-Sisi wa Misri, anayejulikana kama "jenerali" na Trump, alikataa ziara yake ya Washington. Jenerali huyo alijitolea kuendelea na maigizo yake kwani anahofia kupoteza kiti chake cha utawala. Kama tulivyoona kwa Rafah, hata hivyo, mistari nyekundu ya El-Sisi iko tu katika hotuba zake.
"Mfalme" wa Jordan anaendelea kujidhihirisha kama kibaraka wa Magharibi na mtu asiyestahili kutawala Ash-Shaam. Ardhi za Ash-Shaam zimebarikiwa na Mwenyezi Mungu (swt), kama ardhi za riziki, kitovu cha Waislamu, ardhi za Mitume (as), na Ardhi Teule za Mwenyezi Mungu (swt).
Ujasiri, ustahamilivu, na Iman ya Waislamu wa Syria na Palestina ni chimbuko la fahari na msukumo kwa Umma wa Kiislamu.
Mtu muoga anayekaa katika kasri la Jordan na kujiita mfalme hastahili kutawala Waislamu waheshimiwa wa Jordan. Uwepo wake unahakikisha tu kuendelea kuuzwa kwa Ardhi Iliyobarikiwa.
Tunawashajiisha Waislamu jasiri wa Jordan wajitahidi kumuondoa dhalimu huyu na kubeba bendera ya Uislamu mbele.
"Operesheni ya Kimbunga cha Jordan", inayoongozwa na Shaheed Amer Qawwas na Shaheed Hossam Abu Ghazala, ni chanzo cha fahari na faraja kwa wanaume wa Jordan, haswa wanajeshi wanyoofu katika jeshi la Jordan. Operesheni hiyo pia ilionyesha wazi kwamba njia ya kung'oa utawala wa Kizayuni haihusishi utiifu kwa "mfalme" ambaye analinda uvamizi huo kwa uwajibikaji.
"Mfalme" wenu ni kizingiti dhaifu tu; ithibitisheni hofu yake kuwa ya kweli na mumuondoe. Al-Aqsa sio yake kuiuza. Wanajeshi wa Jordan, lini mtaitikia wito wa Amer na Hossam? Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina inakuiteni, ikikutakeni mutimize wajibu wenu wa kuikomboa. Ufurusheni uvamizi wa Amerika wa Wazayuni katika eneo hilo na muunganishe ardhi za Kiislamu chini ya Khilafah moja kwa njia ya Utume.
[انْفِرُواْ خِفَافًا وَثِقَالاً وَجَاهِدُواْ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ فِي سَبِيلِ اللّهِ ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ]
“Nendeni mtoke, mkiwa wepesi na wazito, na piganeni Jihadi kwa mali yenu na nafsi zenu katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Haya ni kheri kwenu mkiwa mnajua.” [Surah At-Tawbah 9:41]
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yunus Musab – Wilayah Pakistan