Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vijana Wamekwama ndani ya Janga la Kibepari

(Imetafsiriwa)

Kama vijana, idadi yetu ni takriban 16% ya idadi ya watu ulimwenguni- hiyo ni takriban vijana bilioni 1.2 (wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 24). Na haijalishi sisi ni nani, au tunaishi wapi, sote tunajitahidi kufikia jambo lile lile - mustakbali mzuri ambao tumeahidiwa, kutokana na bidii na kujitolea kwetu.

Lakini sote tunaishi katika ulimwengu ambao umejaa kutokuwa na uhakika - kwa zama za sasa na katika mustakbali. Kwani tunaishi ndani ya mfumo ambao umetupa:

- Mgogoro wa Uchumi Unaojirudia rudia, huku mwingine ukitabiriwa mwaka huu

- Kupanda kwa Viwango vya Mfumko wa Bei, kwani bei za bidhaa na huduma zilifikia kiwango cha mwaka baada ya mwaka cha 9.1% - kiwango cha juu zaidi tangu 1981 (Labor Department data)

- Kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira kwa vijana - Kwa wastani wa vijana milioni 73 wasio na ajira.

Takwimu hizi, na zengine, zinazidi kudhihirisha kuwa hatuwezi kutegemea mfumo huu kutulinda katika zama hizi za sasa.

Na bado, sote tunatafuta maisha hayo bora; kuhama kutoka eneo hadi eneo kutafuta kitu bora zaidi, lakini matokeo yake ni kwamba wanatulemeza zaidi na kuanguka ndani ya mfadhaiko kwani inatubidi kukabiliana na matatizo mbalimbali ya kijamii ambayo ni matokeo ya kuishi katika Mfumo wa Kibepari wa Kisekula.

Kutokuwa na uhakika huku si jambo la kawaida kwa sisi tunaoishi katika ulimwengu unaoendelea- tunaambiwa kwamba kuishi katika nchi ambazo bado hazijafanikiwa kuwa dola za Kibepari, hufanya kutokuwa na uhakika huku kuwa jambo lisilo epukika. Kwamba matatizo tunayokabiliana nayo si matokeo ya Ubepari, ni matokeo ya miundombinu ya dola, ukosefu wa uboreshaji, utamaduni wa kidini uliopitwa na wakati, ukosefu wa maadili ya kiliberali ndani ya jamii, vita, ... orodha inaendelea.

Kwa hiyo, tumejifunza kuwakubali, tukiamini kwamba tukikubali maadili yao na kutabanni njia yao ya maisha, tutakuwa na maisha bora sasa na katika mustakbali.

Lakini vipi kuhusu vijana wanaoishi katika ulimwengu ulioendelea? Ambako serikali zimetenganisha dini na maisha na kuzingatia usasa? Ambako wana miundombinu ya dola, maadili ya huria, utulivu ...

Je, nchi hizo hazina janga hili?

Jibu ni hapana.

Katika nchi hizo, vijana wanakumbwa na matatizo kila siku ambayo yanafanya maisha yao ya sasa na mustakabali wao kutokuwa na uhakika na kujaa viwango tofauti vya matatizo.

1) Nchini Uingereza, familia milioni 1.7 zinaweza kusukumwa katika ukosefu wa makaazi mwaka huu (Chanzo)

Na nchini Marekani, idadi ya wasio na makaazi inakadiriwa kuwa 552,830 (Chanzo)

2) Nchini Marekani, kijana 1 kati ya 5 yuko ndani ya deni (Chanzo).

Nchini Uingereza, zaidi ya theluthi (37%) ya vijana wamechukua mikopo kwa kutumia kadi za mkopo, mikopo ya akaunti (overdrafts) au vyanzo vyengine. Idadi huongezeka hadi 67% pindi mikopo ya wanafunzi na rehani zinapojumuishwa (Chanzo)

3) Nchini Marekani, takriban watoto milioni 5.7 kwa jumla - wamewahi kutumia dawa haramu za kulevya.

Nchini Uingereza, kulikuwa na vijana 11,013 waliotumia pombe na dawa za kulevya kati ya Aprili 2020 na Machi 2021.   

4) Nchini Marekani, kijana 1 kati ya 8 walikuwa wanatumia dawa haramu za kulevya katika mwaka uliopita. (Chanzo)

Nchini Uingereza, mmoja kati ya watoto kumi wenye umri wa miaka 17 atakuwa ametumia dawa kali za kulevya, kama vile ketamine na cocaine. (BBC)

5) Nchini Marekani, kuna kiwango cha mauaji ya bunduki miongoni mwa vijana ambacho ni mara 49 zaidi ya kile cha mataifa mengine yaliyoendelea. Kila siku, Wamarekani watatu hadi wanne chini ya umri wa miaka 18 wanauawa kwa bunduki. (Chanzo)

6) Nchini Uingereza, takriban watoto 27,000 wako katika magenge (Chanzo)

Na takriban watoto 12,720 (nchini Uingereza) wako katika hatari ya kutumiwa vibaya na magenge mwaka wa 2020/21 (Chanzo)7) Nchini Marekani, watoto na vijana wapatao 42,000 waligunduliwa kutoridhishwa na maisha (dysphoria) ya kijinsia mnamo 2021. Na zaidi ya miaka mitano iliyopita, kulikuwa na angalau vijana 4,780 ambao walianza kutumia vizuizi vya kubalehe na waligunduliwa kabla kutoridhishwa na maisha (dysphoria) ya kijinsia. (Chanzo)

8) Nchini Uingereza, Mtoto mmoja kati ya sita wenye umri wa miaka mitano hadi 16 aligunduliwa kuwa na tatizo la afya ya akili mnamo Julai 2021. Na karibu nusu ya watoto wa miaka 17-19 walio na ugonjwa wa afya ya akili waliogunduliwa na ugunjwa wa kiakili wamejidhuru au kujaribu kujiua wakati fulani. (Chanzo).

In the UK, there were 73,518 recorded offences including rape, online grooming and sexual assault against children in 2019/20 (Source)

10) In the USA, more than half of births to American women under 30 occur outside marriage. (Source)

Nchini Marekani, zaidi ya kijana 1 kati ya 10 anakumbwa na mfadhaiko ambao unaathiri sana uwezo wao wa kufanya kazi shuleni au kazini, nyumbani, pamoja na familia, au katika maisha yao ya kijamii. (Chanzo)

9) Nchini Marekani, kuna takriban wahasiriwa 463,634 (wenye umri wa miaka 12 au zaidi) wa ubakaji na unyanyasaji wa kijinsia kila mwaka.

Nchini Uingereza, kulikuwa na uhalifu 73,518 uliorekodiwa ikiwemo ubakaji, ushurutishaji wa kingoni mtandaoni na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya watoto mnamo 2019/20 (Chanzo)

10) Nchini Marekani, zaidi ya nusu ya wanaozaliwa na wanawake wa Marekani wenye umri chini ya miaka 30 huzaliwa nje ya ndoa. (Chanzo)

Nchini Uingereza, watoto 320,713 waliozaliwa hai walikuwa wa wanawake ambao hawakuwa katika ndoa au walikuwa katika mahusiano ya kiraia wakati watoto wao walipozaliwa. (Chanzo)

Haya ni baadhi tu ya matatizo yanayotia wasiwasi ambayo vijana katika nchi zilizoendelea wanakumbana nayo kila siku- na kuna mengi zaidi. Vijana na watoto kutoka katika malezi yenye misngi ya kidini (wawe Waislamu au Wakristo) wanachagua kuwa wapagani; uonevu wa mtandaoni ni suala muhimu miongoni mwa wanafunzi; shinikizo la marika linatusukuma katika hali ambazo ima tunakosa raha kuwa nazo au kihakika zinaweza kutuweka katika hali hatari.

Kwa hiyo, sasa ni lazima tukae chini kwa dakika na kufikiri. Ikiwa haya yote ni matatizo yanayowakabili vijana katika nchi zilizoendelea, iwe Ubepari, Demokrasia au Uliberali unadaiwa kuwa ‘unafanya kazi’ basi tunawezaje kuuamini Ubepari, Demokrasia au Uliberali kutatua matatizo yetu?

Tunaweza kuja na visingizio vyote duniani kwa nini matatizo hayo yapo; kulaumu watu binafsi, kusema kuwa ni matukio ya kipekee na kadhalika.

Lakini ukweli unabaki kuwa mfumo huu hautatui matatizo yetu, au kutupa tumaini la maisha bora ya baadaye. Unafanya maisha yetu kuwa ya dhiki. Na kuukataa hakutufanyi turudi nyuma, au kutuzuia kuwa ‘wafikiriaji huru’. Kuukataa kunamaanisha kwamba sisi ni watu wanaofikiri, ambao wameelewa tatizo kutoka katika chanzo chake na wanatafuta njia ya kulitatua.

Kwa sababu sasa hivi, tumenaswa katika ulimwengu ambao tumekwama katika mfumo unaotufelisha kila siku. Mfumo ambao manufaa ya watu wachache yanawekwa juu ya ulinzi na ustawi wetu. Mfumo ambao mawazo ya ‘uhuru’ yanatuweka katika njia mbaya. Mfumo ambao ndani yake tunahimizwa kuuweka pembeni Uislamu, pamoja na hukmu zote ambazo zingetulinda.

Tunaweza kufuata baadhi ya hukmu za Uislamu, kama watu binafsi, wakati tunapoendesha maisha yetu ya kila siku. Lakini hadi Uislamu utakapotabikishwa, kwa ujumla wake, hatutapata ulinzi wake katika kila nyanja ya maisha yetu. Na tutaendelea kupitia maisha ndani ya Mfumo wa Kibepari, uliojaa majanga.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fatima Musab
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Fuatilia na Usambaze Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

 #HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu