Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Kusimamisha Sheria ya Mwenyezi Mungu Duniani

Ni Ahadi ya Uongozi wa Kweli ambayo Hujadidishwa Hadi Mwenyezi Mungu Akamilishe Miadi Yake

(Imetafsiriwa)

Utukufu ni Wake ambaye amemuumba mwanaadamu na kumtengeneza, akampulizia roho, na akamtunukia akili. Utukufu ni Wake ambaye amempeleka Mjumbe Wake kuwa ni rehma kwa walimwengu na kuwatoa katika giza la ukafiri kwenda kwenye mwangaza wa imani. Utukufu ni Wake, ambaye ameteremsha Kitabu Chake kwa Mtume Wake, Aliyemchagua, kuwa ni alama na taa yenye kuangaza njia kwa watu wote. Utukufu ni Wake ambaye amesema:

[وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنْسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ * مَا أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ وَمَا أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ]

Nami sikuwaumba majini na watu ila waniabudu mimi. Na sitaki kwao riziki wala sitaki wanilishe.” [Adh-Dhariyat: 56-57]. Utukufu ni Wake ambaye amesema:

[قُلْ إِنَّ صَلاَتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ * لاَ شَرِيكَ لَهُ وَبِذَلِكَ أُمِرْتُ وَأَنَاْ أَوَّلُ الْمُسْلِمِينَ].

“Sema : Hakika Swala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote. Hana mshirika wake. Na hayo ndiyo niliyoamrishwa, na mimi ni wa kwanza wa Waislamu.” [Al-An'am: 162-163].

Mwenyezi Mungu ameumba waja Wake na kuchukua ahadi kwamba watashuhudia kuwa Yeye ndio Mola wao

[وَإِذْ أَخَذَ رَبُّكَ مِن بَنِي آدَمَ مِن ظُهُورِهِمْ ذُرِّيَّتَهُمْ وَأَشْهَدَهُمْ عَلَى أَنفُسِهِمْ أَلَسْتُ بِرَبِّكُمْ قَالُوا بَلَى شَهِدْنَا أَن تَقُولُوا يَوْمَ الْقِيَامَةِ إِنَّا كُنَّا عَنْ هَذَا غَافِلِينَ]

“Na pale Mola wako Mlezi alipowaleta katika wanaadamu kutoka migongoni mwao kizazi chao, na akawashuhudisha juu ya nafsi zao, akawaambia: Je, Mimi si Mola Mlezi wenu? Wakasema: Kwani! Tumeshuhudia. Msije mkasema Siku ya Kiyama sisi tulikuwa tumeghafilika na hayo.” [Al-A’raf: 172].

Ameleta sheria zake ili wale walioko duniani waweze kuishi maisha bora, wakihakikishiwa kwa hukumu zake kuwa hawatoingia kwenye batili au kwenye dosari, zitakazosimamishwa miongoni mwao na kiongozi mcha Mungu. Mwenyezi Mungu (swt) ameuchagua Ummah wa Mtume Wake (saw) kuwa ummah bora ulioletwa kwa watu wanaolingania mema, kuamrisha mema na kukataza maovu, kuwa ni Ummah ambao unaongoza ummah nyengine kwa kile kinachomridhisha Yeye, Utukufu ni Wake

[كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْراً لَّهُم مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma waliotolewa kwa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa watu wa Kitabu nao wameamini ingelikuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu.” [Aali-’Imran :110].

Moja ya Sunnah Zake, Aliyetukuka, ni kuwa amefanya uongozi kuwa ni hitajio la maisha kuendesha mambo ya viumbe Vyake, hivyo makundi ya ndege wana kiongozi anayewaongoza, na ng’ombe na wanyama wanaye anayewaongoza, pamoja na wadudu na nyuki… Wote ni umma kama wanaadamu  

[وَمَا مِنْ دَابَّةٍ فِي الأَرْضِ وَلا طَائِرٍ يَطِيرُ بِجَنَاحَيْهِ إِلَّا أُمَمٌ أَمْثَالُكُمْ مَا فَرَّطْنَا فِي الْكِتَابِ مِنْ شَيْءٍ ثُمَّ إِلَى رَبِّهِمْ يُحْشَرُونَ]

“Na hapana mnayama katika ardhi, wala ndege anayeruka kwa mbawa zake mbili, ila ni umma kama nyinyi. Hatukupuuza Kitabuni kitu chochote. Kisha kwa Mola wao Mlezi watakusanywa.” [Al-An'am:38].

Uongozi ni mamlaka ya kuwaongoza na kuendesha maisha, na ni suala la msingi kwa utekelezaji wake. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ameiweka bay’ah kwa kiongozi Ummah wa Kiislamu ili kutekeleza hukmu za Mwenyezi Mungu na Amewajibisha kwa Ummah kumtii Yeye isipokuwa akiwaamrisha kuasi hapo hatosikilizwa wala kutiiwa.

Mtume (saw) alikuwa kiongozi wa mwanzo wa Ummah wa Kiislamu na ni mtu mtukufu zaidi anayejulikana kwa wanaadamu; amefikisha ujumbe, ametimiza amana, na ameuwacha Ummah wa Kiislamu ukiwa mtukufu na wenye nguvu, ulioongoza mataifa na kueneza mwanga na uongofu wa Mwenyezi Mungu, na wanaadamu hawajashuhudia kiongozi mtukufu zaidi kuliko yeye; Yeye ndiye aliyewaleta watu pamoja wakiwa katika makabila na asili, makundi na rangi tofauti chini ya bendera ya “Laa ilaaha illallah”, akivunja mipaka na kuunganisha nyonyo.

Kumuabudu Mwenyezi Mungu maana yake ni kuijaza watu ardhi na kueneza hikma Zake juu yake. Yaani amana ambayo mbingu, ardhi, na milima ilikataa kuibeba na ambayo mwanaadamu aliichukua. Mitume na Manabii waliipokea, na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alikuwa ni wa mwisho wao kuitekeleza amana hii kubwa kwa kiwango cha hali ya juu kabisa na kumridhisha Mola wake na akimshuhudia kuiweka amana hii kwa Ummah wake kuendelea kutembea juu ya njia yake na kufuata njia yake katika kutekeleza ahadi alizoziweka kuihifadhi dini ya Mwenyezi Mungu na kuieneza duniani kote.

Ilikuwa ni ahadi ya kiongozi mkweli, muadilifu, muaminifu, asiye na jengine ila kumridhisha Mola wake na kueneza sheria zake kwa watu wote ili maisha yawe kama Mwenyezi Mungu anavyopenda na kuridhika nayo kwa waja Wake.

[فَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّن كَذَبَ عَلَى اللَّهِ وَكَذَّبَ بِالصِّدْقِ إِذْ جَاءَهُ أَلَيْسَ فِي جَهَنَّمَ مَثْوًى لِّلْكَافِرِينَ * وَالَّذِي جَاءَ بِالصِّدْقِ وَصَدَّقَ بِهِ أُولَئِكَ هُمُ الْمُتَّقُونَ * لَهُم مَّا يَشَاءُونَ عِندَ رَبِّهِمْ ذَلِكَ جَزَاءُ الْمُحْسِنِينَ]

 “Basi ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule aliye msingizia uwongo Mwenyezi Mungu na kuikanusha kweli imfikiapo? Je! Sio katika Jahannamu makaazi ya hao makafiri? Na aliyeileta kweli na akaithibitisha – hao ndio wacha mungu. Watapata watakacho taka kwa Mola wao Mlezi. Hayo ndiyo malipo ya watendao mema”. [Az-Zumar: 32-34]

Na juu ya njia yake, masahaba zake walitembea, na walikuwa kwenye kile alichowawekea na kile alichowafundisha katika kuihifadhi dini na kufanya kazi kuieneza, kutekeleza maslahi ya Ummah, kueneza uadilifu na amani, na kujitahidi kutosheleza mahitaji ya kila mtu anayehusiana na serikali ya Kiislamu na katika kuhudumia dini na kusimamisha neno lake, wanatumia fedha zao, na kwa ajili ya maisha ya baadaye na kwa ajili ya radhi za Mwenyezi Mungu wanatumia kile walichonacho. Wanafanyakazi katika kuimarisha utekelezaji wa hukumu zake juu ya waja, kuwahofisha kwa Mwenyezi Mungu na juu ya ghadhabu Zake kama watakuwa na upungufu au kutenda makosa. Wanahudumia raia zao na kuwapatia mahitaji yao, hasa vikongwe, na wale wasio na wasimamizi. Na habari ya bibi kipofu aliyehudumiwa na Abu Bakar, Khalifah wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, na baadaye kuendelea kuhudumiwa na Omar Ibn Al-Khattab (ra), ni mfano mwema wa mashindano kwa huduma bora na raha ya mmoja wao kwa ajili ya mwengine kwa hilo ni “Wewe umewamaliza Makhalifah baada yako, Ewe Abu Bakar…” Wamechukua nafasi ya uongozi baina yao, na kila mmoja kati yao akijibidiisha kuitekeleza kwa wema katika namna ambayo itamridhisha Mwenyezi Mungu. Na wakimhofu Mwenyezi Mungu hata kwa ajili ya ndege (wakieneza mapenzi kwao ili wasikae na njaa) na wanyama (wakiwasawazishia njia ili wasijikwae)!

Uaminifu ulitekelezwa na Makhalifah wa Waislamu, kila mmoja kwa kadiri ya uchamungu wake na hofu kwa Mwenyezi Mungu (swt). Wamejitahidi kuihifadhi dini hii na kuilinda na kuieneza katika maeneo yote ya dunia ili neno la Mwenyezi Mungu liwe juu na hukumu ziwe kwa Mwenyezi Mungu Mmoja tu, lakini maadui wa dini hii na kwa msaada wa kikundi kidogo cha vijana wa Ummah waliomkhini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na kupuuza amana na kuiuza, waliweza kuiangusha dola ya Khilafah. Umbo la kisiasa linaloihifadhi dini na ambalo linaegemea juu ya utekelezaji wa sheria zake, wameligawanya katika vijidola tofauti tofauti na wakaweka humo mawakala wao, kwa msingi wa maslahi yao na kuwahifadhia uporaji wa utajiri na ardhi ya Ummah. Mambo yalipewa wale wasiostahiki, na mambo yanapopewa yule asiyestahiki basi tusubiri kuja kwa kiyama kama Mtume (saw) alivyotuambia: «إِذَا ضُيِّعَتْ الْأَمَانَةُ فَانْتَظِرْ السَّاعَةَ» قَالَ: كَيْفَ إِضَاعَتُهَا يَا رَسُولَ اللَّهِ؟ قَالَ: «إِذَا أُسْنِدَ الْأَمْرُ إِلَى غَيْرِ أَهْلِهِ فَانْتَظِرْ السَّاعَةَ» “Amana itakapopotea basi isubiri Saa ya Kiyama” Pakaulizwa, “Vipi kupotea kwake, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu?” Akasema, “Watakapopewa mamlaka wale wasiostahiki, basi isubiri Saa ya Kiyama” [Imepokewa na Al-Bukhari].

Mambo yanawachiwa wale wasioshughulika na kuwahudumia watu na hawasimamii maslahi yao. Wanawabebesha mizigo ya kodi na bei kubwa, na wanawanyima utajiri ambao Mwenyezi Mungu amewapatia. Mambo yameachiwa wale wanaouza nchi na kueneza dhulma miongoni mwa watu na kueneza uchafu na ufisadi miongoni mwao.

Basi wako wapi wale wanaosimamia maslahi ya watu na kuwatawala kwa mfumo wa kibinadamu unaojali maslahi ya wachache na kuwakandamiza walio wengi ambapo watoto wanataabika duniani (vita, ukame, unyanyasaji wa kimwili na wa kijinsia)?! Wako wapi na hofu wanayoishi nayo na kuhamahama kwa watu hawa, hasa watoto wa Waislamu?! Wako wapi wale wanaotawala kwa mfumo usioweza kutoa huduma na ambao hauwapatii mahitaji ya kibinadamu ambapo maelfu ya watoto wanafariki kwa njaa au wanaoponea kwa majani na mabaki ya vyakula ili kupitisha siku?! Na ilhali ni watoto wa Ummah walio na utajiri, basi ni kipi kinacho wadhaminia maisha bora?!

Kuna tafauti kubwa baina ya watu hawa na wale wanaohukumu kwa sheria za Mwenyezi Mungu, wanahuruma kwa watoto na kuwaheshimu wazee! «لَيْسَ مِنَّا مَنْ لَمْ يَرْحَمْ صَغِيرَنَا وَيُوَقِّرْ كَبِيرَنَا» “Sio katika sisi yule asiyewarehemu wadogo wetu na kuwaheshimu wakubwa wetu” [Imepokewa na Abu Dawud na Tirmidhi]

Kuna tafauti baina yao na wale wanaopangusa vichwa vya mayatima na kuwapatia yale wanayoyahitaji!

Wako wapi watawala leo wakati kuna wanaotaabika kutokana na umasikini na kukosa ajira?! Wako wapi vijana wa Ummah wanaomaliza maisha yao kwa kujinyonga, kuzama, au kuungua wakati milango yote imefungwa machoni mwao, na maisha yao yamekuwa ya kiza na ya kukata tamaa, na kuchanganyikiwa kumekuwa ndio kitambulisho chao?!

Wako wapi na maumivu ya vijana wetu wakati wakiwa wamezungukwa na mto wenye nguvu wa mitihani na majaribu?! Wanaishi maisha yanayowavuta kwenye makatazo yote na yanayowakataza usafi na utakaso wa kijinsia! Wako wapi waliochukua amana na kujitahidi kuihifadhi na kumhofu Mwenyezi Mungu katika ujana, ili wawasaidie kufunga ndoa, kuwasamehe na kuwasaidia kutosheleza matashi yao kwa mujibu wa sheria ambazo Mwenyezi Mungu (swt) ameziagiza na kuziridhia?! Kutoka kwa Abu Huraira (ra) amesema, Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) amesema, «ثَلَاثَةٌ حَقٌّ عَلَى اللَّهِ عَوْنُهُمْ؛ الْمُجَاهِدُ فِي سَبِيلِ اللَّهِ، وَالْمُكَاتَبُ الَّذِي يُرِيدُ الْأَدَاءَ، وَالنَّاكِحُ الَّذِي يُرِيدُ الْعَفَافَ» Watu namna tatu Mwenyezi Mungu ana haki ya kuwasaidia: Anayepigana Jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, na mtumwa anayetaka kujikomboa, na anayeoa ambaye anataka maisha ya kujitakasa kutokana na uchafu.”

Wako wapi watawala hivi leo wakati vijana hawawezi kujikimu gharama za ndoa au kusaidia familia na kutosheleza gharama (ukosefu wa kazi umeenea na gharama za ndoa na maisha ni kubwa mno…)?!

Wako wapi watawala, wakati mwanamke anaponyanyaswa, kukandamizwa, kutiwa utumwani, kudanganywa kwa kauli za uhuru na haki wakati yuko katika minyororo, akisubiri wakumuacha huru kutoka kwenye maisha haya ya taabu yanayomfanya apoteze ujanajike wake ambao Mwenyezi Mungu amemuumba nao?!

Wako wapi wale wanaodai kuongoza ulimwengu kutokana na ukame, umasikini, ukosefu wa kazi na vita ambapo dunia yote imeathirika navyo?! Kutoka kwenye maisha ya ovyo, vifua vya watu vimebinywa na shingo zao zimebanwa, wakisubiri mfumo mwengine unaojali maslahi ya watu wote: masikini na tajiri, wadogo na wakubwa, wanaume wao na wanawake wao, unaomhudumia mwanaadamu kama mwanaadamu?!

Je, ana mfumo bora zaidi kuliko ule wa Muumba kushughulikia maslahi yake na kutosheleza mahitaji yake?

[أَلاَ لَهُ الْخَلْقُ وَالأَمْرُ تَبَارَكَ اللّهُ رَبُّ الْعَالَمِينَ]

Fahamuni! Kuumba na amri ni zake. Ametukuka kabisa Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote!” [Al-A’raf: 54]

Wao wako wapi na wapi na viongozi wakweli wenye ufahamu juu ya amana ambayo Mwenyezi Mungu amewakabidhisha kwa waja Wake na kuwa imebebwa na viumbe bora zaidi, masahaba zake, na kila ambaye ni mkweli kwa Mwenyezi Mungu? Yeyote aliye mkweli na akawa anatekeleza amana ataokoka, na anayekosa na kudanganya amekhini na atajuta siku ambayo majuto hayatamfaa!

Uongozi wa kweli unabeba wito wa Mwenyezi Mungu na unakumbusha ukweli pamoja na Mwenyezi Mungu, unabeba ushughulikiaji wa ujumbe huu na ushughulikiaji wa dini hii na unafanyakazi kuihifadhi na kuitukuza juu ya ardhi, bila kujali lawama ya mwenye kulaumu na sio wenye kuvunjwa moyo na wachache wanaofuata njia hii. Ni ule unaofanya kazi kuongoza sheria za Mwenyezi Mungu na kujengwa juu ya kumfanya atawale ardhi kwa nguvu zote na mshikamano. Hana maridhiano (na maadui wa Uislamu), hana kijalizo (juu ya mambo ya dini), havumilii (juu ya ukiukaji sheria). Una ushupavu wa kushinda wasiwasi wote, na uimara na ushujaa, unakataa kila uzembe au kurudi nyuma. Ni uaminifu na unyenyekevu wake kwa Mwenyezi Mungu, Msaidizi, Mtoaji ushindi, Mwenye nguvu zaidi.

Uongozi wa kweli ni jukumu, na kila anayemhofu Mwenyezi Mungu hahofii kuutendea haki yake في رواية عن أبي ذرّ قال: قلت يا رسول الله، ألا تستعملني؟ فضرب بيده على منكبي ثم قال: «يَا أَبَا ذَرٍّ إِنَّكَ ضَعِيفٌ، وَإِنَّهَا أَمَانَةُ، وَإِنَّهَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ خِزْيٌ وَنَدَامَةٌ، إِلَّا مَنْ أَخَذَهَا بِحَقِّهَا، وَأَدَّى الَّذِي عَلَيْهِ فِيهَا»  “Kutoka kwa Abu Dharr alimwambia Mtume (saw): Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, hunipatii uongozi (ugavana)? Mtume (saw) akampigapiga begani kisha akamwambia: “Ewe Abu Dharr, wewe ni dhaifu, na huu uongozi ni amana, nao siku ya kiyama itakuwa ni sababu ya hizaya na majuto, isipokuwa kwa yule atakayeuchukua kwa haki yake na kuutekelezea humo wajibu wake.” Katika mapokezi mengine alimwambia, “Ninakuona wewe ni dhaifu Abu Dharr, na ninakutakia kile ninachojitakia mimi. Usikubali utawala juu ya watu wawili na usiwe msimamizi wa mali ya mayatima.” [Imepokewa na Muslim]

Uongozi wa kweli ni ule ambao mazingatio yake yamejengwa juu ya utekelezaji wa hukumu za Mwenyezi Mungu juu ya watu kuangazia maisha yao pamoja nao, ili ukamilifu wa Sharia za Mwenyezi Mungu udhihiri katika kutatua matatizo yao, kuhifadhiwa mahitaji yao na kuhakikishiwa maisha bora. Kueneza haki na wema miongoni mwao na kuwafanya wajihisi salama na wataingia kwenye Uislamu kwa makundi. Kiongozi mkweli ni yule asiyeiona dunia isipokuwa ikitawaliwa, ikimilikiwa, na kuongozwa kwa sheria za Mwenyezi Mungu kwa sababu anauhakika wa ahadi ya Mwenyezi Mungu ya tamkini na ushindi kwa waja Wake waaminifu.   

Kiongozi mkweli ni yule anayeweka uaminifu mkubwa juu ya mazingatio yote, kama bwana wetu Abu Bakar, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, aliye chukua kutoka mbora wa viumbe na akasuhubiana naye katika hijra. ."فَمَنْ كَانَ مِنْكُمْ يَعْبُدُ مُحَمَّداً ﷺ فَإِنَّ مُحَمَّداً ﷺ قَدْ مَاتَ، وَمَنْ كَانَ يَعْبُدُ اللَّهَ فَإِنَّ اللَّهَ حَيٌّ لَا يَمُوتُ" “Yeyote kati yenu aliyekuwa akimuabudu Muhammad, basi Muhammad amekufa. Na yeyote aliyekua akimuabudu Mwenyezi Mungu basi Mwenyezi Mungu yuhai na hafi.”

Na katika hatua ya maamuzi, ikaweza kuunganisha umoja wa dola na kuondoa uasi.

Kiongozi mkweli ni yule asiyewadanganya watu wake, ni muaminifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na Waumini, hufanya kazi mchana na usiku kuregesha utukufu na heshima ya Uislamu na kuwaunganisha Waislamu chini ya bendera ya tawhid na kuwaunganisha katika dola moja ambapo chini ya kivuli chake wanaishi maisha ya ukakamavu na heshima na kutokana nayo wanawashinda maadui, wanawanyenyekesha, kuwatawala na kuwaongoza kwa hukumu za uadilifu za Mwenyezi Mungu.

Uongozi wa kweli ni ule unaoweka ahadi yake kwa Mwenyezi Mungu juu ya vitendo vyake, kwa sababu unaamini kuwa huu ni wajibu juu yake na dhima ya kisheria ambayo lazima kushikamana nayo. Ni uongozi ambao unajadidisha ahadi hii kila leo na kuhakikisha kuwa hakuna mapumziko kwa ajili yake hadi sheria za Mwenyezi Mungu zitawale dunia na Uislamu uregeshe utukufu wake na kuwa ni uongozi pekee unaowaleta watu kutoka kwa kiza cha hukumu za mwanadamu kwenda katika mwangaza wa hukumu za Mola wa walimwengu, uongozi unaojali utekelezaji wa sheria za Mwenyezi Mungu na kuishi chini ya kivuli chake.

Ni uongozi uliounganishwa ndani ya chama cha kisiasa, Hizb ut Tahrir, ambacho kinafanya kazi kuregesha maisha kamili ya Uislamu, hakitaki wadhifa na hakitafuti heshima ya kidunia, bali kinamhofu Mwenyezi Mungu kana kwamba kinamuona na ni chenye uaminifu katika utekelezaji wa ahadi ilichoweka hadi bendera ya tawhid ipae angani na dini yote iwe kwa Mwenyezi Mungu pekee na hakuna amri ila Kwake. Ni uongozi mtukufu ulioje huu ambao ni mkweli kwa Mola wake: kwake Yeye unategemea, na katika ahadi Yake umekamata na kuwa na yakini.

[مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]

Miongoni mwa Waumini wapo watu waliotimiza waioahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo. [Al-Ahzab: 23].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Zeina As-Samit

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu