Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ndio Bw. Blair! Licha ya Ajenda Karne Nzima ya Wamagharibi ya Kuigawanya Mashariki ya Kati

Mustakbali Hauna Shaka Utakuwa ni Uislamu Ulioamuliwa na Ummah

Tony Blair amethibitisha kuwa sio utaifa wala usekula utakaokuwa msingi wa fikra ya mapambano ya kisiasa katika Mashariki ya Kati, bali ni mapambano ya kisiasa katika Uislamu ambayo Uingereza na washirika wake wanaendelea kuyazuia.

Akijitokeza kama mgeni mtandaoni, katika taasisi ya Washington mnamo 11 Januari 2021 kwenye kipindi ‘Geopolitics 2021 – America, The Middle East, and the World’ alisema yafuatayo: “Uoni wangu uko wazi kabisa na Mashariki ya Kati bado ni yenye kuzingatiwa na huzingatiwa kupita kiasi. Inazingatiwa kwa sababu katika Mashariki ya Kati ndipo ujaji wa Uislam utaamuliwa…

…Hii ndio sababu ninaamini kuwa hakuna sera nzuri katika Mashariki ya Kati hivi leo isioanzia kutokea katika uchambuzi makini wa kile kilicho cha sawa na kisicho sawa tokea kuingia kwa karne, au ule uliosimama kutoka kwenye hoja ilioundwa kwa uongo kuhusu mapambano muhimu katika eneo. Kwa sababu vyenginevyo utamalizia katika hali ambayo utalifahamu eneo kuwa ni mapambano baina ya Iran na Saudi Arabia au baina ya Shia na Sunni. Hapana sio hivyo! Kwa kweli haiishii hivyo. Ni mapambano baina ya watu wanaosema kuwa dini hiyo—huenda ikawa uoni mmoja ni Uislamu—utawale na kugeuka kuwa itikadi ya kisiasa, na wale wasiotaka. Huo ndio mgawanyo wa maana sana na wa msingi…

…Na hivyo, ninafikiri ni muhimu sana sana kuwa tuendelee kutambua Mashariki ya Kati ni muhimu, ni suala la umuhimu mkubwa na kuwa kuna watu ambao tunapaswa kuwaunga mkono katika eneo na kuna watu ambao tunapaswa kuwazuia.”

https://www.washingtoninstitute.org/policy-analysis/america-middle-east-and-world-conversation-tony-blair

Kile kilicho cha sawa au kisicho cha sawa katika Mashariki ya Kati kwa miaka 100 iliopita ni wazi kuwa uwepo wa fikra za kigeni kama utaifa, Ukomunisti na Ubepari tokea kuvunjwa kwa Dola ya Khilafah ambayo imechukuliwa nafasi yake na tawala za wateja wa Uingereza au Amerika waliotawala, wakijishughulikia wenyewe pamoja na tabaka dogo na maslahi ya kigeni—badala ya kuwahudumia watu wa eneo. Watawala hawa kwa kiasi kikubwa wanachukiwa na watu wanaowatawala. Wanatumia majeshi kwa madhumuni mawili. Kwanza, kuwakandamiza watu wao wenyewe – hasa wanapoona mtikisiko wa ukosoaji wa kisiasa au hisia za Kiislamu; na pili kutumikia maslahi yoyote ya kijeshi ya Wamagharibi wanayotakiwa kuyatumikia.

Dola hizi kubwa zilizopo za wateja wa Wamagharibi ni Ufalme wa Saudi Arabia na Jordan. Saudi Arabia ilibuniwa katika Afisi ya Mambo ya Kigeni ya Uingereza kiasi cha karne moja iliopita na tokea hapo imeweza kufuja kiasi kikubwa cha mali. Familia ya utawala wake imenufaika na fungamano la karibu na Uingereza na Amerika tokea wakati huo. Jordan pia ni familia ya kibiashara, imesimikwa na Uingereza baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia. Uingereza imeweka wanafamilia, wanaoonekana kote kuwa ni wasaliti wa Uislamu na Waislamu, kutawala Iraq na kwa muda Syria – kwa kiasi cha kuona tu tawala zao za kifalme zikipinduliwa katika maeneo haya kwa mapinduzi na kupindua mapinduzi yanayo dhaminiwa mara nyingi na Uingereza na Amerika.

Kwa hivyo Ummah katika miaka 100 iliopita umeshuhudia sio tu kushindwa na matokeo ya maafa ya ubeberu wa Uingereza na sera za mwanzoni za kikoloni kupitia upandikizaji wao wa fikra za kigeni kama utaifa ambao unaelekeza kuuvunja umoja wa Kiislamu na Khilafah ya Uthmaniya bali ni kushindwa kunakoendelea na matokeo ya uvamizi wa kijeshi wa ‘kubadili utawala’ na uvamizi wa Iraq 2003 ambao umepandikiza kwa mabavu mgawayiko baina ya Waislamu wa Kishia na Kisunni unaopelekea mivutano ya mawakala baina ya Saudi Arabia na Iran nchini Yemen na Syria.    

Hata hivyo, katika mwaka 2021 ambapo mhalifu wa vita Tony Blair amefichua ukweli wa mapambano asili yaliyochukuwa miaka 100 ambayo ni baina ya walio katika ulimwengu wa Kiislamu wanaohangaika kurejesha Khilafah Rashida ambayo muda wote yamekuwa ni ya fikra za kisiasa kwa miaka 1400 na wale walio upande muovu wa historia ambao wamepotoka, waliorogwa na kuungwa mkono na maadui wa Uislamu kama Blair na vipote vya wanasiasa, asasi zao na mashirika.

Hivyo ni sawa kabisa kuwa mustakbali wa mapambano utaendelea kuwa wa Kiislamu katika Mashariki ya Kati na kote katika ulimwengu wa Kiislam na ndio mustakbali ambao Uingereza na washirika wake wanaendelea kujihusisha nao. Hata hivyo, ni Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake Mpendwa (saw) ambaye ametabiri matokeo ya mpambano huu mkubwa na kurudi kwa Dola ya kisiasa ya Khilafah Rashida kwa njia ya Mtume (saw) Mtukufu bi’idhnillah.

Kwa hiyo Khilafah sio matumaini tu; ni takwa la kisharia, ambapo uhakika wa kurejea kwake Muislamu aukubali kwa imani kubwa. Utajo huu wa kurejea kwake unapatikana katika hadith tofauti, lakini bila shaka ni kuwa moja ya hadithi maarufu zaidi ni hadith sahihi kutoka Musnad ya Imam Ahmad, ambapo Mtume Muhammad (saw) ameshatubashiria hali yetu ya sasa (na “hatua ambazo Ummah utazipitia baada ya kifo chake) na kutujulisha sisi juu ya kurejea kwa Khilafah baada ya kuanguka kwake.

Tutambue kuwa kuongezeka kwa ukandamizaji ambao waumini na wabebaji da’wah ya Uislamu wanakumbana nao bila shaka ni alama ya kurejea kwa Khilafah na uthibitisho kwa hili kwa wale wanaotaka kuchelewesha kisichoepukika. Mapokezi yanayoelezea masuala haya yapo mengi lakini mapokezi katika Musnad ya Imam Ahmad yanatupa ufupisho wa hali ya uongozi wa Ummah kote katika historia, ukiendelea kupitia hatua zinazoanza na uongozi chini ya Mtume (saw) na kumalizia kurejea kwa Khilafah kwa njia ya Utume.

Imam Ahmad b. Hanbal, ambaye pia alipewa cheo cha Amir al-Mu’minin katika fani ya Hadith, inayoonyesha ubingwa katika sayansi ya hadith, na muandishi wa kitabu maarufu cha Musnad kinachokusanya hadith 40,000, amepokea hadithi ifuatayo:

 حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ دَاوُدَ الطَّيَالِسِيُّ حَدَّثَنِي دَاوُدُ بْنُ إِبْرَاهِيمَ الْوَاسِطِيُّ حَدَّثَنِي حَبِيبُ بْنُ سَالِمٍ عَنِ النُّعْمَانِ بْنِ بَشِيرٍ قَالَ كُنَّا قُعُودًا فِي الْمَسْجِدِ مَعَ رَسُولِ اللَّهِ ﷺ وَكَانَ بَشِيرٌ رَجُلًا يَكُفُّ حَدِيثَهُ فَجَاءَ أَبُو ثَعْلَبَةَ الْخُشَنِيُّ فَقَالَ يَا بَشِيرُ بْنَ سَعْدٍ أَتَحْفَظُ حَدِيثَ رَسُولِ اللَّهِ ﷺ فِي الْأُمَرَاءِ فَقَالَ حُذَيْفَةُ أَنَا أَحْفَظُ خُطْبَتَهُ فَجَلَسَ أَبُو ثَعْلَبَةَ فَقَالَ حُذَيْفَةُ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ ﷺ: «تَكُونُ النُّبُوَّةُ فِيكُمْ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةٌ عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا عَاضًّا فَيَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ ثُمَّ سَكَتَ»

Ametuhadithia Sulayman b. Dawud Attayalis; Amenihadithia Dawud b. Ibrahim al-Wasitwy; Amenihadithia Habib b. Salim kutoka kwa Nu’man b. Bashir kuwa amesema: Tulikuwa tumekaa ndani ya msikiti, na Bashir alikuwa akimzuia mtu kusema (yakuffu hadithahu). Abu Tha’laba al-Khushani alikuja na akasema: Ewe Bashir b. Sa’d! Umehifadhi hadithi ya Mtume (saw) kuhusiana na watawala? Hudhaifah akasema: Mimi nimehifadhi khutba yake (SAW). Abu Tha’laba akakaa na Hudhayfah akasema: Mtume (saw) amesema: “Utakuwa Utume kwenu kwa muda ambao Mwenyezi Mungu anataka, kisha atauondoa muda anaotaka kuuondoa. Kisha itakuwa Khilafah kwa njia ya Utume na itakuwa kwa muda ambao Mwenyezi Mungu anataka na kisha ataiondoa muda Anaotaka. Kisha utakuwa utawala wa kurithishana na utakuwa kwa muda ambao Mwenyezi Mungu anataka, kisha atauondoa Anapotaka kuuondoa. Kisha utakuwa utawala wa kimabavu na utaendelea muda anaotaka Mwenyezi Mungu, kisha atauondoa muda Anaotaka kuuondoa. Kisha itakuwa Khilafah kwa njia ya Utume, kisha akanyamaza. [Musnad Ahmad, 4/273 #18596]

أقيموا_الخلافة#
#ReturnTheKhilafah
#YenidenHilafet
خلافت_کو_قائم_کرو#

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Tsuroyya Amal Yasna

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu