- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Kurejesha Tafakari ya Kiislamu
Muitikio wa Waislamu wa Pakistan juu ya matukio yanayouangukia Ummah duniani unafichua kuwa njia ya kufikiri ya Kiislamu inaongezeka katika ubora wake, umaarufu na ukamilifu.
Kuhusiana na matendo yanayofanywa na watawala wa Kiarabu kusawazisha mahusiano na uvamizi wa Mayahudi Palestina, kumekuwa na kukataliwa kukubwa kiasi kwamba serikali ya Pakistan imebidi kukataa mara kwa mara juu ya mwendo wake katika upande huo. Ni jambo la kuzingatiwa, kwamba kumekuwepo na kumbukumbu ilioenea sana kwa hatua za kukatikiwa za Dola ya Uthmaniya dhidi ya tamaa za Wazayuni juu ya Palestina, pamoja na mjadala juu ya katazo la kuisalimisha Ardhi ya Waislamu. Sura hii pia ina mfanano katika mjadala juu ya suala la Kashmir Iliokaliwa Kimabavu, ambapo wito wa Jihad kwa jeshi la Pakistan unabaki kuwa ni takwa (la Ummah).
Kuhusiana na udhalilishaji wa kiserikali, shambulio la Ufaransa dhidi ya heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), Waislamu wa Pakistan walijiandaa vyema. Ikiwemo malalamiko yenye athari, kumekuwepo na ususiaji uliopangika wa bidhaa za Ufaransa na miito ya kuondoshwa kwa ubalozi wa Ufaransa. Ni jambo lililo wazi kuwa, kumekuwa na mjadala kuhusiana na majibu ya Khilafah ya Uthmaniya juu ya mashambulizi kwa heshima ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kwa Uingereza na Ufaransa kabla ya Vita vya Kwanza vya Dunia. Kumekuwa na mlinganisho uliofanywa baina ya kitisho cha kutumia nguvu za kijeshi cha dola ya Uthmaniya, ikilinganishwa na shutuma zisizo na meno za watawala wa sasa.
Kuhusiana na mkandamizo wa kichokozi juu ya Uislamu barani Ulaya, ukiongozwa na Ufaransa na kuelekezwa na Uingereza, kuna shutuma zilizoenea za maadili ya kiliberali ya Magharibi kwenyewe na kutoweza kwao kutoa njia bora ya maisha kwa wanaadamu. Haya yakienda pamoja na uidhinishaji ulio na ari wa sheria za Kiislamu zinazotawala mambo ya kiutawala na kifamilia.
Ni hakika kuwa, kuna maendeleo yenye kutia moyo kuelekea katika kurejea kwa Uislamu kama kipimo cha kuhukumu masuala ya kisiasa na kijamii. Kabla ya kuangushwa kwa Khilafah miaka mia moja ya Hijria mwezi huu unaokuja wa Rajab 1442, tafakari ya Kiislamu ilikuwa na umaarufu mchache na kuparaganyika zaidi.
Kurejeshwa kwa tafakari ya Kiislamu katika ukamilifu wake bado hakujafikiwa, lakini ukweli wa kuwa ipo katika kutengenea ni jambo la kutia moyo. Hakuna njia kwa ajili ya kuuhuisha Ummah wa Kiislamu mbali na kurudisha tafakari ya Kiislamu, ambayo inajumuisha kuyahisi matatizo kulingana na kipimo cha Uislamu na kutaka suluhisho juu ya msingi wake. Huku Ummah ukirejea kwenye Uislamu, watawala hufarakana zaidi na zaidi na manunguniko, matarajio na matakwa ya Waislam.
Watawala hubakia wamefungika kwa ushupavu na mpangilio uliopo wa kiulimwengu, ambao umefinyangwa kwa mfumo wa kiliberali wa Kimagharibi. Wote wakihisi pengo linaloongezeka, pamoja na kushtushwa nalo, watawala hujaribu kwa hasira kuliziba kwa kushawishi na kujitetea, vikienda sambamba na hatua za utumiaji nguvu na vitisho.
Kuna hali isiohimilika na isiothabiti ndani ya Ulimwengu wa Kiislamu hivi sasa. Ima Waislamu warudi nyuma kutokana na kujitolea kwao kunakoongezeka kuelekea kuufanya Uislamu kuwa ni njia ya maisha, au watawala waondoke. Ni mkwamo wa upangaji hivi sasa, ukiwa na msukumo mkubwa dhidi ya walioshika nguvu za utawala, wakiwa ni vikosi vya jeshi na idara ya intelijensia. Kwa hakika, kujiweka kwao upande wa msimamo wa watawala unaoendelea kutokukubalika ni kuzuia msuguano usivunjike. Kwa upande wa Pakistan hasa, japokuwa jeshi ni lenye kuheshimika na Waislamu, hivi sasa linakabiliwa na dhihaka kwa kumuweka Imran Khan katika utawala.
Wakati maadhimisho ya miaka mia moja ya Hijria ya kuvunjwa kwa Khilafah yakikaribia mwezi huu unaokuja wa Rajab 1442, mambo yanasonga mbele. Kwa hakika, heshima kubwa inalisubiri jeshi tukufu ambalo kwanza litatoa Nussrah kwa ajili ya kurejea kwa kuhukumu kwa yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt). Kisha, wakati huo ndipo fikra ya Uislamu ndani ya Waislamu itakuwa katika mapatano na sera na matendo ya watawala, pamoja na sheria na katiba ya dola.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Hababri ya Hizb ut Tahrir na
Musab Umair - Pakistan