Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Muamala wa Aibu Ambao Kyrgyzstan Inaamiliana na Dada Zetu Waheshimiwa

Kyrgyzstan katika juhudi zake za kupambana na ile unayoitwa "misimamo mikali" imepelekea unyanyasaji mbaya kwa miaka mingi.

Mnamo 2018, Shirikia la Kutetea Haki za Kibinadamu la Human Rights Watch liliona kwamba katika Kifungu cha 299-2 cha sheria ya jinai ya Kyrgyzstan, hukumu inayo tekelezwa sana kuhusiana na umilikaji wa nyenzo zenye misimamo mikali ni kifungo cha kati ya miaka mitatu na kumi gerezani hata kama hakuna uchochezi wowote wa ghasia au ikiwa ugawanyaji kusababisha mamia ya watu kupatikana na hatia na kufungwa gerezani.  

Kwa uchache watu 258 wamepatikana na hatia nchini Kyrgyzstan tangu 2010 ya kumiliki nyezo zenye kufafanua waziwazi misimamo mikali. Hii ndio hukumu inayo tekelezwa sana nchini humu dhidi ya washukiwa wa ugaidi na misimamo mikali. 

Mamia ya washukiwa wangali wanasubiri hukumu juu ya mashtaka haya na kila mwaka idadi inaongezeka, huku kesi mpya 167 zikifunguliwa katika miezi tisa ya kwanza ya 2016.

Katika kesi nyingi mamlaka za Kyrgyzstan zimekuwa zikitumia kufungu cha 299-2 kuwafunga gerezani washukiwa kwa suluki zisizo za vurugu pekee kama vile kumiliki fasihi au video marufuku au utekelezaji wa Uislamu asili, Shirika la Human Rights Watch liligundua. 

Katika jaribio la kuficha uhalifu wao, Kyrgyzstan ilibadilisha sheria yake ya jinai mnamo Januari 2019, ikahalalisha umiliki wa video, matoleo, nyimbo, na nyenzo nyenginezo ambazo mamlaka zilizipa kibandiko cha misimo mikali.

Huenda ukadhani hizi ni habari njema, lakini uhalisia wa kusikitisha unahadithia tofauti na dhulma kwa Waislamu zinaendelea nchini Kyrgyzstan. Kuhusu sheria hiyo ya juu ya jinai wale ambao wangali wanasubiri hukumu kwa kosa lililofutiliwa mbali bado hawajaona mashtaka yao yakiondolewa, pia wale ambao tayari washapatikana na hatia wangali wako gerezani.

Ukamataji unaendelea kufanywa chini ya sheria nyenginezo za kawaida za jinai kama vile kuwa mwanachama wa yale ambayo serikali imeyapa kibandiko cha "mashirika ya misimamo mikali". Yeyote anayeikashifu serikali anaweza kukamatwa na kufungwa gerezani chini ya sheria hizi.

Unaweza ukawa umeketi na dada zako Waislamu mkinywa chai na mara nyumba yenu ikavamia kwa vurugu na Kamati ya Dola ya Usalama wa Taifa, ambao wamekuja kukukamata wewe na dada zako Waislamu bila ya kukupeni mda wa kusitiri uchi wenu, wakiamiliana nanyi visivyo na kuwazuia kutokana na kushughulikia mambo yenu muhimu. Jinamizi hili uhalisia wake ulikuwa mnamo 27 Juni ya mwaka huu, kwa kukamatwa wanane katika dada zetu waheshimiwa, majina yao yakiwa: Arunova Erkingul, Baktybek kyzy Mahabat, Ajumudinova Almagul, Ajumudinova Archagul, Ismailova Meerim, Kadyralieva Meerim, Aytbekova Gulnur, Mamirkanova Amangul. 

Wanawake hawa waheshimiwa ni kina mama wa watoto wadogo, baadhi yao ni walemavu, na ni wachungaji wa wazazi wao wakongwe na ni watu wasioweza kukosekana uwepo wao katika familia zao. Lakini hadi leo, wawili kati ya dada zetu hawa wangali wako gerezani pasi na ushahidi wowote na katika kipindi cha janga la maambukizi.

Kyrgyzstan, chini ya pazia la kupigana na ugaidi na misimamo mikali, kihakika wanapigana na Uislamu na Waislamu mithili ya nchi jirani zao China na Uzbekistan. Katika mchakato huu wameamua kwa uoga kuwakamata dada wanane walipokuwa wakinywa chai pamoja.

Dada hawa ni dada wa kila mmoja wetu. Wao ni washirika wa thamani zaidi wa Ummah huu. Kuwachukua kutoka kwa familia zao, kuwafunga gerezani na kuwakosea heshima katika vita vyenu dhidi ya kuibuka tena kwa Uislamu inaonyesha tu kutowajali kwenu wanawake na hatua za kutapatapa mulizochukua katika vita vyenu dhidi ya Uislamu.

Sisi, Ummah, tunataka waachiliwe huru mara moja dada hawa waheshimiwa na wafungwa wote wa kisiasa nchini mwenu ambao hawana hatia ya uhalifu wowote.

﴿إِنَّ الَّذِينَ يُحَادُّونَ اللَّهَ وَرَسُولَهُ أُوْلَئِكَ فِي الأَذَلِّينَ * كَتَبَ اللَّهُ لَأَغْلِبَنَّ أَنَا وَرُسُلِي إِنَّ اللَّهَ قَوِيٌّ عَزِيزٌ

“Hakika wanao mpinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hao ndio miongoni mwa madhalili wa mwisho. Mwenyezi Mungu ameandika: Hapana shaka Mimi na Mtume wangu tutashinda. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kushinda.” [TMQ Al‐Mujadilah 58: 20‐21]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yasmin Malik
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
 

مسلمات_قرغيزستان#   

#KırgızistanlıMüslümanKadınlaraÖzgürlük     

#FreeMuslimahsKyrgyzstan

#WaacheniHuruWanawakeWaKiislamuKyrgyzstan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 29 Agosti 2020 16:11

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu