- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
India ina Shaka juu ya Mahusiano ya Marekani
(Imetafsiriwa)
Marekani iliondoa vizuizi vyote wakati Waziri Mkuu wa India Narendra Modi alipozuru Marekani mwishoni mwa Juni katika ziara rasmi ya kiserikali. Modi, ambaye wakati fulani alinyimwa visa ya kusafiri kwenda Marekani kwa sababu ya wasiwasi juu ya haki za binadamu, alikula na kulala katika Ikulu ya White House na hata kuhutubia kikao cha pamoja cha Bunge la Congress. Marekani imetamani uhusiano wa kina na wa kimkakati na India tangu kugawanyika, ambao umechukua umuhimu zaidi na kukua kwa China. Lakini uhusiano kati ya Marekani na India haujafikia uwezo wake huku New Delhi ikiendelea kuwa na mashaka mbalimbali.
Wakati Marekani ilipoibuka kuwa dola kuu yenye nguvu duniani baada ya Vita vya Pili vya Dunia na Vita Baridi vilipokuwa vikianza, huko Asia Kusini watunga sera wa Marekani walikuja kuiona India kama dola yenye nguvu katika eneo hilo na taifa muhimu mno ambalo Marekani ililihitaji ili kuzuia kuenea kwa ukomunisti. Lakini waanzilishi wa India hawakutaka kuchukua upande katika Vita Baridi na walitafuta mahusiano mazuri na Marekani na Muungano wa Kisoviet. Wote wawili Gandhi na Nehru walitazamia India ambayo ilikuwa ya kisekula na iliyofuata muangaza wa mawazo ya Ulaya, huku katika uchumi walivutiwa na mtindo wa Kisoviet, na walitafakari mahusiano ya kina ya kiuchumi nao. Katika sera ya kigeni waanzilishi walijificha nyuma ya kutofungamana na mtu ili wasichukue upande katika Vita Baridi.
Kutokana na hali hiyo Marekani ililazimika kukaa na Pakistan kama mshirika wake katika eneo hilo ambaye kisha alijiunga na mashirika ya Vita Baridi yaliyoongozwa na Marekani na kupokea misaada na vifaa vya kijeshi vya Marekani. Maafisa wa Marekani hata hivyo waliendelea kuwasiliana na India ili kupata imani yake na kuiunganisha katika muundo wa muungano wake wa Vita Baridi. Wakati India ilipopigana vita na China huko Himalaya mnamo 1962 Marekani ilipeleka silaha India ili kuisaidia juhudi zake za vita.
Wakati Muungano wa Kisovieti ulipoporomoka mwaka wa 1991, mshirika mkuu wa kibiashara wa India sasa alikuwa ametoweka jambo ambalo lilisababisha mgogoro wa kiuchumi, ambao uliilazimisha New Delhi kugeukia IMF. Kutokana na masharti ya IMF yaliyohitaji ukombozi na hitaji la India la mtaji na uwekezaji katika miaka ya 1990, India ilipitia msukumo mkubwa wa ukombozi. Katika mgao wa amani baada ya kumalizika kwa Vita Baridi watunga sera wa Marekani waliona fursa mpya ya kujishindia India.
Kwa kukua kwa China katika miaka ya 2000, umuhimu wa India ukawa wa dharura zaidi kwa Marekani. Mnamo 2005, Waziri wa Mambo ya Nje wa wakati huo wa Marekani Condoleezza Rice alisema kwamba kuisaidia India kuwa dola ya kimataifa lilikuwa ni lengo la sera ya Marekani. Kufikia mwaka wa 2006, Bunge la Congress la Marekani lilipitisha Mkataba wa kihistoria wa Nyuklia wa India-Marekani ambao ulifungua njia ya kuhamisha teknolojia ya nyuklia ya kiraia hadi India. Hii pia iliondoa vikwazo vyote vya Marekani kwa India baada ya majaribio ya nyuklia ya 1998.
Lakini licha ya msukumo wa Marekani wa kusawazisha mahusiano na India, kumekuwa na changamoto nyingi. India na Marekani hazina makubaliano ya biashara huria kati yao. Kampuni za Marekani kwa muda mrefu zimekuwa zikitaka ufikiaji wa soko kubwa la ndani la India na tawala mtawalia jijini New Delhi zimelinda soko la ndani kwa sera za ulinzi. Lalamiko kuu la Marekani dhidi ya India ni matumizi yake ya vikwazo vya ushuru na visivyo vya ushuru kuwakinga wazalishaji wa kilimo na kuchagua viwanda vya utengenezaji.
Lakini pamoja na matatizo haya Marekani imefanya katika miaka ya hivi karibuni mikataba mingi ya kiuchumi ambayo ilitarajia itafungua njia ya uhusiano wa kina. Marekani imesema inapanga kutoa ufadhili kwa ajili ya kuanza kwa teknolojia ya India na miradi ya miundombinu kutoka kwa Mfuko wake wa Ushirikiano wa Kimataifa wa Miundombinu na Uwekezaji (PGII) wenye thamani ya dolari bilioni 200. Mnamo Januari 2023 washauri wa usalama wa kitaifa wa India na Marekani walitangaza kuzinduliwa kwa Mpango wa Marekani-India katika Teknolojia Muhimu Zinazoibuka (iCET). Ushirikiano huu wa kimkakati wa teknolojia ni dhahiri unahusiana na wasiwasi wa Marekani kuhusu China, ambayo India inaonekana kushiriki pamoja nayo. Lakini inabakia kuonekana endapo India itaunganisha teknolojia zake na zile za Marekani na kuachana kabisa na teknolojia ya China na Urusi.
Modi anapotembelea India, hatimaye Marekani iko mahali ambapo imeimarisha mahusiano na India, baada ya miongo kadhaa ya kuachwa kwenye baridi. Lakini uhusiano huu, licha ya makubaliano yote ya kiuchumi na kijeshi, sio muungano na bado unakabiliwa na shida nyingi. India haiuoni ulimwengu kama Marekani inavyouona. Kwa muda mrefu, kikwazo kikubwa kwa uhusiano wa karibu wa India na Marekani ni kwamba nchi zote mbili zina historia ya kuwa na urafiki na wapinzani wa kila mmoja. India inachukia kuendelea kwa usaidizi wa kimada wa Marekani kwa Pakistan. Pia ina shaka na majaribio ya sasa ya Marekani ya kudhibiti na kushirikiana na China kwa wakati mmoja. Ingawa India ina mzozo wa mpaka na China pia ina mahusiano ya kiuchumi nayo na inataka haya yaendelee. India haiangalii China jinsi Marekani inavyoiangalia. India kwa kweli haiyaoni mambo mengi jinsi Marekani inavyoyaona, lakini inataka kufaidika na uwekezaji, teknolojia na biashara ya Marekani.
Watawala wa India kihistoria hawajawa vibaraka wa Marekani mithili ya watawala wengi wa Waislamu walivyofanya. Wengi wa watawala wa Waislamu ima walijiunga na Marekani kwa manufaa yao binafsi au waliletwa madarakani na Marekani. Wanahalalisha uwepo wa Marekani na kuendeleza umuhimu wake, huku mataifa mengine yakiuona uhalisia wa Marekani na yana shaka kuiunga mkono.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Adnan Khan