Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Musharraf atajibu kwa Uhaini wake katika Mahakama ya Mwenyezi Mungu (swt)

 Je, Watawala wa Sasa Watazingatia?

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 5 Februari 2023, baada ya kuugua kwa muda mrefu, Musharraf aliaga dunia katika hospitali ya kibinafsi jijini Dubai. Jenerali Pervez Musharraf alichukua mamlaka baada ya mapinduzi kwa serikali ya Nawaz Sharif mwaka wa 1999. Utawala wa Jenerali Musharraf unaweza kutajwa kuwa enzi mbaya zaidi ya kujisalimisha kwa Marekani. Jenerali Musharraf ndiye aliyefungua milango ya mafuriko kwa uwepo rasmi wa wanajeshi wa Marekani katika eneo hilo. Musharraf alikisalimisha 'Kina cha kimkakati' cha Pakistan kwa maongezi ya mara moja tu ya simu bila malalamiko yoyote. Zaidi ya hayo, Musharraf alitoa njia za anga, viwanja vya ndege vitano vya kijeshi, laini ya usambazaji ya NATO kwa jeshi la Marekani. Musharraf kisha alilisambaratisha taifa kwa kuanzisha vita dhidi ya ugaidi ndani ya Pakistan ambavyo viliteketeza jeshi la Pakistan na ujasusi na kusababisha mgawanyiko mkubwa kati ya wanajeshi na raia, uliopelekea umwagaji damu wa miaka 20 katika eneo hilo unaoendelea hadi leo.

Mikono ya Musharraf imelowa damu ya mamia ya maelfu ya Waislamu. Musharraf aliwaua wanafunzi wa Jamia Hafsa na Lal Masjid, na kuruhusu jeshi la Marekani kufanya mashambulizi ya droni kwa raia kutoka katika kambi na njia za anga alizozitoa. Kambi maarufu ya mtandao ya Black Water na Raymond Davis iliundwa wakati wa enzi yake ambayo iliongoza kampeni za ulipuaji mabomu kote nchini. Musharraf pia alijigamba kuhusu kuwauza kina kaka na dada wa Kiislamu kwa dolari kwa Marekani, akiwemo Dkt. Aafia Siddiqui ambaye angali anasota katika magereza ya Marekani.

Orodha ya uhalifu wa Musharraf ni ndefu. Aliruhusu jeshi la India kuweka uzio kando ya LoC na aliwakandamiza na kuwapiga marufuku wapiganaji wa upinzani wa Kashmir, na hivyo kuitoa zawadi Kashmir Inayokaliwa Kimabavu kwa India kama matokeo yake. Musharraf aliweka misingi ya sura mpya ya usaliti, ambayo warithi wake wameiongeza na wanaendelea kufanya hivyo. Musharraf alikuwa mtawala wa jeshi lenye uwezo lenye silaha za nyuklia na bado alitumia nguvu hiyo kwa watu wake mwenyewe ili kujisalimisha kupata maslahi ya Marekani. Huu ni ukiukaji wa wazi wa sheria za Mwenyezi Mungu (swt) na tangazo la wazi la khiyana dhidi Yake. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «لِكُلِّ غَادِرٍ لِوَاءٌ يَوْمَ الْقِيَامَةِ يُرْفَعُ لَهُ بِقَدْرِ غَدْرِهِ أَلا وَلَا غادر أعظم مِن أميرِ عامِّةٍ» “Siku ya Kiyama kila msaliti atakuwa na bendera itakayonyanyuliwa kwa ajili yake kwa kadiri ya usaliti wake, basi jueni hakuna msaliti mkubwa kuliko kiongozi watu.” [Muslim]

Tunawausia kwa ikhlasi watawala wa sasa, kabla Mwenyezi Mungu (swt) hajakaza mshiko wake shingoni mwenu, wacheni kuwa kizuizi katika njia ya utabikishaji mfumo ulioteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt) na tubuni kwa ajili ya kujisalimisha kwenu kwa mfumo wa kibepari wa Kimagharibi. Onyo la Mwenyezi Mungu (swt) liko wazi,

[اِنَّ بَطْشَ رَبِّكَ لَشَدِیْدٌ]

“Hakika kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali.” [Surah Al-Buruj 85:12]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Naveed Zafar – Wilayah Pakistan

Fuatilia na Sambaza Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

#HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu