Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Tumechomwa Kisu Mbele Yetu

Mkataba wa amani wa wiki iliopita baina ya dola ya Mayahudi, Bahrain na Imarati ulikuwa ni mchomo ndani ya moyo wa kadhia ya Palestina na ni pigo kwa Ummah wa Kiislamu – ambao kwa kweli unatamka hivi, hamu yetu kuu zaidi ya Ummah ni kana kwamba si halali na isiostahili umoja wa Waarabu na Waislamu.

Katika mikataba iliofanyiwa mnada na Jared Kushner mkwe wa Raisi Trump, Mataifa ya Ghuba yalionyesha kwa furaha muungano mpya na Waziri Mkuu Netanyahu katika eneo la White House la South Lawn. Kwa pamoja wakijinata kuhusu zama mpya za muungano wa Waarabu na umbo la Kiyahudi – ambao unatarajiwa karibuni kuhusisha Oman na Saudia, kabla ya maeneo yenyewe yaliotawanywa ya Palestina.

Muingilio huu wa kidanganyifu wa utawala wa Trump katika masuala ya Waislamu na Ardhi Tukufu ya Al Quds, ni muendelezo wa maono ya muda mrefu ya Amerika katika eneo ambalo imekuwa ikilifanyia kazi kwa miongo kadhaa.

Mwaka 1978 Raisi wa Amerika Jimmy Carter aliweka mkataba wa Camp David. Mkusanyiko wa makubaliano baina ya aliyekuwa Raisi wa Misri Anwar Sadat na Waziri Mkuu aliyepita Menachem Begin.

Ulipewa jina rasmi kuwa ni ‘Mpango kwa ajili ya Mashariki ya Kati’ yakiwa malengo yake matatu ni 1) kuupatia mchakato wa kujitawala Wapalestina katika Gaza na Ukingo wa Magharibi, 2) kukubali ukamilishaji wa mkataba wa amani baina ya Misri na dola ya Kizayuni, na 3) kuutoa tena ‘mpango’ huu pamoja na dola la Kizayuni na majirani wengine.

Mbadala wa kukubali mpango huu, kuimarisha mahusiano ya amani, kuitambua rasmi dola ya Kizayuni, na kuufungua Mkondo wa Suez, umbo la Kiyahudi litajiondoa katika Rasi ya Sinai na kuanzisha biashara ya pande mbili.

Ikiegemea juu ya ‘mpango’ huu, Mikataba ya Oslo ya 1993 na 1995 ilitiwa saini baina ya umbo la Kiyahudi na PLO. Makubaliano hayo mawili yaliupatia mamlaka machache utawala wa Palestina katika Gaza na Ukingo wa Magharibi, ambapo pande zote mbili zilitambuana rasmi kwa matumaini ya kutoa fursa ya kutatua masuala ya mipaka ya dola ya Kizayuni, makaazi yake na hadhi ya Jerusalem.

Mwishowe katika 1994, yakifanyiwa udalali tena na Amerika, Raisi Bill Clinton alishuhudia Mfalme Hussain wa Jordan na Waziri Mkuu Yitzak Rabin wakifanya amani na kusawazisha mahusiano katika mji wa mpaka wa Wadi Araba, kwa kulingana na Mpango kwa ajili ya amani katika Mashariki ya Kati. Na hivyo kupunguza kutengwa kwa umbo la Kiyahudi kulikoikumba tokea ilipoingilia na kuinyakua Palestina mwaka 1948.

Ni wazi kuwa watawala wa Waislamu wanafurahia kushirikiana kwa usaliti na umbo la Kizayuni na vibaraka wake mara kwa mara. Hawatilii maanani orodha ya maovu yenye kuumiza na ya kikatili na kushikilia hadithi za udanganyifu ambazo zinaufanya kuwa ni jinai upinzani wa Wapalestina.

Hata hivyo hisia za Ummah wa Kiislamu ziko tofauti.

Tumekuwa muda wote tukipinga fikra ya kusawazisha mahusiano na Mazayuni, na tumekuwa macho kwa kila dhara na ukatili dhidi ya watu wa Palestina na Ardhi Tukufu. Tokea kuanza kwa dola vamizi, Ummah wa Kiislamu umeshuhudia mauwaji kwa maelfu, utesaji wa kila siku na mauwaji ya kinyama ya wasio na hatia, watu wasio na silaha, wanaume, wanawake na watoto, kufungwa kwa vijana wengi wa Kipalestina kwa wakati mmoja katika miongo kadhaa, hata kwa watoto wa chini ya miaka kumi. Kuibiwa na kuvunjwa kwa majumba, ardhi za kilimo na matunda – mbali na mzingiro, kutolewa viungo na muendelezo wa kupiga mabomu Gaza kwa fosfarasi nyeupe na mabomu ya kutawanyika katika miaka ya karibuni.

Vizazi vya Waislamu vina uelewa, mapenzi na hisia kwa ndugu zao wake kwa waume katika Uislamu. Umoja wao ni mkubwa zaidi ya utii kwa mshikamano wa kitaifa au fungamano la umoja wa Kiarabu. Kama ilivyo ardhi ya Al-Isra na Mi’raj ambapo Mtume wetu mpendwa (saw) aliinuliwa kuelekea mbingu ya saba – Palestina na watu wake wapendwa waliobarikiwa, hawawezi na hawatoweza kuachwa na kutelekezwa!

Kwa hivyo ukataaji wa Ummah kwa wingi wake juu ya wavamizi wasio halali ni jambo linalojulikana na linaendelea kukua. Hii ni wazi kutokana na idadi kubwa ya taasisi na harakati, makala, magazeti na matoleo, mikutano na maandamano, kususia bidhaa za ‘Israeli’ ambayo imeshuhudia harakati ya BSD kukua kwa kasi sana – pamoja na miito ya Jihad na kuirejesha Khilafah ilioahidiwa katika njia ya Utume kushughulikia tatizo hilo.

Tangu kuanza kwa usaliti huu wa karibuni wa Imarati na Bahrain, kundi la kiraia la Imarati lijulikanalo kama ‘Jumuia ya Imarati ya Kupinga Usawazishaji Mahusiano’ imezindua kampeni ya mtandao ya Twitter ikiwa na alama ishara ‘watu dhidi ya usawazishaji mahusiano’, ambayo hadi sasa imepata zaidi ya saini milioni moja na hata kuamuru katiba yao wenyewe inayounga mkono Palestina. Licha ya ukandamizaji wa wanaharakati wake wanaohatarisha kuwa katika kifungo cha hadi miaka kumi kwa makosa yasio wazi yanayohusu usalama wa taifa, idadi kadhaa ya jumuiya kote katika eneo zimetoa uungaji mkono wao kwa juhudi hizo, ikiwemo Chama cha Mawakili wa Palestina, Jumuiya ya Kupinga Usawazishaji Mahusiano ya Bahrain, Uangalizi wa Morocco Dhidi ya Kusawazisha Mahusiano na Jukwaa la Wapalestina nchini Jordan.

Hatua hii, kama zilivyo nyengine, kutaka amani na maadui wa wazi wa Uislamu na Waislamu, ni dhambi kubwa ambayo imewaweka wazi na kuendelea kuwadhalilisha wote wanaounga mkono na kushiriki – inazalisha mzunguko wa matokeo ambayo watawala wa Waislamu wameshindwa moja kwa moja kuyatarajia.

Zingatia mataifa yote ya Waislamu ambayo yalikuwa yamekata tamaa kabisa kuonyesha thamani yao kwa mabeberu wa Kimagharibi wanaofahamu vibaya maendeleo ya kimada ya nchi za Magharibi kuyafanya ni maendeleo matukufu na utulivu wa kijamii ambao Uislamu unaweza kuutoa.   

Licha ya utiifu wao kwa Mabepari walaghai, mataifa haya ya Waislamu yamerudishwa kuwa madogo zaidi ya Makasino, (ambapo nyumba hizo mara zote hushinda) kwa ajili ya mataifa ya Kimagharibi, ambao hutumia kila njia na lengo la chini chini linalowezekana kusomba rasilimali zao, kuweka kodi kwenye bidhaa zinazosafirishwa nje, kuweka kambi za kijeshi katika ardhi zao, idhini ya kulipa huduma hewa ya afya ya kiulimwengu na makongamano ya mabadiliko ya hali ya hewa kana kwamba maoni yao yana uzito wowote, na kwamba kura zao katika Umoja wa Mataifa, hata kwa wao wenyewe licha ya uungaji mkono wa Palestina kuwa ni zenye kupingwa tu.

Haya ndio matokeo ya usaliti wa viongozi wetu – na malipo ya Ummah unaoyalipa kwa umoja wao na mmoja mmoja pia ni kiwango chengine cha dhulma na unyanyasaji.

Licha ya usaliti mkubwa unaoukumba Ummah huu chini ya mikono ya viongozi wao wenyewe, Mwenyezi Mungu (swt) ameahidi kuwa wema na matendo mazuri ya Ummah hayatopotea bure. Mwenyezi Mungu (swt) atawatoa watu Anaowapenda katika Ardhi ya Israa na Mi’raj kulishinda umbo baya la Kiyahudi na kuling'oa moja kwa moja.

Mwenyezi Mungu (swt) anasema katika Quran,

 ﴾يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ مَن يَرْتَدَّ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَسَوْفَ يَأْتِي اللّهُ بِقَوْمٍ يُحِبُّهُمْ وَيُحِبُّونَهُ أَذِلَّةٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ أَعِزَّةٍ عَلَى الْكَافِرِينَ يُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللّهِ وَلاَ يَخَافُونَ لَوْمَةَ لآئِمٍ ذَلِكَ فَضْلُ اللّهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاء وَاللّهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ﴿

“Enyi mlioamini! Atakaeiacha miongoni mwenu Dini yake, basi Mwenyezi Mungu atakuja leta watu anaowapenda nao wanampenda, wanyenyekevu kwa waumini na wenye nguvu kwa makafiri, wanapigania Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawaogopi lawama ya anaelaumu. Hiyo ndio fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakae. Na Mwenyezi Mungu ni Mkunjufu na Mwenye kujua.” [Surah Al Maidah: 54].

Chama kiaminifu kinachofanya kazi kukamilisha ahadi hii ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na bishara njema za Mtume Wake (saw), itakuwa ni harakati isiodanganya watu wake. Kwa uoni na utambuzi, itauongoza Ummah kwenye wema ambao utauhuisha kwa utukufu na ushindi katika maisha haya na Yajayo.

Mwenyezi Mungu (swt) anasema katika Quran,

إِنْ أَحْسَنتُمْ أَحْسَنتُمْ لِأَنفُسِكُمْ وَإِنْ أَسَأْتُمْ فَلَهَا فَإِذَا جَاء وَعْدُ الآخِرَةِ لِيَسُوؤُواْ وُجُوهَكُمْ وَلِيَدْخُلُواْ الْمَسْجِدَ كَمَا دَخَلُوهُ أَوَّلَ مَرَّةٍ وَلِيُتَبِّرُواْ مَا عَلَوْاْ تَتْبِيرًا﴿

 “Basi mkifanya wema mnajifanyia wema nafsi zenu. Na mkifanya ubaya, mnajifanyia wenyewe. Na ikifika ahadi ya mwisho ili waziharibu nyuso zenu, na waingie Msikitini kama walivyoingia mara ya kwanza, na waharibu kila walichokiteka kwa uharibifu mkubwa.” [Surah Al Isra’: 7].

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb Ut Tahrir na
Maleeha Hasan

 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu