Jumanne, 21 Rajab 1446 | 2025/01/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  13 Shawwal 1444 Na: 1444 / 11
M.  Jumatano, 03 Mei 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Hizb ut Tahrir / Uzbekistan Yahitimisha Kampeni “Hapana kwa Katiba iliyo na Mapungufu ya Mwanadamu! Ndiyo, kwa Katiba inayotokana na Qur’an na Sunnah”
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir / Uzbekistan ilihitimisha kampeni yake chini ya kauli mbiu: "Hapana kwa katiba iliyo na mapungufu ya mwanadamu! Ndiyo kwa katiba inayotokana na Qur’an na Sunnah,” ambayo iliandaliwa wakati wa kura ya maoni ya katiba mpya ya Uzbekistan iliyoandaliwa mnamo tarehe 30 Aprili. Kwa rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu kampeni hii ambayo kimsingi iliandaliwa katika mitandao ya kijamii ilifanikiwa, kwani iliweka wazi kupitia makala, video na machapisho mafupi kuwa Waislamu wa nchi yetu kamwe wasikubali kuipitisha katiba hii ya Kikafiri ya kidemokrasia kwa sababu ni kinyume kabisa na Uislamu na hukmu zake. Pia yaliyoangaziwa ni ukweli kwamba kura hii ya maoni ni usanii wa kuongeza muda wa Rais Shavkat Mirziyoyev.

Kampeni hii ilipingwa na mmoja wa "Wanachuoni!" ambaye hakuweza kudiriki ukweli huu na siku zote anahalalisha sera ya chuki dhidi ya Uislamu inayofuatwa na utawala wa Uzbekistan. Alidai kuwa kampeni hii iliyoandaliwa na hizb inaeneza fitna miongoni mwa Waislamu wa nchi yetu! Yeye ni miongoni mwa wale wanaobeba jukumu kubwa sana, kama wanazuoni, la kuwaongoza Waislamu, lakini aliifuata njia ya khiyana na kujidhalilisha nafsi yake kwa kuizulia uongo hizb hii inayoshikamana na njia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Yeye alifanya hata jinai mbaya zaidi kwa kudai kuwa Maswahaba walikuwa wanademokrasia, ili kuhalalisha sera za serikali hii! Hizb ilimtaka amche Mwenyezi Mungu, aache kusaliti haki za Waislamu, na aachane na biashara duni ya kuiuza dunia hii na Akhera kwa dunia ya watawala hawa wasaliti.

Na twamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwamba Khilafah Rashida itangazwe kwa njia ya Utume, ambayo itaurudisha Umma wa Kiislamu katika fahari, utukufu, na nguvu katika siku za usoni. Na twamuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu kuihifadhi na kuinusuru hizb hii inayofanya kazi usiku na mchana kwa ajili ya kusimamisha Khilafah.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum 4-5]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu