Afisi ya Habari
Uzbekistan
H. 11 Sha'aban 1444 | Na: 1444 / 08 |
M. Ijumaa, 03 Machi 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ziara ya Blinken nchini Uzbekistan
(Imetafsiriwa)
Februari 28, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Anthony Blinken alishiriki katika mkutano wa kilele wa C5 + 1 wa wakuu wa idara za sera za kigeni wa nchi za Asia ya Kati - Marekani jijini Astana. Kisha, siku hiyo hiyo, alifika Tashkent kwa ziara rasmi. Mnamo Machi 1, Rais Shavkat Mirziyoyev alipokea ujumbe ulioongozwa na Blinken. Kama ilivyotarajiwa, mada kuu ya ziara ya afisa huyo mkuu wa Marekani ilikuwa kutoa wito kwa nchi za Asia ya Kati kuchukua tahadhari na kujiepusha na sera ya uchokozi ya Urusi. Kuhusiana na hilo, pia alisisitiza kwa nguvu kwamba Marekani iko tayari kuzisaidia nchi za eneo hilo kwa kutumia uwezo wote unaowezekana. Hasa, Blinken alisema katika mkutano wa C5 + 1 kwamba watu wa eneo la Asia ya Kati wameteseka zaidi kutokana na vikwazo vya Marekani dhidi ya Urusi kuliko nchi nyengine na kwamba Marekani itafidia hasara hizi. Siku hiyo hiyo, ilitangazwa katika taarifa iliyoandikwa kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani kwamba dolari milioni 25 zitatengwa kwa ajili ya programu za kikanda ndani ya mfumo wa Mpango wa Uthabiti wa Kiuchumi wa Asia ya Kati. Aidha amesema vita vya uvamizi vya Urusi dhidi ya Ukraine vinatia wasiwasi nchi za eneo hilo, na hakuna hakikisho kwamba Urusi haitaanzisha uchokozi dhidi yake hapo kesho.
Kuhusiana na ziara ya Blinken nchini Uzbekistan, alisisitiza kwanza na tena kwamba Marekani imedhamiria daima kuunga mkono uhuru, ubwana wa kujitawala na uadilifu wa eneo la Uzbekistan. Alidokeza kuwa Uzbekistan, kama nchi za eneo hilo, inateseka kutokana na uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine, na kusema kuwa dolari milioni 16 zimetengwa kama msaada (wa dharura) kwa ajili ya chakula. Pia alieleza fikra zake kuhusu kuimarisha machapisho ya ndani dhidi ya propaganda za Kirusi nchini Uzbekistan. Wakati wa mkutano wake na Mirziyoyev, Blinken aliwasilisha salamu na maombi mema ya Biden. Alisisitiza kuwa mageuzi ya kidemokrasia nchini Uzbekistan yalipata kasi katika zama za utawala wa Mirziyoyev na kwamba Marekani inakaribisha hilo. Blinken pia alitoa wito wa kutopendelea upande wowote na uwazi katika uchunguzi wa ghasia zilizotokea katika mji wa Nukus huko Karakalpakstan mnamo Julai 1 na 2 mwaka jana, na kujadili utabikishaji kamili wa mageuzi katika majali ya uhuru wa kidini na haki za binadamu.
Ni wazi kuwa Marekani inaamini kuwa wakati umewadia wa kufanya kile ambacho imekuwa ikitamani kila wakati, ambacho ni kutumia kushughulishwa kwa Urusi na Ukraine kupanua wigo wake wa ushawishi katika Asia ya Kati, haswa Uzbekistan. Ndio maana, mwanzoni mwa vita vya Urusi na Ukraine, mahusiano ya Magharibi, haswa Marekani, na Uzbekistan yalikola kasi. Ziara ya Blinken ni mojawapo ya hatua ambazo Marekani imepiga kuelekea lengo lake, na inajaribu kuiondoa Uzbekistan kutoka kwa ushawishi wa kisiasa na kiuchumi wa Urusi kadri inavyowezekana kupitia miradi ya kiuchumi na kielimu.
Tunatoa wito kwa Waislamu wa nchi yetu kuwa makini na hatua hizi za Marekani, kwa sababu nyuma ya "malengo yake matukufu" kuna maslahi yake pekee. Inaituhumu Urusi kwa uchokozi dhidi ya Ukraine na kupiga kelele kwa ulimwengu mzima na kupiga kelele zisizo na maana juu ya ubwana na uadilifu wa eneo. Marekani ndiyo iliyo angamiza ubwana wa nchi za Kiislamu hasa pale ilipoivamia Iraq na Afghanistan kinyume na kanuni na sheria za kimataifa ilizozitabanni. Popote ilipokuwa, haikuacha chochote ila ufukara, njaa, uharibifu, muozo, na uchafu wa maadili. Demokrasia mbaya ilitabanniwa kama silaha ya kuwafanya watu kuwa watumwa na kunyakua mali zao. Ikiwa ni hivyo, mnawezaje kuamini anachokisema mwakilishi wake rasmi?!
Suluhisho la kweli sio Marekani, Urusi, China au Ulaya, bali ni Uislamu pekee. Uislamu ndio njia pekee ya kutuokoa na dola hizi ovu za kikoloni. Njia hii ni njia iliyonyooka inayopelekea kwenye kusimamisha Khilafah.
Enyi Waislamu wa Uzbekistan: Wasaidieni wale wanaofanya kazi ya kusimamisha Khilafah kama Mola wenu Mlezi anavyofaradhisha, kwani katika hilo ndiyo furaha ya dunia na Akhera. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ)
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal 8:24].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uzbekistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Uzbekistan |
Address & Website Tel: |