Jumatano, 02 Rabi' al-thani 1447 | 2025/09/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uholanzi

H.  30 Rabi' I 1447 Na: 02 / 1447
M.  Jumatatu, 22 Septemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Suluhisho la Dola Mbili: Njia ya Uhai kwa “Israel”, Sio kwa Palestina

(Imetafsiriwa)

Dola nyingi zaidi za Magharibi zinawasilisha wito wa suluhisho la dola mbili kama hatua ya kimaadili na ya haki. Lakini wale wanaotazama nyuma ya pazia wanaona kuwa halina uhusiano wowote na huruma kwa Wapalestina au utambuzi wa “haki yao ya uhuru”. Kinyume chake: ni hatua ya dharura ya kisiasa, inayoendeshwa na shinikizo kutoka kwa watu wao wenyewe na hasara inayokuja ya uhalali wa umbile la Kizayuni.

Rai jumla ya umma katika nchi za Magharibi inabadilika. Watu zaidi na zaidi wanakabiliwa na ukweli: uharibifu wa kiserikali wa Gaza, mauaji ya kijamii, na mauaji ya halaiki ambayo yanaweza kufuatiliwa moja kwa moja kwenye skrini zao. Serikali ambazo kwa miongo kadhaa zimeilinda “Israel” bila mashiko sasa zinahisi shinikizo kutoka kwa maeneo bunge yao. Sio kwa sababu ghafla wamekuuza sikitiko kwa masaibu ya Wapalestina, lakini kwa sababu haipigiki debe tena kusimama bila masharti upande wa “Israel”.

Kwa kuongeza, dola za Magharibi zinazidi kufahamu kuhusu udhaifu wao wenyewe wa kisheria na kimaadili. Mahakama ya Kimataifa ya Haki inazungumzia mauaji ya halaiki, mashirika ya haki za binadamu yanakusanya ripoti zao, na ushiriki wa serikali za Magharibi unazidi kuonekana zaidi. Sio tu ushiriki wa kivitendo, lakini pia wa kimya, kupitia usambazaji unaoendelea wa silaha, pazia la kidiplomasia, na uhalali wa kisiasa.

Hii haimaanishi kwa vyovyote vile kwamba utiifu wa milele kwa “Israel” unatelekezwa. Kinyume chake. Maandamano hayo yanaelekezwa tu kwa Netanyahu na njia yake ya sasa, kwa sababu ni njia hiyo ndiyo inaiweka “Israel” yenyewe hatarini. Kwa maana ikiwa “Israel” itaendelea kwa njia hii, pamoja na vita vya kudumu na uharibifu, kuungwa mkono uwepo wa “dola ya Kiyahudi” utapungua, katika kanda hiyo pamoja na kimataifa. Ni kwa sababu hii haswa kwamba suluhisho la dola mbili kwa mara nyingine tena linafufuliwa: sio kama uokozi kwa Palestina, bali kama ulinzi kwa mustakabali wa “Israel”.

Katika maono ya Magharibi, dola kama hiyo ya Palestina lazima bila shaka itimize masharti yao: kuondolewa kikamilifu nguvu za kijeshi, chini ya usimamizi wa “Israel”, na kuwiana na desturi na maadili ya Kimagharibi. Dola isiyo na ubwana wa kweli, iliyo kikamilifu chini ya mradi wa kikoloni ambao “Israel” inauwakilisha tangu 1948. Kwa maana nyengine: “dola” ambayo haimalizi uvamizi na udhibiti, bali inauimarisha.

Hata ikiwa dola mbili zingeanzishwa, ni nini kingetokea kwa mateso yote ambayo “Israel” imesababisha kwa muda zaidi ya miaka 77 iliyopita? Kwa uharibifu wa Gaza, mauaji ya halaiki, mauaji ya kijamii, na ardhi zilizoporwa? Hakuna chochote kabisa. Kama vile ambavyo makampuni ya kikoloni ya Kimagharibi katika ulimwengu wa Kiislamu hayajawahi kukabiliwa na matokeo ya jinai zao za ukandamizaji, uporaji na uharibifu.

Ndio maana ni muhimu kwamba Waislamu wasijibu kwa hamasa masuluhisho haya batili, bali kwa maono ambayo Uislamu unawapatia. Palestina si faili ya kibinadamu inayosubiri wema wa Magharibi. Ni suala la Kiislamu, na utatuzi haupo katika huruma za dola za kisekula, kikoloni, kibepari, unyonyaji damu, bali katika ukombozi wa Palestina na Waislamu wenyewe. Hapo pekee ndipo haki itatendeka kwa wahasiriwa, na ndipo mradi wa kikoloni ndani ya moyo wa ulimwengu wa Kiislamu utafikia mwisho.

Suluhisho la dola mbili linaweza kuonekana kama hatua kuelekea “amani”, lakini kiuhalisia, ni jaribio la kuiokoa “Israel” kutokana na kuanguka kwake na kuiepusha Magharibi kutokana na mzigo wa kushirikiana nayo.

Okay Pala
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir
Uholanzi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uholanzi
Address & Website
Tel:  0031 (0) 611860521
www.hizb-ut-tahrir.nl
Fax:  0031 (0) 611860521
E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu