Jumamosi, 11 Shawwal 1445 | 2024/04/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Uholanzi

H.  17 Rajab 1444 Na: 10 / 1444
M.  Jumatano, 08 Februari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Katuni ya Kuchukiza kutoka kwenye Gazeti la Kejeli la Ufaransa Inaonyesha Kuporomoka kwa Maadili na Chuki za Magharibi kwa Waislamu

(Imetafsiriwa)

Haitoshi kwa gazeti la kejeli la Ufaransa, Charlie Hebdo, kutukana nembo za Uislamu. Wanakejeli hata mateso wanayopitia Waislamu kupitia kutengeneza katuni kuyahusu. Nchini Uturuki na Syria, matetemeko ya ardhi kadhaa makubwa yametokea. Idadi ya vifo imeongezeka hadi zaidi ya 6,000 na idadi ya waliojeruhiwa ni makumi kwa maelfu. Charlie Hebdo wanatumia haki yao ya uhuru wa kujieleza kudhihaki mateso ya ndugu na dada zetu katika hali hii.

"Kejeli" ambayo Charlie Hebdo inaficha nyuma ni dhihirisho la chuki yao dhidi ya Uislamu na Waislamu. Kumekuwa na matukio kadhaa ambapo kipenzi chetu Mtume Muhammad (saw) ametukanwa au ambapo Uislamu umedhihakiwa. Mnamo 2007, katuni za Denmark za Mtume (saw) zilichapishwa. Mwaka 2015 na 2020, walifanya hivyo hivyo tena kwa kumtukana Mtume (saw) kwa njia ya vibonzo. Hii ni dalili ya wazi ya chuki iliyojengeka ndani ya nyoyo za watu hawa wapotovu.

Sasa gazeti hilo la kejeli kwa mara nyengine tena limetumia "haki yake ya uhuru wa kujieleza," lakini safari hii kuwakejeli watu walio katika hali mbaya. Mchoro huo wa kuchukiza unaonyesha jinsi nchi za Magharibi zisivyojali hali ya kutisha na ya kusikitisha ambayo kaka na dada zetu wa Syria na Uturuki wamo ndani yake. Mfumo unaoruhusu vitendo kama hivyo umefilisika kifikra. Ni mfumo potovu.

Katika katuni, majengo yaliyoanguka yalionyeshwa na maandishi: "Huna haja hata ya kutuma vifaru." Kwa maana nyengine, uharibifu wa nchi za Kiislamu unapaswa kufanyika kwa kupenda au kutopenda. Waislamu lazima daima wateseke. Na inaafikiana tu na waundaji wa katuni kwamba hakuna vifaru/gharama itapaswa kutumwa huko.

Yale yaitwayo mabango ya usawa, uhuru, na udugu yanakanyaga maiti kihalisi. Wanafurahia mateso katika ulimwengu wa Kiislamu, wanawatakia Waislamu kutokana na chuki ya kimfumo, na hata kudhihaki waziwazi mateso ya maelfu ya watu. Ni lazima tutambue chuki hii ya kimuundo dhidi ya Uislamu, nembo zake, na wafuasi wake. Ni lazima tutambue mapambano ya kimfumo yanayofanyika. Ni lazima tutambue kwamba tunapaswa kuchagua upande. Kama Waislamu, tunaweza kuchagua upande mmoja pekee, ule wa kujisalimisha kwa Mwenyezi Mungu (swt).

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Uholanzi

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uholanzi
Address & Website
Tel:  0031 (0) 611860521
www.hizb-ut-tahrir.nl
Fax:  0031 (0) 611860521
E-Mail: okay.pala@hizb-ut-tahrir.nl

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu