Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia

H.  10 Dhu al-Qi'dah 1443 Na: 1443/26
M.  Alhamisi, 09 Juni 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kuwaandama Mahakimu ni Natija Isiyoepukika ya Mifumo Iliyotungwa na Mwanadamu na Hukmu ya Matamanio
(Imetafsiriwa)

Rais Kais Saied aliwafuta kazi majaji 57 kupitia agizo la rais kwa tuhma za "ufisadi, kula njama, na kuzima kesi za washukiwa wa ugaidi." Sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia tunafafanua yafuatayo:

1. Jambo hili ni sehemu ya jitihada za Rais Kais Saied kutaka kudhibiti idara ya mahakama ili kuwamaliza wapinzani wake wa kisiasa, baada ya kushindwa kuajiri Baraza Kuu la Mahakama licha ya kubadilishwa kwa baraza jipya mnamo tarehe 12/2/2022.

2. Amri na amri za rais zinathibitisha upuuzi wa kisheria chini ya tawala zilizobuniwa na mwanadamu zinazotumikia tu matakwa ya mtawala dhalimu au kikundi cha wapiga debe, wataalamu wa kisiasa na mabwana zao kutoka ng’ambo.

3. Majaji leo wanapigana vita vya kihistoria dhidi ya majaribio ya kutapatapa dhidi ya kumilikiwa idara ya mahakama na junta tawala. Vita vyao sio juu ya mkate na malipo ya kila mwezi kama inavyoonyeshwa na vyombo vya habari vilivyo nyuma, lakini ni vita hatari vya kuhifadhi kile kilichosalia cha mafanikio ya mapinduzi na kuzuia kurudi kwa idara ya mahakama katika kutoa maagizo. Wanawakilisha ngome za mwisho za uimara na upinzani, na leo wanakabiliwa na haki ya kihistoria: ima wavumilie ili kudhamini haki za watu na kufikia malengo ya mapinduzi, au wasalimu amri kwa dhulma na wachangie katika kuregesha dola ya kipolisi zaidi kuliko ilivyokuwa katika zama za Ben Ali, ambayo sisi wala watu wa Tunisia, au vizazi vijavyo haturidhiki nayo.

Sisi katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia tunawaambia majaji kwa barua hii ya wazi ya tarehe 8 Dhul Qa’adah 1443 H sawia na 7 Juni 2022 M. Tunaweka mikononi mwao msimamo wa kisiasa na wa vyombo vya habari kuhusiana na kuhakikisha uwepo wa idara ya mahakama isiyokuwa na ufisadi na ubaguzi, inayohifadhi haki za watu na yenye msimamo thabiti katika kuwahesabu watawala, ili watu wetu nchini Tunisia, haswa mahakimu, wanazuoni, watu wa fiqh na sheria, waone utukufu na uadilifu wa sheria ya Kiislamu ili kuitekeleza na kuitabikisha kivitendo.

Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[إِنَّ اللهَ يَأْمُرُكُمْ أَن تُؤَدُّوا الْأَمَانَاتِ إِلَى أَهْلِهَا وَإِذَا حَكَمْتُم بَيْنَ النَّاسِ أَنْ تَحْكُمُواْ بِالْعَدْلِ إِنَّ اللهَ نِعِمَّا يَعِظُكُم بِهِ إِنَّ اللهَ كَانَ سَمِيعاً بَصِيراً]

“Hakika Mwenyezi Mungu anakuamrisheni mzirudishe amana kwa wenyewe. Na mnapo hukumu baina ya watu mhukumu kwa uadilifu. Hakika haya anayo kuwaidhini Mwenyezi Mungu ni mazuri sana. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kusikia, Mwenye kuona.” [An-Nisaa: 58].

 Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
Address & Website
Tel: 71345949 / 21430700
http://www.ht-tunisia.info/ar/
Fax: 71345950
E-Mail: tunis@htmedia.info

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu