Afisi ya Habari
Wilayah Tunisia
H. 22 Dhu al-Qi'dah 1443 | Na: 1443/28 |
M. Jumanne, 21 Juni 2022 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kongamano la Kila Mwaka la Khilafah la Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia 2022
(Imetafsiriwa)
Katika kumbukumbu chungu ya miaka 101 ya kuvunjwa kwa Khilafah, na kwa kuzidishwa kwa juhudi za kuisimamisha tena, ili Waislamu waweze kufurahia kilele cha izza chini yake, na kurudisha fahari yao iliyopotea, hadhi iliyodhalilishwa na uongozi kwa ajili ya wanadamu. Hizb ut Tahrir inafanya kongamano lake la kila mwaka katika Wilayah ya Tunisia chini ya kichwa:
“Ruwaza ya Kiuchumi ya Hizb ut Tahrir”
Kundi la wasomi, wanamaoni na wataalamu kutoka nchi mbalimbali watashiriki, na kupitia kwalo watatoa masuluhisho ya kimsingi ya kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi unaotishia nguvu za watu na umbile la dola. Kupitia kwayo, Hizb itathibitisha kwamba Dola ya Khilafah inayoifanyia kazi kuisimamisha ni dola ya usimamizi na ustawi inayowahakikishia maisha ya staha wale wanaoishi chini yake na kutoa mahitaji ya kimsingi ya watu binafsi kama vile makaazi, chakula na mavazi, na mahitaji ya kimsingi ya wananchi kuanzia afya, usalama na elimu, jambo ambalo ni kinyume kabisa na dola ya ukusanyaji ushuru, inayochipuza kutokana na itikadi ya kutenganisha dini na dola, iliyowafanya watu wengi nchini Tunisia kuteseka na umaskini, maradhi, ukosefu wa ajira na utunzaji duni.
Kongamano hilo litakuwa katika sehemu tatu, ambapo uwasilishaji wa ruwaza ya kiuchumi ya Hizb ut Tahrir utawasilishwa kama ifuatavyo:
Sehemu ya Kwanza:
1. Mgogoro wa kiuchumi ulimwenguni na bei za juu
2. Sababu jumla na maalum za mgogoro wa kiuchumi nchini Tunisia
3. Athari za mgogoro wa kiuchumi nchini Tunisia
Sehemu ya Pili:
1. Tatizo la kiuchumi
2. Sera ya Uchumi katika Uislamu
3. Uislamu ulitatua vipi umasikini?
4. Maendeleo ya kiuchumi: kuendeleza kwa nchi kiviwanda, kuamsha sera ya kilimo katika Uislamu, na kuchochea biashara
Sehemu ya Tatu:
1. Utajiri na uwezo mkubwa uliopo nchini Tunisia
2. Uwekaji bajeti na kufadhili miradi ya kifedha yenye mapato kwa msingi wa utoshelevu wa kiviwanda na kilimo
3. Suluhisho la Uislamu kwa ukosevu wa ajira
4. Mtazamo wa Uislamu juu ya sarafu na suluhisho la kizungumkuti cha kuanguka kwa thamani ya sarafu
Kongamano hili litafanyika, Mwenyezi Mungu akipenda, mnamo siku ya Jumamosi, tarehe 26 Dhul Qa'adah 1443 H sawia na 25 Juni 2022 M, saa 10:00 asubuhi kwenye ukumbi ulioko ndani ya makao makuu, makutano ya Soukra-Ariana, katika mji mkuu wa Tunis, na litapeperushwa moja kwa moja kwenye chaneli ya Al-Waqiyah TV, Mwenyezi Mungu akipenda.
Sisi, katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia, tunayo furaha kuwaalika Waislamu kwa jumla, na wanahabari, wanasiasa na wataalamu haswa, nchini Tunisia na nchi nyenginezo za Waislamu, kushiriki katika kongamano hili, na kufanya maingiliano nalo na kulitangaza katika vyombo vya habari.
Twamuomba Mwenyezi Mungu (swt) alijaalie kongamano hili liwe ni utambuzi na uongofu kwa walimwengu. Mwenyezi Mungu (swt) asema:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal: 24].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Tunisia |
Address & Website Tel: 71345949 / 21430700 http://www.ht-tunisia.info/ar/ |
Fax: 71345950 E-Mail: tunis@htmedia.info |