Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 14 Sha'aban 1446 | Na: HTS 1446 / 49 |
M. Alhamisi, 13 Februari 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wanasiasa wa Sudan Wanatekeleza Njama za Amerika Kuichana Nchi!
(Imetafsiriwa)
Mnamo Alhamisi, 13 Februari 2025, Al-Sharq iliripoti kwamba Osama Saeed, kiongozi wa Chama cha Mapinduzi, alisema: “Kundi letu linapanga kutangaza serikali kufikia mwisho wa Februari.” Alikuwa anakusudia serikali sambamba na ile iliyopo Port Sudan kwa sasa. Alifafanua zaidi: “Ngazi za utawala katika serikali ya kiraia ndani ya maeneo yanayodhibitiwa na Vikosi vya Msaada wa Haraka (RSF) zitajumuisha rais wa Baraza Kuu, wajumbe, na Baraza la Mawaziri.”
Msisitizo wa baadhi ya wanasiasa—ambao hapo awali walikuwa sehemu ya muungano wa Taqaddum—kuanzisha serikali sambamba na utawala wa Al-Burhan mjini Port Sudan, hasa katika maeneo yanayodhibitiwa na RSF, unakuja wakati ambapo jeshi linasonga mbele na kuyalinda maeneo makubwa ya Al-Jazeera, Khartoum, na kwengineko. Wakati huo huo, vikosi vya RSF vinaelekea Darfur, ngome yao, ambapo tayari wanadhibiti sehemu nne kwa tano za eneo hilo, huku Darfur Kaskazini pekee ikisalia nje ya udhibiti wao. Ni katika maeneo haya kwamba Osama Saeed na wanasiasa wengine wanaonekana kuwa na nia ya kuanzisha serikali, na kuifanya Darfur mgombea mkuu wa kujitenga – kama vile Sudan Kusini ilivyofanya. Hii inaendana na mpango wa muda mrefu wa kikoloni.
Na cha kusikitisha ni kwamba, haya yanatendeka mikononi mwa wana haswa wa nchi hii yenye taabu—wanasiasa wabinafsi ambao ni vibaraka wa wakoloni makafiri wa Magharibi. Wanatekeleza mradi wa Bernard Lewis, mwanahistoria wa Kiyahudi wa Marekani anayejulikana kama "muuaji wa Mashariki ya Kati," ambaye alipigia debe mgawanyiko zaidi na kugawanywa kwa ardhi za Kiislamu kwa misingi ya kikabila, madhehebu, na kikanda. Katika kikao cha siri mwaka 1983, Bunge la Congress la Marekani lilipitisha ruwaza ya Bernard Lewis, ambapo Marekani inataka kuigawanya Sudan katika dola tano tofauti, kama Rais wa zamani Omar al-Bashir alivyotaja katika mojawapo ya mahojiano yake na vyombo vya habari.
Kupitia Al-Bashir na wanasiasa wengine, Amerika ilifanikiwa kuitenganisha Sudan Kusini kupitia Mkataba muovu wa Naivasha. Sasa, ni inajitahidi kuitenganisha Darfur kupitia kwa wanasiasa ambao wamemsaliti Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na waumini—wanaouza dini yao kwa ajili ya manufaa ya kidunia ya wengine!
Sisi katika Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan hapo awali tulionya dhidi ya kutenganishwa kwa Sudan Kusini na tukawasihi watu wa Sudan kufahamu njama za wakoloni makafiri za kuichana nchi yetu. Sasa, tunafichua mpango wa kuitenganisha Darfur kabla haujatokea. Tunatoa wito kwa watu wenye ikhlasi wa nchi hii kutong’atwa mara mbili kutoka kwenye tundu moja. Tunawataka wasimame kidete dhidi ya njama za dola za kikoloni za Magharibi, hususan Marekani, na kuwazuia wanasiasa hao ambao wamejitia katika mikono ya ubeberu na wanatekeleza njama zake dhidi ya ardhi yetu.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرًّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal:24].
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |