Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  1 Muharram 1446 Na: HTS 1446 / 01
M.  Jumapili, 07 Julai 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kongamano la Cairo Larudisha tena Utawala ule ule Uliosababisha Migogoro na Kuichana Nchi
(Imetafsiriwa)

Jana, Jumamosi, tarehe 6 Julai 2024, lile linaloitwa Kongamano la Kisiasa na Majeshi ya Kiraia ya Sudan lilifanyika katika mji mkuu wa Misri, Cairo; nukta muhimu katika taarifa ya mwisho zilizotolewa zilikuwa: “...wanakongamano pia walisisitiza ulazima wa kushikamana na Azimio la Jeddah na kuzingatia taratibu za utekelezaji na maendeleo yake ili kuendana na maendeleo katika vita… Ama kuhusu njia ya kisiasa kutatua mgogoro huo, washiriki walikubaliana juu ya kuhifadhi Sudan kama nchi moja kwa misingi ya uraia, haki sawa, na serikali ya kiraia, kidemokrasia, kifederali…”

Kwa kuzingatia yale yaliyotajwa katika taarifa ya mwisho ya Kongamano la Cairo, sisi katika Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan tunathibitisha yafuatayo:

Kwanza: Wanasiasa walio mstari wa mbele katika matukio nchini Sudan bado wanafuata njia zao potofu za zamani, wanashangilia na kusherehekea masuluhisho ya mkoloni kafiri. Hawaoni suluhisho la machafuko ya Sudan, yaliyoundwa na mikono ya maadui, isipokuwa katika njama za maadui wenyewe, kwa hivyo methali isemayo, “Niponye kwa ugonjwa wenyewe!” inatumika kwao.

Pili: Kongamano hilo linarudisha utawala ule ule uliosababisha migogoro na kuichana nchi, hii ni kupitia kujadili serikali ya kiraia, kidemokrasia na ya kifederali. Ni serikali ile ile aliyoiunda kafiri mkoloni Muingereza nchini Sudan, kisha akawakabidhi wale aliowaundia kwa makusudi, hivyo wakafuata upotofu wake mpaka tukaifikia baada ya takriban miongo saba uhalisia huu mchungu.

Tatu: Wahudhuriaji wa kongamano hilo wamethibitisha kuwa wao ni sehemu ya sera ya Marekani ya kujaza ombwe hadi mapishi yake yenye sumu yatakapoiva na kuwapeleka Jeddah. Washiriki wa kongamano hilo hawana ruwaza ya kisiasa iliyo wazi zaidi ya kuregelea masuluhisho ambayo mkoloni kafiri Magharibi anawapatia kwa manufaa yao na dhidi ya maslahi ya watu wa Sudan.

Nne: Hatukuona katika kongamano hilo zaidi ya nyuso zinazohusishwa na mkoloni kafiri ambaye anamakinisha ukoloni na kutumikia miradi yake.

Kwa kumalizia: Tunawaambia watu wetu wa Sudan kwamba nyinyi ni Waislamu mnaomuamini Mwenyezi Mungu kuwa ni Mola wenu Mlezi, Uislamu ni Dini yenu, na Muhammad (saw) kuwa ni Nabii na Mtume wenu, basi vipi mnakubali kuwa mtu anayehusishwa na

maadui zenu makafiri, wasiokutakieni kheri, afanye kazi kutatua masuala yenu? Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[مَّا يَوَدُّ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ وَلَا الْمُشْرِكِينَ أَن يُنَزَّلَ عَلَيْكُم مِّنْ خَيْرٍ مِّن رَّبِّكُمْ]

“Walio kufuru miongoni mwa watu wa Kitabu na washirikina hawapendi mteremshiwe kheri yoyote kutoka kwa Mola wenu Mlezi.” [Al-Baqara: 105].

Mwisho: Tunasisitiza kwamba hakuna suluhisho la migogoro ya Sudan na dunia nzima isipokuwa katika mfumo wa Uislamu na Shariah yake iliyonyooka inayotabikishwa na dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo wakati umewadia, Mwenyezi Mungu akipenda, na ambayo ni bishara njema ya kipenzi mteule (saw):

«ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ. ثُمَّ سَكَتَ»

“Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume, kisha akanyamaza.” [Imam Ahmad ameisimulia katika Musnad yake].

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu