Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 9 Dhu al-Hijjah 1445 | Na: HTS 1445 / 49 |
M. Jumamosi, 15 Juni 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mauti katika Mipaka ya Sykes-Picot Yatakomeshwa tu na Khilafah Pekee
(Imetafsiriwa)
“Jeshi la Misri lashambulia magari ya wasafirishaji haramu yanayobeba Wasudan,” hiki kilikuwa kichwa cha habari kwenye tovuti ya ‘Sudan Tribune’ mnamo Ijumaa, Juni 14, 2024, ambapo liliripoti mkasa wa Wasudan wanaokimbia vita wanaojaribu kuingia Misri. Habari hizo zilisema, “Walinzi wa mpaka wa Misri walipiga risasi magurudumu ya magari yaliyokuwa yakiendeshwa na wasafirishaji haramu yalipokuwa yanajaribu kuingia Misri...” Vyombo vya habari vya Sudan na Misri viliripoti kwamba vyombo vya usalama vya Misri vilikamata mabasi 7 yaliyokuwa yamepakia wakimbizi wa Sudan katika muda wa siku mbili zilizopita... Shirika la Habari la Sudan limesema kuwa hali mbaya ya hewa ilisababisha vifo vya makumi ya watu... na kwamba Balozi wa Sudan huko Aswan, Abdul Qadir Abdullah, alitoa rambirambi zake kwa watu wa Sudan na familia za marehemu.
Wale ambao mamlaka za Misri zinawaita wakimbizi wanaokuja Misri kinyume cha sheria, na mamlaka za Sudan zinakubaliana nao, hawajafanya uhalifu ili kupokea unyanyasaji huu na hawajakiuka hukmu ya kisheria kwani Misri ni nchi yao, kama Sudan. Wanapaswa kupokelewa kwa mikono miwili baada ya kuhamishwa na vita vya kutengenezwa. Kiasili, ni kwamba hakuna mipaka kati ya Misri na Sudan, ambazo zilikuwa ni nchi moja kabla ya Waingereza na vibaraka wao kutenganisha Sudan na Misri kwa jina la madai ya uhuru, na kisha wakarudia mandhari hiyo hiyo ya kuitenganisha Sudan ya Kusini na ile ya kaskazini. Ni sera ya kafiri adui mkoloni, kugawanya na kutawala, ambayo bado anaitumia kusambaratisha sehemu zilizosambaratika za nchi za Kiislamu na kuzichana zile zilizogawanyika.
Maafa ya watu wa Sudan hayatakwisha, na hata maafa ya Umma wa Kiislamu, ambao unaathiriwa na vitendo vya watawala wake katika vijidola vidogo vya uharibifu vilivyoundwa na wakoloni na wao, yaani, watawala, kutekeleza kazi hiyo hiyo, ambayo inasambaratisha nchi, kuwahamisha watu, kuhifadhi mazizi ya Sykes-Picot, na kuugeuza udugu wa Kiislamu kuwa udugu wa ardhi na nchi! Matendo haya hayatakoma na mauti kwenye mpaka wa Sykes-Picot hayatakoma isipokuwa kwa kusimamishwa Khilafah, ambayo itaondoa mipaka ya nchi za Kiislamu, hivyo abiria atasafiri kutoka Jakarta hadi Tangier na kutoka Tripoli Ash-Sham hadi Khartoum, akipitia miji yote ya nchi za Kiislamu bila visa au pasi ya kusafiria.
Basi njooni, enyi watu wa Sudan, na kwa hakika, enyi Waislamu, nyote mufanyeni kazi pamoja na watu wenye ikhlasi wanaotaka kuregesha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, kwani ndiyo ambayo ndani yake umo wokovu wenu, na utukufu wenu, na radhi za Mola wenu Mlezi.
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Al-Anfal 8:24]
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |