Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  6 Jumada II 1442 Na: HTS 1442 / 44
M.  Jumanne, 19 Januari 2021

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mapigano ya Kikabila Huko Darfur kwa Kukosekana Dola ya Uchungaji; Khilafah kwa njia ya Utume – Imepelekea na Ingali Inapelekea Umwagikaji wa Damu

(Imetafsiriwa)

Siku ya Jumatatu, 1/18/2021, Kamati ya Madaktari wa Darfur Magharibi ilitangaza kuwa wahasiriwa wa mji wa El Geneina wameongezeka hadi wafu 129 na majeruhi 198 katika mzozo ulioibuka kati ya Waarabu wahamaji na mapote ya kabila katika eneo hilo. Huko Darfur Kusini, mzozo wa wenyewe kwa wenyewe ulitokea kati ya makabila mawili, ambayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 20, katika wilaya ya Al-Tawil, ambayo ni kilomita 65 kutoka mji wa Nyala; mji mkuu wa Jimbo la Darfur Kusini.

Hii sio mara ya kwanza kwa matukio haya mabaya kuzuka, ambayo yangali yanaendelea kutokea huko Darfur, magharibi na kusini. Mnamo Januari mwaka jana, matukio mithili ya haya yalizuka huko El Geneina, na kuua zaidi ya watu 54, kujeruhi 60, na makumi ya maelfu kuachwa bila ya makao.

Ilikuwa ni kushindwa kwa serikali zote ambazo zilifanikiwa kutawala Sudan katika kumaliza mapigano kwa misingi ya kikabila, ikiwa sio baadhi ya serikali hizi kuwa ndio sababu kuu ya kuzuka kwa vita hivi, kwa sababu ya ubaguzi wa kisiasa kwa misingi ya kikabila, na tuna hakika kuwa serikali hii ni mithili ya mtangulizi wake, haitaweza kuondoa mizozo hii kwa sababu ni serikali ambayo haujengwa juu ya msingi wa kujali mambo ya watu. Badala yake, ni serikali kibaraka ambayo dhamira yake ni kutekeleza sera za Magharibi mkoloni kafiri katika nchi yetu, hata ikiwa ni kwa gharama ya riziki na usalama wa watu.

Hakika Uislamu umeharamisha damu ya Waislamu, Mwenyezi Mungu (swt) asema:

]وَمَنْ يَقْتُلْ مُؤْمِناً مُتَعَمِّداً فَجَزَاؤُهُ جَهَنَّمُ خَالِداً فِيهَا وَغَضِبَ اللَّهُ عَلَيْهِ وَلَعَنَهُ وَأَعَدَّ لَهُ عَذَاباً عَظِيماً]

Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannamu humo atadumu, na Mwenyezi Mungu amemkasirikia, na amemlaani, na amemuandalia adhabu kubwa.” [An-Nisaa: 93] Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«لاَ تَرْجِعُوا بَعْدِي كُفَّاراً، يَضْرِبُ بَعْضُكُمْ رِقَابَ بَعْضٍ»

Musirudi baada yangu mukawa makafiri, mukakatana shingo wenyewe kwa wenyewe.”

Yule ambaye husitisha mizozo hii mara moja, na kuyayeyusha makabila haya ndani ya kinu kimoja, ni Uislamu mtukufu pekee, alifanya hivyo mwanzoni mwa utawala wake, wakati makabila katika Bara Arabu yalipokuwa yakipigania sababu zisizo za maana, kwa hivyo aliwafanya kuwa Ummah mmoja ambao hakuna tofauti kati ya Mwarabu na asiyekuwa Mwarabu, wala kati ya mweusi na mweupe isipokuwa kwa uchaji Mungu. Watu hawakurudi katika Jahiliyya kupigana kwa misingi ya kikabila isipokuwa wakati dola ya Kiislamu ilipovunjwa; Khilafah, na mahali pake kusimam vijidola hivi bandia dhaifu, vibaraka ambavyo kwa muumini haviheshimu udugu wala dhima.

Hakika Hizb ut-Tahrir, ambayo inataka kuunganisha Ummah na kuuingiza katika kinu cha Uislamu, kuhakikisha ndugu waumini wanapendana chini ya kivuli cha Dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa ya njia ya Utume, na ambayo pekee ndiyo inayoweza kumaliza mizozo hii, kupitia kuondoa mizizi ya matatizo kwa msingi wa hukmu za Uislamu ambazo huiwajibisha dola kuchunga mambo ya Ummah, miongoni mwa uchungaji huu ni kutoa usalama na amani kwa raia wote, pamoja na kutoa maisha bora ambayo hayawezekani isipokuwa kwa kuafikiana na njia ya Mwenyezi Mungu (swt) ambaye amesema:

]وَلَوْ أَنَّ أَهْلَ الْقُرَى آمَنُوا وَاتَّقَوْا لَفَتَحْنَا عَلَيْهِمْ بَرَكَاتٍ مِنَ السَّمَاءِ وَالْأَرْضِ وَلَكِنْ كَذَّبُوا فَأَخَذْنَاهُمْ بِمَا كَانُوا يَكْسِبُونَ]

Na lau kuwa watu wa miji wangeli amini na wakamchamngu, kwa yakini tungeli wafungulia baraka kutoka mbinguni na katika ardhi. Lakini walikanusha basi tukawapatiliza kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyachuma.” [Al-A'raaf: 96]

Ibrahim Uthman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu