Alhamisi, 03 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  19 Jumada I 1446 Na: 1446 / 17
M.  Alhamisi, 21 Novemba 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Gaza ni Kadhia ya Umma na Majeshi yake, Sio Vibaraka wa Kamandi Kuu ya Kijeshi ya Marekani (US CENTCOM)

(Imetafsiriwa)

Mnamo tarehe 15 Novemba 2024, Mkuu wa Majeshi aliregelea mauaji ya Gaza, akisisitiza kwamba Pakistan haitakuwa sehemu ya “mzozo wowote wa ulimwengu.” Gaza ni kadhia ya Ummah na majeshi yake, sio vibaraka wa US CENTCOM. Mkuu wa Majeshi alipewa amri za kina kuhusu Gaza wakati wa ziara yake nchini Marekani mnamo Disemba 2023, ambazo zinafuatiliwa mara kwa mara. Kwa kutii amri za Waamerika, Jenerali Asim Munir anazuia vikosi vya jeshi shujaa na vyenye uwezo vya Pakistan kuhamasishwa kuinusuru Gaza, licha ya shinikizo linaloongezeka kutoka kwa Umma na vikosi vyake vya jeshi.

Enyi Waislamu wa Pakistan na Majeshi yao! Uongozi wa kijeshi umetangaza kuwa hautashiriki katika mizozo ya kimataifa. Kwa hiyo, ni kwa msingi gani unatetea suluhisho la Marekani la dola mbili, ambalo linasalimisha sehemu kubwa ya Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina kwa umbile la Kiyahudi? Je, ni kwa msingi gani uongozi wa kijeshi ulipeleka meli za wanamaji za Pakistan ili kulinda vifaa kwa ajili ya umbile la Kiyahudi, kutokana na mashambulizi ya mujahidina wa Yemen?

Ikiwa uongozi wa kijeshi haushiriki katika mzozo wa kimataifa, basi kwa nini kuna vikwazo ambavyo havijatangazwa vilivyowekwa katika upandishaji wa bendera kuunga mkono Gaza nchini Pakistan? Kwa nini, basi, wenye mamlaka wanawafunga Waislamu wanaoandamana kuwapendelea wanyonge wa Gaza? Kwa nini mamlaka huharibu kambi zao za maandamano na kufungua kesi za kimahakama dhidi yao? Kwa kweli, uongozi wa kijeshi unashiriki katika mzozo huu wa kimataifa, lakini kwa upande wa umbile la Kiyahudi, Amerika na makruseda wa zama hizi. Ndani ya nchi, uongozi wa kijeshi unawaogopa Waislamu na vikosi vyao vya kijeshi, na hivyo unavunja jaribio lolote la kuwahisabu Kishariah watawala.

Enyi Wanajeshi wa Pakistan! Uongozi wa kijeshi umekataa waziwazi kuwalinda Waislamu, Al-Masjid Al-Aqsa na Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina. Sasa, hamuwezi kudai kwamba munasubiri amri kutoka kwa uongozi wa kijeshi kwa sababu amri hizo hazitakuja kamwe. Kwa hivyo, ni njia gani nyingine muliyobakisha ya kutekeleza faradhi ya Kishariah ya kuwanusuru wanyonge, zaidi ya kuuondoa uongozi wa kijeshi ambao ni kikwazo katika njia yenu? Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[وَمَا لَكُمْ لَا تُقَـٰتِلُونَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱلْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ ٱلرِّجَالِ وَٱلنِّسَآءِ وَٱلْوِلْدَٰنِ ٱلَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَآ أَخْرِجْنَا مِنْ هَـٰذِهِ ٱلْقَرْيَةِ ٱلظَّالِمِ أَهْلُهَا وَٱجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ وَلِيًّۭا وَٱجْعَل لَّنَا مِن لَّدُنكَ نَصِيرًا]

“Na mna nini msipigane katika Njia ya Mwenyezi Mungu na ya wale wanao onewa, wanaume na wanawake na watoto, ambao husema: Mola Mlezi wetu! Tutoe katika mji huu ambao watu wake ni madhaalimu, na tujaalie tuwe na mlinzi anaye toka kwako, na tujaalie tuwe na wa kutunusuru anaye toka kwako.” [Surah an-Nisa 4:75].

Hizb ut Tahrir imekuwa ikikuiteni tangu siku ya kwanza ya vita vya dunia dhidi ya Gaza. Kwa kila mwezi unaopita, imekuwa wazi kwenu kwamba uongozi wa kijeshi ni kibaraka wa Amerika. Basi jitokezeni na mtoe Nusrah yenu kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Khilafah ndio mradi pekee wa kisiasa wa Kiislamu ndani ya Ummah ambao kupitia kwao hali hii yote inaweza kugeuzwa. Dawah na Jihad zitaanza tena baada ya Nusrah yenu. Kisha, Khalifa wenu Rashid (Khalifa muongofu) atakuongozeni katika Jihad katika Njia ya Mwenyezi Mungu (swt), na ataung'oa utawala na ushawishi wa Marekani duniani.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu