Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 7 Safar 1443 | Na: 1443 / 09 |
M. Jumanne, 14 Septemba 2021 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Sera ya Vyombo vya Habari ya Khilafah Pekee Ndio Inayohakikisha Uwajibikaji Huku Vyombo vya Habari Vikiwa ni Ala Yenye Nguvu ya Kubeba Ukweli wa Uislamu Ulimwenguni
(Imetafsiriwa)
Wanahabari, vyombo vya habari, mawakili, vyama vya upinzani na mashirika ya kutetea haki za binadamu ya Pakistan wanapambana na Mswada wa Maendeleo ya Vyombo vya Habari wa Pakistan, wakiulaani kama jaribio la kuvinyonga vyombo vya habari. Kwa upande mwingine, serikali inadai haja ya kuzuia habari bandia na kutoa haki kwa wafanyikazi wa vyombo vya habari. Huku wakiwa na huruma chache kwa upinzani, Waislamu pia wanaona kuwa serikali inanyonga kila aina ya uwajibikaji, ikiwemo utekaji nyara wa hivi karibuni wa wanaharakati sita wa Hizb ut Tahrir kutoka Karachi, kwa sababu tu ya kufichua msimamo unaoegemea upande wa Amerika wa serikali kwa Afghanistan.
Vile vile, serikali huwateka nyara waandishi wa habari, ikiwashinikiza kueneza hadithi ya serikali. Ummah inaona kuwa sehemu kubwa ya vyombo vya habari vimekuwa chombo cha ukoloni, katika kuhudumia serikali au dola za kigeni, vikipotosha Ummah kupitia hadithi huria, zenye kupinga Uislamu. Kwa hivyo, vyombo vikuu vya habari vimepoteza uaminifu, huku Ummah ukielekea kwa vyombo vya habari visivyo vya kawaida, kama mtazamaji asiyevutiwa na mgogoro ulioko sasa.
Vyombo vya habari ni tawi la kudumu la serikali katika dola ya Khilafah, huku vyombo vya habari mahiri vya kibinafsi vitashajiishwa. Vyombo vya habari ni sehemu isiyoweza kutenganishwa ya sera ya dola ya kuutawalisha mfumo wa Kiislamu kote ulimwenguni. Hakuna leseni inayohitajika kwa aina yoyote ya chombo cha habari, ikiwa inatosha tu kwake kuifahamisha dola kubuniwa kwake pekee. Kila chombo cha habari kinawajibika kwa habari zake zilizochapishwa au zilizoripotiwa, kuhisabiwa mbele ya mfumo huru wa mahakama ya Kiislamu ikiwa kutakiukwa sera ya vyombo vya habari. Msingi wa uwajibikaji wa dola ni sera ya Kiislamu ya kuamrisha mema na kukataza maovu, sio uhuru wa kujieleza, kutoka kwa ustaarabu wa kiliberali wa Magharibi. Hakuna chombo chochote cha habari kitakachopewa idhini kuanzisha uhusiano huru na serikali au taasisi za kigeni.
Vyombo vya habari haviwezi kutoa vyenzo zisizo za Kiislamu wala kuhujumu msingi wa dola, kwani Waislamu wote na waandishi wa habari wana haki ya kikatiba ya kuwawajibisha watawala na maafisa wa serikali kwa msingi wa Uislamu, kama vile Mwarabu mmoja Mbedui alivyomuuliza Umar (ra) kuhusu shuka mbili alizokuwa anazimiliki, au mwanamke mmoja kumlazimisha Umar (ra) kubadilisha amri yake juu ya mahari. Kila chombo cha habari kinawajibika kwa habari zake zilizochapishwa au zilizoripotiwa, chenye kuhesabiwa mbele ya mfumo huru wa mahakama ya Kiislamu.
Katika demokrasia na udikteta, sheria ni kwa kufuata matakwa ya wanadamu, badala ya kuvuliwa kutoka kwa Quran na Sunnah. Kwa hivyo watawala wanazuia vyombo vya habari ili kulinda maslahi ya kibinafsi na ya wakoloni, huku baadhi ya vyombo vya habari vyenye nguvu vikifanya vivyo hivyo. Vyombo vya habari vya Khilafah ndivyo vitakavyofanya kazi chini ya sera isiyoweza kubadilishwa ya Shariah ya Kiislamu, ambayo haiwezi kuharibiwa na Khaleefah wala Baraza la Ummah. Vyombo vya habari hivyo vitazindua kampeni ya kiulimwengu dhidi ya dola za kirasilimali, vikifichua sera zao angamivu za kikoloni na itikadi na mifumo batili, vikiandaa uwanja wa ufunguzi wa Uislamu wa ardhi zao. Baada ya kuzipata nyoyo na akili za watu wao kwa uadilifu wa Uislamu, jeshi litatumwa kuwaondoa watawala wanaobakia kama kizingiti. Na ni vyombo vya habari kama hivyo vya Kiislamu ambavyo vitamhisabu mtawala awajibike, bila kumuogopa yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu (swt), kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt). Hivi vitakuwa ni vyombo vya habari vinavyoweka mifano katika ushujaa, ukweli na unyofu.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: https://bit.ly/3hNz70q |