Jumamosi, 21 Muharram 1446 | 2024/07/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  22 Dhu al-Qi'dah 1445 Na: 1445/27
M.  Alhamisi, 30 Mei 2024

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mumewaachia Nini Wananchi Baada ya Mkate?!

Dumisheni Usaidizi wenu na Muregeshe Haki za Watu
(Imetafsiriwa)

Dkt. Mostafa Madbouly, Waziri Mkuu, alitangaza ongezeko la bei ya mkate iliyofadhiliwa kutoka piaster 5 hadi piaster 20 kuanzia Juni ijayo. Madbouly aliongeza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo kwamba gharama ya mkate kwa serikali inafikia piasters 125, lakini iliuzwa kwa piaster 5 pekee, hivyo serikali ina gharama ya ruzuku ya pauni bilioni 120. (Masrawy, 29/5/2024)

Hakuna kilichosalia isipokuwa mkate tu ambao kwao utawala unachapa migongo ya watu! Suala siyo tu ufisadi wa serikali, utepetevu wa kiidara, na kushindwa katika uongozi, bali ni dhamira ya makusudi ya kuwaweka njaa na kuwabana wananchi, ili kuendelea kuufukuzia mkate wao wa kila siku bila kuupata. Kufikiwa lengo hili ndiko kunakoifanya serikali, kwa mtazamo wake, kuwa salama na hasira za wananchi, wanaotamani kuzamisha meno yao katika fikra za utawala huu na nembo zake, hususan kwa kuzidisha faili za ufisadi, usaliti, kufeli na uzembe wa utawala huo kwa maslahi na matukufu ya watu wote. Suala la Gaza sio pekee ambalo limepandisha joto la watu hadi kiwango cha kuchemka, karibu kuwafanya walipuke mbele ya utawala huu. Ni suala la elfu moja linalothibitisha ulazima na kutoepukika kwa kuondoka utawala huu na kupinduliwa kwake.

Mkate ndio kimbilio la mwisho la watu maskini baada ya sera za utawala huu kuwafanya kuwa maskini zaidi. Utawala haukuishia katika kuongeza bei za umeme, gesi na mafuta mengine, ambazo kwa kawaida husababisha kuongezeka kwa bei kutokana na mfumko wa bei na chini ya ushawishi wa kushuka kwa thamani. Sasa mkono wa utawala umefika kwenye chakula cha maskini, wasiopata chochote isipokuwa mkate!

Utawala hautoi ruzuku kwa mkate au kitu chengine chochote. Badala yake, watu ndio wanaoisaidia serikali kwa ushuru unaokusanywa kwa nguvu, ambao unazidi 85% ya bajeti ya serikali. Utawala huu unapuuza ardhi na utajiri wa nchi, na kuzipa nchi za Magharibi bure. Makampuni ya mafuta na gesi, mikataba ya uchimbaji madini yenye vifungu vya siri ambavyo hakuna mtu anayeweza kuvipata au kuvipinga, zinashuhudia uzembe huu wa makusudi, na kubebesha Misri na wananchi wake gharama ya uzembe huu, mpaka kuwawajibisha kuwalinda waporaji na kuwawezesha kukamata bidhaa zilizoibwa bila usumbufu wowote.

Wananchi wa Misri hawahitaji usaidizi wa utawala huu unaojivunia na ambao hauna thamani wala manufaa yoyote baada ya mawimbi ya mfumko wa bei uliowatafuna. Badala yake, wanataka haki zao, ambazo zinaminywa. Utawala uregeshe haki hizi kwa wananchi na ubaki wenyewe na usaidizi wake, na uache kuchukua pesa za wananchi kwa njia ya kodi, ambazo zimekuwa ndio chanzo kikuu cha mapato ya utawala huu, ambazo kwazo unapata usaidizi unaojivunia kwa wananchi.

Je, ziko wapi haki za watu za gesi, mafuta, dhahabu na rasilimali nyingine nyingi zinazotosha kwa Wamisri wote kuishi kwa ustawi ikiwa rasilimali hizi hazingeporwa na zingegawanywa kwa haki? Misri, kwa kweli, na ndani ya mipaka ya Mkataba wa Sykes-Picot, ina mali na rasilimali za kutosha kuifanya iwe huru kutoka kwa Magharibi, mikopo yake, na uwekezaji wake. Uwezo huu unaweza kuifanya Misri kuwa na nguvu kubwa, kama si nchi inayoongoza, kama ingekuwa na khiyari na usimamizi wa dhati wa kutumia rasilimali hizi ipasavyo. Misri ina mashamba makubwa ya kilimo ambayo hayatumiki na yangeweza kulimwa ili kuzalisha ngano badala ya kuiagiza kutoka nje ya nchi, pamoja na mazao mengine mengi ili kukidhi mahitaji ya watu. Zaidi ya hayo, kuna maeneo mingi ya maji yanazofaa kwa uvuvi, yanayofunika zaidi ya feddans milioni 11, yenye kutoa faida kwa sekta zinazohusiana. Kutumia rasilimali hizi za ardhi na maji pia kungeajiri vijana wasio na kazi, ambao serikali inawaona kama mzigo wa idadi ya watu wanaotumia juhudi zao za maendeleo, wakati ni serikali ndiyo inayopoteza nguvu hizi! Aidha, kwa mujibu wa takwimu za Baraza la Mawaziri, uzalishaji wa kila siku wa mafuta na gesi nchini Misri ni mapipa milioni 1.73, na uzalishaji wake wa dhahabu kwa mwaka ni takriban tani 15.8, nyingi zikitoka kwenye Mgodi wa Sukari katika Jangwa la Mashariki. Misri ina takriban maeneo 270 ya dhahabu, yakiwemo maeneo na migodi 120 ambapo kihistoria dhahabu ilichimbwa, huku Mgodi wa Sukari ukiwa ndio mkubwa na maarufu zaidi nchini Misri. (Al Arabiya).

Misri ina aina ya kipekee ya rasilimali, pamoja na nguvukazi yenye uwezo wa kuzalisha mali kutokana na rasilimali hizi. Kinachohitaji Misri ni mfumo wa usimamizi unaolenga kuwajali wananchi, si kuwanyang'anya pesa zao, kuhifadhi haki zao, na kuwawezesha kunufaika na rasilimali hizo badala ya kuzifuja na kuziwezesha nchi za Magharibi kuzipora. Hili haliwezekani chini ya mfumo wa kibepari ambao serikali inatawala nao. Misri inahitaji mfumo ambao lengo lake ni kuwajali wananchi na kudhamini haki zao, wenye sheria zinazohakikisha hili na kuwawajibisha watawala kwa uzembe wowote ule. Hili linapatikana tu katika Uislamu na mfumo wake, pamoja na Shariah zake zinazomfunga mtawala na mtawaliwa, zinazodhamini haki za watu na kuzuia mkono wowote kuzifikia. Hutoa utunzaji bora zaidi bila kuwabebesha watu mzigo wa kodi au kuwahadaa kwa usaidizi wa juujuu tu, kuwapa haki zao wanazostahiki bila kutarajia shukran kwa sababu haki hizi zimeamrishwa na Shariah, ambayo inawajibisha serikali kuwapa. Suluhisho pekee kwa Misri ni Uislamu, mfumo wake, Dola yake na Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Enyi Wanajeshi wa Kinana, Askari Bora: Kinachowapata watu wa Misri kinawaathiri nyinyi pia, na hamna kinga dhidi yake. Ruzuku na marupurupu ya serikali ni hongo tu ili kukunyamazisheni juu ya uhalifu wake, na kukufanyeni kuwa fimbo nzito ya kuwapiga wale wanaoasi maamuzi yake mabaya na umaskini wao unaosababishwa nayo. Fadhila hizi, vyeo na mishahara havitakunufaisheni, si duniani wala Akhera. Kinachokunufaisheni ni kuwa upande wa watu wanaodhulumiwa wa Misri ambao, kama sio kwa riziki zao zilizoandikwa, wangekufa njaa chini ya maamuzi na sera za serikali hii. Simameni pamoja na watu wenu wanaokandamizwa na utawala, munusuru udhaifu wao, ondoeni dhulma ya utawala shingoni mwenu, na mtangaze hasira ya haki kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ili kuing’oa na kuregesha utukufu wa Misri chini ya Uislamu na Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Surat Al-Anfal:24]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu