Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  7 Jumada II 1445 Na: 1445/14
M.  Jumatano, 20 Disemba 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Utawala wa Haki, Ustawi wa Kiuchumi, na Ukombozi wa Al-Quds kutokana na Kunajisiwa na Mayahudi ndio Sababu za Kushinda Uchaguzi
(Imetafsiriwa)

Mamlaka ya Kitaifa ya Uchaguzi, inayoongozwa na Mshauri Hazem Badawi, ilitangaza uchaguzi wa Rais Abdel Fattah el-Sisi kama Rais wa Jamhuri kwa muhula mpya wa urais, kufuatia kutangazwa rasmi kwa matokeo ya uchaguzi wa rais jana, Jumatatu. (Al-Youm Al-Sabea). Na Rais huyo wa Misri alishinda muhula wa tatu wa urais kwa muda wa miaka sita, akipata kura milioni 39.7, ambayo ni 89.6% ya jumla ya kura zote. Alishindana pamoja na wagombea wengine watatu: Hazem Omar, ambaye alipata nafasi ya pili kwa 4.5% ya kura, akifuatiwa na Farid Zahrani katika nafasi ya tatu, akipata 4% ya kura. Katika nafasi ya mwisho alikuwa Abdel Sattar Yumama kwa asilimia ya 1.9%. (BBC Kiarabu)

Hivi ndivyo uchaguzi hufanyika chini ya urasilimali, ambapo wapiga kura wanashawishiwa, na rai ya jumla hutengenezwa, haswa katika nchi yetu ambapo hakuna mfumo au sheria isipokuwa sheria ya msituni. Katikati ya demokrasia ambayo imethibitisha kufeli kwake, waundaji wake na watetezi sasa wanatafuta njia mbadala baada ya kukabiliwa na mapungufu ya kutokuwa na uwezo wa kufikia haki au kupata masuluhisho yoyote.

Asilimia iliyotangazwa na idadi ya kura huzidishwa kwa kiwango kisichoweza kuelezeka! Utawala haufurahii kukubaliwa kokote miongoni mwa watu, na kila mtu aliyeshiriki katika upigaji kura alifanya hivyo chini ya kulazimishwa. Ima kutongozwa na rushwa za uchaguzi au kutishiwa na tishio la kutupwa nje ya kazi zao na nyumba zao. Hii haimaanishi kwamba walipiga kura kwa kumpenda rais wa serikali, ambaye Wamisri wote wanamchukia ulimwenguni na kumlaani mchana na usiku.

Asilimia hii iliyotangazwa isingeweza kupatikana hata na Omar Ibn al-Khattab, Mwenyezi Mungu awe radhi naye, lau angegombea urais, licha ya kuwa ni Khalifa mwadilifu anayejulikana kwa uadilifu wake. Wala na Omar Ibn Abdulaziz, ambaye aliwaambia watu, "Yeyote aliye na deni, na aje kwetu, na yeyote anayetaka kuoa, na aje kwetu kwa ajili ya ndoa." Alitekeleza umalizaji madeni na uwezeshaji ndoa chini ya uangalizi wa dola. Hata pia na Salah al-Din, Qutuz, au Mabaybar ...

Haya yote, utapata miongoni mwa watu, ambao baadhi yao hawajaridhika na hatma yao au wanakataa kuikomboa Al-Quds, wakiwazingatia kuwa watu ovyo kwa kuitupa nchi kwenye moto wa vita.

Asilimia hii ya kinajimu imetoka wapi?! Wakati idadi ya wale waliopiga kura zao katika uchaguzi ilifikia wapiga kura 44,777,668, na kiwango cha ushiriki cha asilimia 66.8, kutoka jumla ya idadi iliyosajiliwa katika orodha ya wapiga kura, ambayo ni karibu milioni 67 kwa walio na zaidi ya umri wa miaka 18, kutoka idadi jumla ya watu milioni 104. Ambapo inamaanisha kulingana na madai yao kwamba mtu mmoja au zaidi kutoka kwa kila familia alishiriki? Hii haiwezekani kutokea, haswa kwa kuzingatia mgogoro wa kiuchumi unaoisibu nchi, unaosababishwa na serikali. Pamoja na matukio katika Ardhi Iliyobarikiwa na ukandamizaji wa Mayahudi na mauaji yao, ambayo ilifanya watu nchini Misri kusahau kuhusu uchaguzi, bila shaka ni mojawapo ya misumari ya mwisho kugongwa kwenye jeneza la demokrasia. Ni wakati wa ufisadi katika kila kitu, wakiwemo wale ambao ni wafisadi. Hawaoni aibu katika kusema uongo, kughushi, na kudanganya!

Tunafahamu vyema kuwa uchaguzi haujawahi na kamwe hautawahi kuwa njia ya mabadiliko, haswa chini ya utawala wa urasilimali. Tunafahamu kuwa ni udanganyifu ulioandaliwa na mfumo na Magharibi kuwasilisha kwa watu machaguo ambayo yote ni uchungu, na kuwalazimisha kuchagua kutokana na machaguo ambayo hayafai na hayatawafaa. Kwa njia hii, mzozo unabaki tu umefungika kwa kiongozi wa serikali badala ya kushughulikia serikali yenyewe. Mfumo unadumisha nguvu yake, ukibadilisha kichwa chake ili kuzimua hasira za watu na kudhibiti uasi wowote.

Udanganyifu umefichuliwa, na Ummah haudanganywi tena na wadanganyifu. Unatazamia mabadiliko ya kweli ambayo yataung’oa ubepari na matawi yake yote, zikiwemo ala zake, nembo, sera, kanuni, na matarajio. Mahali pake, mfumo mpya utokao kwa Mwenyezi Mungu wenye uwezo wa kushughulikia matatizo ya watu, sambamba na maumbile yao, na unaochipuzo kutokana na aqida (itikadi) yao unahitajika. Unapaswa kuwa mfumo ambao unatawala watu kwa uadilifu wa Mwenyezi Mungu, wenye kuwahakikishia haki zao kama ilivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu. Mfumo huu unapaswa kuondoa tofauti kati ya watawala na raia, wachungaji na kundi lao, bila mapendeleo na kwa uadilifu kamili, chini ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume.

Sisi, katika Hizb ut Tahrir, tunakuiteni, Enyi watu wa Kinana, kama taifa na kama jeshi. Tunakuhimizeni muikumbatie na kuifanyia kazi, pamoja na wanaharakati, muinusuru kwa ushindi wa dhati na wa kujitolea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Ili isimamishe hukmu za Uislamu ndani yake. Labda Mwenyezi Mungu ataamuru kupitia nyinyi, kwa ajili yenu, na pamoja na nyinyi. Kwa hakika, ni maisha yenu ambayo lazima muishi na Akhera yenu ambayo munaitarajia. Kuweni wachangiaji na wafuasi wake wachangamfu. Mwenyezi Mungu afungue kupitia nyinyi, akupeni ushindi mkubwa.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا لِلَّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal:24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu