Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  26 Dhu al-Hijjah 1444 Na: 1444/19
M.  Alhamisi, 15 Juni 2023

 

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Sheikh Mkuu wa Al-Azhar atambua Uwepo wa Umbile la Kiyahudi na Ayaondolea Majeshi ya Waislamu Wajibu wa Kuikomboa Bayt al-Maqdis na Viunga vyake
(Imetafsiriwa)

Sheikh wa Al-Azhar ametoa wito Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa kuharakisha kuitambua dola huru ya Palestina ambayo mji mkuu wake ni Al-Quds. Aidha amesisitiza haja ya kuulinda Msikiti wa Al-Aqsa dhidi ya ukiukaji wa kila siku unaoukabili. Wakati wa hotuba yake mnamo siku ya Jumatano tarehe 14/6/2023 mbele ya Baraza la Usalama, Sheikh Al-Tayeb alisema “Nilizungumza kuhusu matukufu ya Palestina, matukufu yangu na yenu. Ninaelezea wasiwasi wangu juu ya ushupavu wa madaraka, ukatili wa udhalimu, na ukimya wa jamii ya kimataifa kuhusu haki za watu wa Palestina." (Dunya Al-Watan)

Ardhi ya Palestina ni ardhi ya Kharaj inayomilikiwa na Ummah mzima, hakuna hata shubiri moja yake inayoweza kuachiliwa. Ni wajibu wa Ummah mzima kuilinda na kuikomboa kutokana na wavamizi wake, na wajibu huu unaangukia nchi zote jirani, huku Misri ikiwa mstari wa mbele. Miito ya Sheikh wa Al-Azhar kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na jamii ya kimataifa ni sawa na kutambua uwepo wa umbile la Kiyahudi na kuyaondolea majeshi ya Umma wa Kiislamu wajibu wao wa kuikomboa ardhi ya Uislamu na matukufu yake. Taasisi za kikoloni za Kimagharibi ndizo zilizoliunda umbile la Kiyahudi kama jambia lenye sumu ndani ya moyo wa Ummah, na kuzuia umoja wake kwa mara nyingine tena. Wao ndio watetezi na walinzi wake wakuu, wanaolilinda dhidi ya hasira ya moja kwa moja ya Ummah kupitia tawala za vibaraka katika ardhi zetu, huku utawala wa Misri ukiongoza katika kucheza dori yake ya khiyana kwa ukamilifu.

Misri, pamoja na watu na jeshi lake, inatamani ukombozi wa Palestina, ambayo wanaichukulia kama kitovu na kadhia kuu. Imekita mizizi katika hisia zao za Kiislamu, udugu, kushikamana na Aqiydah yake na ari yao ya kulinda matukufu na utakatifu wake, pamoja na kumwagwa damu ya Waislamu. Ukombozi wa Palestina ni wajibu kwa majeshi ya Umma mzima wa Kiislamu, na hasa kwa jeshi la Misri, likiwa mojawapo ya majeshi yenye nguvu zaidi na kijiografia karibu na Palestina. Tuna hakika kwamba kuna watu wengi wanyoofu ndani ya jeshi la Misri wanaotamani kwa hamu ukombozi huu, wakijua kikamilifu kwamba ni wajibu wao kwa Umma, Dini na ndugu zao. Kikwazo pekee kilichosimama katika njia yao ni utawala wa sasa. Hivyo basi, ukombozi wa Palestina unalazimu kuung'oa utawala huu kutoka katika mizizi yake na kusimamishwa dola ya Kiislamu inayohamasisha majeshi ili kukomboa sio tu Palestina bali pia ardhi nyingine za Waislamu zinazokaliwa kwa mabavu.

Enyi Wanyoofu katika Jeshi la Kinanah: Kuikomboa Palestina na watu wake waliodhulumiwa ni wajibu wenu, nanyi mtahisabiwa kwa hilo mbele ya Mwenyezi Mungu Siku ya Kiyama. Utawala huu unaokuzuieni kutimiza wajibu huu hauna mamlaka juu yenu; kwa hakika, ni haramu na unapora mamlaka ya Ummah, unatutawala kwa ukafiri. Kung'oa mizizi ya utawala huu ni hatua ya kwanza ya lazima kuelekea njia ya ukombozi wa Palestina. Kwa hiyo, jukumu lenu msingi ni kuung’oa kutoka katika mizizi yake, pamoja na zana na nembo zake zote, na kuukabidhi utawala kwa wanyoofu miongoni mwa Ummah wenye uwezo wa kuutabikisha Uislamu kwa ukamilifu wake, na kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Khilafah hii itahamasisha majeshi kukomboa ardhi zote za Uislamu, sio Palestina pekee. Ewe Mwenyezi Mungu, harakisha kusimamishwa kwake na utuhesabu sisi miongoni mwa askari na mashahidi wake.

[وَالَّذِينَ آمَنُواْ وَهَاجَرُواْ وَجَاهَدُواْ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالَّذِينَ آوَواْ وَّنَصَرُواْ أُولَئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقّاً لَّهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْق كَرِيمٌ]

“Na walio amini wakahama na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio toa mahala pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli. Watapata msamaha wa Mwenyezi Mungu na kuruzukiwa kwema.” [Al-Anfal: 74]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 
http://hizb.net/
E-Mail:  info@hizb.net

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu