Jumapili, 22 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Misri

H.  11 Shawwal 1444 Na: 1444/14
M.  Jumatatu, 01 Mei 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Utawala wa Misri Hauna Uhalali na Mazungumzo yake ni Ujanja wa Kuwahadaa Watu Waliodhulumiwa
(Imetafsiriwa)

Mazungumzo ya kitaifa ambayo utawala wa Misri unadai si chochote bali ni ujanja ambao ulilazimishwa na hali mbaya ya kiuchumi, na yote ambayo inaota ni kwamba mgogoro huu upite, ili kuregelea sera zake za zamani, na pengine kuwafuta washirika wao wenyewe ambao walitoa shinikizo la aina yoyote juu yake, au wapinzani wake, ambao wanaweza kuwa wamekataa kuwa kama wale ambao Sisi aliwaleta kwenye kile alichokiita mazungumzo ya kisiasa ya kitaifa.

Tunatambua kwamba utawala huo hauna umakini katika madai yake ya mazungumzo, na inaonekana kwamba umelazimika kutafuta utulivu wa ndani, baada ya kuongezeka kwa migogoro ya nje na ya ndani. Benki Kuu ya Misri ililazimika kupandisha kiwango cha riba na kushusha thamani ya pauni mara kwa mara hadi pauni ilipozama, katika dalili ya kina cha mgogoro unaoikumba Misri. Kwa uamuzi huu wa kupunguza thamani ya pauni, bei za bidhaa zote zilizoagizwa kutoka nje, ambazo ni nyingi, zilipanda moja kwa moja. Kwa hivyo, bei za bidhaa katika soko la Misri zilipanda, na sarafu ngumu iliyohitajika kuagiza ngano, mafuta, na bidhaa nyingine za chakula na pembejeo zao, bila kusahau bidhaa za viwandani, ikawa haba. Hili liliongezeka baada ya serikali, kupitia miongo kadhaa ya sera za kilimo zilizofeli, kubadilisha mashamba yenye rutuba ya kilimo katika Bonde la Mto Nile kutoka kulima ngano na vipengee vingine vya usalama wa chakula hadi kwa mazao yasiyofaa na yasiyo ya lazima, chini ya maagizo ya Marekani ya kuhakikisha udhibiti wa serikali na watu wa Misri.

Mazungumzo haya yanajiri katika jaribio la kupunguza ghadhabu za watu wengi ambazo chombo cha mamlaka kinazifahamu kikamilifu, na ambacho kilipendekeza kufanya kazi ili kuzipunguza kupitia mazungumzo haya na mengine, labda rai jumla itashughulishwa nayo, hata kwa muda, haswa kwa shinikizo linaloongezeka la Mfuko wa Fedha wa Kimataifa kutekeleza maamuzi yake ya hivi karibuni, ambayo serikali inasita kutekeleza na inahusiana na kuondoka kwa jeshi kutoka kwa uchumi na kuelea kihalisi kwa pauni bila kuingiliwa na serikali, na serikali inaogopa masharti haya mawili mno; kwa sababu kuondoka kwa jeshi kutoka kwa utawala wa uchumi husababisha kupotea kwa utiifu wa msaidizi wa kijeshi mwenye nguvu zaidi, huku ueleaji mpya wa pauni unadhihirisha janga la halisi na labda mapinduzi ambayo hayabaki au kuondoka.

Mazungumzo hayatauokoa utawala ambao umepoteza vipengele vyote vya maisha. Bali mageuzi yake yoyote ni kuzunguka katika shimo la kufeli na kunusurika katika kinamasi cha majanga, na hakuna tiba isipokuwa kwa kuung'oa kabisa, kwani ndio mzizi wa maradhi na sababu ya kila balaa. Hakuna wokovu wa kweli kwa Misri isipokuwa chini ya Khilafah Rashida kwa Njia ya Utume, na fursa hiyo inafaa kwa watoto waaminifu wa Kinana kuisimamisha kwa kuwanusuru wafanyikazi wake.

Enyi Wanyoofu katika Jeshi la Kinana: Sasa mko kati ya machaguo mawili; ima Pepo ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na neema yake ya milele, au Pepo ya watawala na starehe yake ya muda inayopita, na Wallahi bila shaka itakuburuteni mpaka Motoni. Mtu mbaya zaidi ni yule aliyeiuza dunia yake kwa Dini yake, basi vipi kuhusu mtu aliyeiuza Dini yake kwa ajili ya dunia hii kwa watawala wasaliti waliotangaza vita na Mwenyezi Mungu, Dini yake na walinzi wake?! Wallahi inachokupeni serikali hii ni sehemu ya haki zenu ambazo ilikunyang'anyeni, basi ikataeni kikamilifu au ichukueni kwa haki yake kama halali, kwa kutoa nusrah (msaada) kwa Hizb ut Tahrir kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa Njia ya Utume, basi fanyeni hima Mwenyezi Mungu akuandikieni ufunguzi na juu ya mikono yenu, ili mpate ushindi mkubwa.

[وَالَّذِينَ آمَنُواْ وَهَاجَرُواْ وَجَاهَدُواْ فِي سَبِيلِ اللهِ وَالَّذِينَ آوَواْ وَّنَصَرُواْ أُولَئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقّاً لَّهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ]

“Na walio amini wakahama na wakapigana Jihadi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na walio toa mahala pa kukaa na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli. Watapata msamaha wa Mwenyezi Mungu na kuruzukiwa kwema.” [Al-Anfal 8:74]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Misri

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Misri
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu