Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  11 Dhu al-Qi'dah 1440 Na: 1440 H / 12
M.  Jumapili, 14 Julai 2019

 Taarifa kwa Vyombo Vya Habari

Merekebisho Kwenye Kanuni za Kuzuia Ugaidi ni Hatua Nyingine ya Kuushambulia Uislamu

        Tarehe 5 Julai, 2019 Rais Uhuru Kenyatta alitia saini mswada wa kanuni ya Sheria zilizofanyiwa marekebisho jumla ya mwaka 2019 ikiwemo ile kanuni ya kuzuia ugaidi (The Statute Law (Miscellaneous Amendment) Act 2019 – No. 21 of 2019). Hatua hii inamaanisha kuanzia sasa Huduma ya Kitaifa ya Polisi, Wizara ya Masuala ya Kigeni, Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, Huduma ya Wanyama Pori, Huduma za Magereza na Mamlaka ya Usafiri wa Angani zimejumuishwa na kuwa wanachama wa Kituo cha Kupambana na Ugaidi. Hii ni sambamba na mswada wa marekebisho wa sharia ya kuzuia ugaidi (Prevention of Terrorism (Ammendment) Bill, 2018) unaopendekeza kuhakikisha kuwa bodi za shule na mashirika ya kibinafsi pamoja na ya kidini yanashirikiana pamoja na asasi za serikali katika kusimamia utekelezwaji wa mipango maalum ya kupambana na mafunzo ya itikadi kali. Lau ukipita mswada huu basi wasimamizi wa shule watahitajika kuweka na kusasisha kumbukumbu za wanafunzi wote shuleni, kuhakikisha kuwa walimu wanahamasishwa kufuatilia na kutambua itikadi kali miongoni mwa wanafunzi. Fauka ya hayo, kuna mswada mwengine wa marekebisho ya kifungu nambari 30 cha sheria ya kuzuia ugaidi unaopendekeza vifungo vya vya kuanzia miaka ishirini na thelathini kwa watakao kuwa na hatia ya matendo ya ugaidi.

        Kulingana na maelezo ya kanuni hizi tungependa kufafanua yafuatayo:

       ‘Vita dhidi ya ugaidi’ nchini vinachukua sura pana zaidi inayohatarisha usalama jumla wa raia hususan jamii ya Waislamu nchini Kenya ambayo ndio inayolengwa zaidi katika kampeni jumla dhidi ya ‘ugaidi’. Licha ya kuwa polisi wa Kenya kuwa na rekodi mbaya za ukiukwaji wa haki msingi za raia, twaona kupitia kanuni hizi serikali imewaongeza nguvu zaidi ambazo twahisi kuwa polisi pamoja na asasi za kiusalama zilizojumuishwa zitakandamiza jamii ya Waislamu.

       Kuhusishwa shule, mashirika ya kibinafsi na makundi ya kidini kwenye mchakato wa vita dhidi ya ‘ugaidi’ na kile kiitwacho itikadi kali ni kuibua wasiwasi na hofu baina ya Waislamu ili waweze kufanyiana ujasusi wao kwao jambo ambalo Uislamu umelikataza. Na twatahadharisha wazazi na walimu Waislamu na washika wadau wa mashirika mbalimbali ya kidini wasije wakaingia katika kazi inayofanywa na maadui wa Uislamu kote ulimwenguni ya kuupiga vita Uislamu kwani kufanya hivyo kutawapelekea kupata idhlali hapa duniani na kesho akhera kukabiliwa na adhabu kali. Tunakumbusha kila Muislamu kwenye taasisi yoyote ile sawa ya serikali au ya kibinafsi kuwa anawajibika kuwa balozi wa ulinganizi safi wa Uislamu usiotumia njia za uhuni, fujo na mabavu kama njia ya kuleta mabadiliko. Waislamu mahala popote pale wanawajibika kuhami na kulinda utambulisho wa Uislamu.

      Tafsir ya matamshi ya itikadi kali na misimamo mikali zapaswa kutiliwa shaka na kupigwa darubini kwani twaona kwamba matamshi hutumika mara nyingi katika kubana ufahamu wa Uislamu kuwa ni dini ya kiroho tu wala sio kimfumo. Isitoshe twahisi misamiati hii itazuia Waislamu kutoshikamana na mafunzo yao ya Kidini bali kuhofia pia kuzungumza na kuzilingania rai za Uislamu kuhusu jamii, uchumi na siasa. Na haya yote itakuwa pia ni kukiuka hata zile ziitwazo haki msingi za kibinadamu za uhuru wa itikadi na uhuru wa maoni kama zinavyoelezwa kwenye katiba ya nchi. Tunafahamu kuwa licha ya Kenya kushesheheni wanasiasa waovu wanaochochea raia kuleta vurugu kwa maslahi yao ya kisiasa, twaona wanasiasa hao kattu hawashtakiwi kwa kuwa na misimamo mikali au itikadi kali!

      Kama tunavyoendelea kukariri kuwa sheria hizi za kupambana na ugaidi zinalenga si mwengine isipokuwa jamii ya Waislamu. Hakika sheria hizi ni sehemu ya kampeni ya kiulimwengu inayoongozwa na Marekani ya kushambulia fikra za Kiislamu. Fauka ya hayo zinapitishwa ili kuweza kutia hofu katika mioyo ya Waislamu ili wawache Uislamu na kuwatia mihemko ili kubeba fikra ovu za kisekula ambazo zinakwenda kinyume na Dini yao, Kampeni hii inalenga kuweka kizuizi kwa Uislamu usiweze kuongoza dunia katika ulingo wa kisiasa, kiuchumi, kijamii na kielimu kupitia hivi karibuni kusimama kwa Khilafah kwa njia ya Mtume (saw) ambayo wakati wake unakaribia kwa kasi mno. In Shaa Allah.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi Kwa Vyombo Vya Habari wa Hizb ut Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu