Jumatano, 26 Safar 1447 | 2025/08/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  8 Safar 1447 Na: 1447 / 04
M.  Jumamosi, 02 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ayman Safadi: Yeyote ambaye ana badali ya Suluhisho la dola mbili, basi na aiwasilishe!
Hizb ut Tahrir imewasilisha na inaendelea kuwasilisha suluhisho halali na la kivitendo
(Imetafsiriwa)

Je, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan anauliza kwa dhati njia badali ya suluhisho la dola mbili ili tujibu?

Haya ndiyo yaliyosemwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan Ayman Safadi katika kikao kikuu cha “Kongamano la Kimataifa la Umoja wa Mataifa kuhusu Suluhisho la Amani la Kadhia ya Palestina na Utekelezaji wa Suluhisho la Dola Mbili”, lililofanywa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, chini ya uenyekiti wa Saudi Arabia na Ufaransa mnamo Jumatatu, tarehe 28/07/2025.

Serikali ya Jordan ndio iliyowawekea watu wa Jordan na Umma wa Kiislamu suluhisho linaloendana na kuhifadhi usalama wa umbile katili la Kiyahudi. Hukuwa na maregeleo ya masuluhisho ya kadhia ya Palestina isipokuwa Marekani, rafiki wa serikali hii, mshirika wa umbile la Kiyahudi, mdhamini wake, mlinzi wake, na mshirika wake katika vita vya maangamizi na njaa dhidi ya watu wa Gaza.

Je, kuna yeyote aliyewasilisha suluhisho la kadhia ya Palestina tofauti na suluhisho la dola mbili, tangu mwanzo wa kadhia hiyo—iwe kutoka kwa watu wa Jordan au kutoka kwa vyama vya kisiasa vyenye kanuni na wanaharakati wa dhati—amepokea chochote kutoka kwenu zaidi ya kukamatwa, kuteswa, kufunguliwa mashtaka katika Mahakama ya Usalama ya Taifa, na kufungwa jela chini ya mashtaka madogo kama kuchochea kuhujumu serikali? Je, usalama na uwepo wa serikali hii umefungwa kujibu masuluhisho ya maadui zake?!

Ni wazi kuwa miradi yenu ya kisiasa ndiyo iliyothibitisha kufeli kwa miongo mingi hadi hali ya nchi na wananchi kufikia hali ya udhalilifu wa aibu. Ilithibitisha kwamba mmejitolea kuwatii maadui wa Ummah, kutoka kwa umbile la Kiyahudi na mfumo wa kimataifa unaowakilishwa na makafiri wa kikoloni wa Magharibi Amerika na Ulaya. Masuluhisho yenu badali kama lile la dola mbili hayatafaa dhidi ya suluhisho la asili, ambalo ni jihad katika njia ya Mwenyezi Mungu, na kurudi kwa dola ya Kiislamu na kutabikishwa kwa Shariah ili kuinusuru nchi na watu kutoka katika makucha ya wale mnaowaita kuishi ubavuni na kuhifadhi usalama wao.

Lakini hilo liko mbali! Nyinyi si katika Ummah na Ummah si katika nyinyi. Mliletwa na makafiri wakoloni wa Magharibi kukaa juu ya vifua vya watu kwa masuluhisho ya kunyenyekea na kujisalimisha. Ikiwa mulikuwa chembe ya ikhlasi na mulijua kuwa Mayahudi wachukizao wanakataa suluhisho la dola mbili, na kwamba hawataki mazungumzo - kama nyinyi wenyewe mlivyosema - wakati Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilishambulia kongamano la Umoja wa Mataifa jijini New York juu ya suluhisho la dola mbili kwa kusema: “Kitendo cha hadhara kinachodhuru juhudi za kidiplomasia”, ikiegemea upande wa umbile la Kiyahudi katika kukataa suluhisho la dola mbili,  basi kwa nini mnaendelea na uteteaji na upigiaji debe ulio tasa wa suluhishio hilo na kutegemea baadhi ya dola za Ulaya na nia yao ya kuitambua dola ya kindoto ya Palestina ambayo haina uhalisia wowote? Au je, suluhisho kama hilo lina tafsiri nyengine, na mnawahadaa tu watu wa Palestina na Jordan ili kuifilisi kadhia ya Palestina kwa gharama zao, ima kwa njia ya uhamishaji wa kidanganyifu au kwa kuwapa wakaazi wa Ukingo wa Magharibi mwavuli wa Jordan ili kukidhi matarajio ya Mayahudi?

Hata kama tukisia kwa madhanio kuwa mnataka suluhisho la dola mbili, hata suluhisho hilo linahitaji nguvu wa kulilazimisha juu ya umbile la Kiyahudi na Amerika. Na nguvu kubwa muliyonayo ni malalamiko na shutuma za kidiplomasia zinazoelekezwa kwa sheria ya kimataifa ambayo Safadi mwenyewe aliitaja awali kuwa imekufa. Je, hamuoni kwamba munakabiliwa na chaguzi mbili: ima kulilazimisha umbile la Kiyahudi kwa nguvu—ikimaanisha kupigana—angalau kuuhifadhi ubwana wa Jordan ambao mumeudhalilisha katika vumbi huku mukidai kuutetea, au kusalimu amri na kunyenyekea?!

Ama ustadi wako wa maneno matupu ya kisiasa ambayo hayawashi wala hayazimi, ni kielelezo cha fedheha ambacho hakitoki hata kwa dola dhaifu zaidi, kama ulivyosema: “Ni wakati wa ulimwengu kuchukua hatua dhidi ya Israel inayopinga suluhisho la dola mbili”. Ulimwengu huu unaozungumza nao ni upi? Je, ni ulimwengu ambao umenyamaza kimya kuhusu umbile la Kiyahudi, hata kushiriki katika mauaji na njaa ya watu wa Gaza?!

Iwapo kuna matumaini yoyote ya kuukomboa Ummah kutoka katika makucha ya ukoloni wa Magharibi na udhibiti wake wa kihadhara, kisiasa, kijeshi, na kiuchumi na kung'oa umbile la Kiyahudi kutoka kwenye mizizi yake, basi umoja wa kinyenzo wa Kiislamu juu ya ardhi - pamoja na umoja wa kihisia ambao tayari unaonekana - ndio unaofanikisha matumaini haya. Haya ndiyo tunayoyafanyia kazi sisi katika Hizb ut Tahrir tunapotangaza kazi ya kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume, kwani ndio njia pekee na ya asili ya kutoka kwa Ummah kutokana na majanga yake ambayo umekumbwa nayo kwa miongo kadhaa. Hili ndilo nchi za Magharibi linaloliogopa na kulipiga vita, ima moja kwa moja au kupitia njia badali za udanganyifu za kujisalimisha kama vile suluhisho la dola mbili ambalo serikali zenu zimetumia miongo mingi kulifuatilia, zikijua kwamba hazifanikiwi chochote ila uhai wa serikali yenu ili kuendelea kukariri ibara “suluhisho la dola mbili” ambalo halina uhalisia wowote wa siasa za kijiografia hata kama Ulaya yote hadaifu ingelitambua.

Kama kweli uko makini na hili, basi hili hapa ni suluhisho mbele yako uwafikishie watawala wa nchi yako; la sivyo, swali lako si lolote bali ni mazungumzo pumba miongoni mwa kauli mbiu tupu unazozikariri katika majukwaa ya mfumo wa kimataifa uliokufa.

Suluhisho halali la ikhlasi na la kivitendo ni lile ambalo Hizb ut Tahrir imewasilisha katika miaka yote ya dawah yake tangu kuanzishwa kwake. Ni kiongozi asiyewadanganya watu wake, na imekubainishia wewe na watu wake wa Jordan na nchi za Kiarabu zinazoizunguka Palestina wakati gharama ilikuwa chini zaidi kwa Umma na tawala, kabla ya mambo kuwa mabaya zaidi kufikia kiwango hiki cha kutelekezwa kutokana na sera na utegemezi wenu.

Na liko, kwa uwazi kabisa: kupeleka majeshi, kupigana na umbile la Kiyahudi, na kuikomboa Palestina yote kutokana na maovu yao na kukata kamba ya msaada wa watu kwao.

[إِنَّ فِي ذَلِكَ لَذِكْرَى لِمَن كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ]

“Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia.” [Qaf:37]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu