Jumapili, 24 Sha'aban 1446 | 2025/02/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  11 Sha'aban 1446 Na: 1446 / 14
M.  Jumatatu, 10 Februari 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Trump asingeweza Kututawala kama Tungekuwa na Khalifa, na Umbile la Kiyahudi Lisingekuwepo bila Usaliti wa Watawala wetu
(Imetafsiriwa)

Viongozi wa ukafiri nchini Amerika na Ulaya, pamoja na chombo chao, umbile la Kiyahudi, wanajua kwamba misimamo ya watawala wa Waislamu, duara zao za kisiasa, na wapambe wao—wanaowatukuza—hawawakilishi wengi wa Waislamu, wala hawaakisi matumaini yaliyo ndani ya nyoyo zao kwa ajili ya kuregeshwa kwa mamlaka yao. Ukitaka kuelewa msimamo wao wa kweli na jibu lao kwa maamrisho ya Mwenyezi Mungu mbele ya chuki kwenu na kuwaua duniani kote, na kusubutu kwenu kutishia kukalia ardhi zao zaidi na kupora mali zao, musiangalie zaidi ya kiburi cha kiongozi wenu Trump. Kwa kutokuwa na haya mbele ya ulimwengu, ameonyesha kiburi cha Amerika kafiri na msaada wake kwa wale walioshukiwa na ghadhabu ya Mwenyezi Mungu.

Wakati huo huo, nyoyo za wapiganaji wa kimsalaba wa Ulaya zinaficha hata chuki kubwa zaidi kwa Waislamu—iwe ni kwa wito wa Trump wa kuhamishwa watu wa Gaza, vita vya Kiyahudi dhidi ya watu wa Ukingo wa Magharibi kama utangulizi wa kile wanachokiita "Judea na Samaria," au utetezi wa Muungano wa Ulaya wa suluhisho la dola mbili.

Uongo, udanganyifu, usaliti, na uchokozi umetosha sasa! Marekani ni adui mkubwa wa Umma wa Kiislamu na ardhi zake. Si rafiki, mshirika, wala mwandani isipokuwa katika msamiati wa watawala vibaraka. Yeyote anayejihusisha nao kwa kisingizio hiki, kwa kiwango chochote, anashiriki katika dhambi na uchokozi wake. Na adui namba moja anayekaririwa mara kwa mara ni Uingereza—kichwa cha nyoka—ambayo ilicheza na dori kubwa zaidi katika kulipanda umbile la Kiyahudi nchini Palestina na kisha kuliwezesha kupitia watawala wake watiifu na wasaliti.

Haikubaliki kwa watu wa Jordan, katika kupinga kwao uhamishaji makaazi, kutetea maafikiano yaliyofanywa na utawala wa Jordan kwa maadui zake tangu kuasisiwa kwake—makubaliano ambayo yameipeleka nchi hii na watu wake katika hali hii ya udhaifu, udhalilifu na unyenyekevu, kama walivyofanya na watu wa Palestina hapo awali. Ni jambo lisilokubalika vile vile kwamba wakati matamshi ya hivi majuzi ya Trump yanapoleta tishio la kuwepo kwa utawala huu, inawageukia watu wa Jordan kwa ajili ya kuungwa mkono na kutetewa—wakati ni utawala huu huu uliowaleta kwenye hali yao ya sasa ya taabu, udhalilifu, na ugumu wa maisha. Na bado, unaendelea kucheza kamari katika kuimarisha mafungamano yake na Amerika na umbile la Kiyahudi.

Hata sasa, wakati wa ziara yake ya hivi sasa nchini Marekani—ikitanguliwa, kama kawaida, na ziara ya Uingereza kwa ajili ya mashauriano na maelekezo—serikali hii inakutana na Trump na vyombo mbalimbali vya utawala vya Marekani chini ya kile Wizara ya Mambo ya Nje ya Jordan inakiita “uhusiano wa muungano na urafiki.” Lakini baada ya tishio la wazi la Trump kwa Jordan, baada ya maandamano ya watu wa Jordan kuelezea utayari wao wa vita na makabiliano ya kijeshi, na baada ya umbile la Kiyahudi kukejeli udhaifu wa vikosi vya Jordan, vipi bado kunaweza kuwa na uhalali wowote wa kuendeleza uhusiano huu wa kizembe?!

Inashangaza kweli kwamba nyinyi, watu wa Jordan, mnasimama na kueleza utayari wenu wa kujitolea mbele ya majeshi ya uvamizi na uovu—kama vile mataifa ya jirani ya Palestina yalivyofanya—baada ya maadui wa Umma kutoa meno yao na kuweka wazi njama zao na uungaji mkono wao usio na mipaka kwa ajili ya umbile la Kiyahudi. Wakati huo huo, utawala huu unaendelea kujiweka sawa nao kwa kudumisha majeshi ya Marekani, kushikilia mkataba wa pamoja wa ulinzi, na kuhifadhi makubaliano ya Wadi Araba. Hii inathibitisha udanganyifu na ulaghai wake, pamoja na ushirikiano wa wasaidizi wake—waandishi, wabunge, waheshimiwa, na vyama—ambao wanakupotosheni huku wakipamba matendo ya utawala huu unapokabidhi nchi kwa maadui zake. Mnachotaka na kinachotumikia maslahi yenu kinatofautiana kabisa na maslahi ya utawala huu, ambao unakubebesheni gharama kubwa kutokana na mahusiano yake na maadui zenu. Katika dhurufu kama hizo, ulipaswa kuvikusanya vikosi vyake kwa ajili ya vita vitukufu dhidi ya Mayahudi badala ya kuzuru pango la adui mkubwa huko Washington.

Enyi watu wa Jordan, enyi Umma wa Kiislamu!

Mahusiano yenu na maadui yamefafanuliwa wazi na Uislamu. Hadhi ya ardhi ya Jordan inaamuliwa na maneno ya Mwenyezi Mungu:

[سُبْحَانَ الَّذِي أَسْرَى بِعَبْدِهِ لَيْلاً مِّنَ الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ إِلَى الْمَسْجِدِ الْأَقْصَى الَّذِي بَارَكْنَا حَوْلَهُ]

SUBHANA, Ametakasika aliye mchukua mja wake usiku mmoja kutoka Msikiti Mtukufu mpaka Msikiti wa Mbali, ambao tumevibariki vilivyo uzunguka, [Al-Isra: 1]

Ardhi ya Jordan ni miongoni mwa ardhi zilizobarikiwa zinazozunguka Msikiti wa Al-Aqsa. Kwa hiyo, haijuzu kuamiliana na wanyakuzi wa Al-Aqsa na washirika wao kwa njia yoyote isiyokuwa ya yale aliyoamrisha Mola wetu Mlezi—kupigana ili kuirudisha. Kuanzisha mahusiano na maadui hawa hairuhusiwi. Mayahudi ni wanyakuzi wahalifu, na Amerika, pamoja na Wapiganaji wa Msalaba nyuma yake, iko katika hali ya vita halisi dhidi yenu. Jordan na Amerika si washirika-huu ni upuuzi mtupu ambao haupaswi tena kukuhadaini.

Bila kujali matokeo ya mikutano ya serikali nchini Amerika - iwe makubaliano, makaazi, au kupunguza vitisho - hii si chochote ila udanganyifu, unaotumikia kufutwa kunakoendelea kwa kadhia ya Palestina huku ikirefushwa muda zaidi.

Hatuzungumzi juu ya ndoto au mawazo. Hili ndilo suluhisho la dhati na la halali—njia fupi zaidi ya kujinasua kutoka kwenye mtego wa maadui. Chombo cha kisiasa cha Uislamu, Khilafah kwa njia ya Utume, ndiyo itakayokusanya majeshi kwa ajili ya ukombozi. Kwa muda mrefu majeshi yetu yamepuuza wajibu wao mbele ya Mola wao Mlezi, lakini uregeshwaji wake uko karibu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, ili kukuonyesha nguvu za kweli za Umma wa Kiislamu—kwanza kupitia Aqidah yake, kisha kupitia mali yake iliyoporwa na ushujaa wa watu wake.

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا بِطَانَةً مِّن دُونِكُمْ لَا يَأْلُونَكُمْ خَبَالاً وَدُّوا مَا عَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ]

Enyi mlio amini! Msiwafanye wasiri wenu watu wasio kuwa katika nyinyi. Hawataacha kukufanyieni ubaya. Wanayapenda yanayo kudhuruni. Imekwisha fichuka chuki yao katika midomo yao. Na yanayo ficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Ishara ikiwa nyinyi mtayatia akilini.” [Al-i-Imran: 118]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu