Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Iraq

H.  4 Rabi' I 1444 Na: 1444 / 05
M.  Ijumaa, 30 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Iraq Mpya ambayo Amerika Iliahidi
(Imetafsiriwa)

Mnamo siku ya Jumatano na Alhamisi, Septemba 28-29, 2022, Iran ilishambulia vikali wilaya za majimbo ya Erbil na Sulaymaniyah kwa makombora ya balistiki na droni zilizonaswa, zikilenga makao makuu ya vyama vya upinzani vya Kikurdi. Mnamo Jumatano, Wakfu wa Kupambana na Ugaidi katika Mkoa wa Kurdistan ulitangaza kwamba "Walinzi wa Mapinduzi ya Iran walifanya shambulizi la kombora katika eneo hilo katika hatua nne, ambalo liliwaacha mashahidi 13 na 58 kujeruhiwa." Na siku ya Alhamisi, Naibu Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Vidant Patel alithibitisha kifo cha raia wa Marekani wakati wa shambulizi la kombora la Iran lililolenga maeneo ya upinzani katika eneo la Kurdistan jana (Jumatano) kulingana na kile kilichochapishwa na Habari za Shafaq. Hili lilisadifu na ndege za Uturuki kushambulia kwa mabomu maeneo ya Chama cha Wafanyikazi cha Kurdistan kaskazini mwa Dohuk, chama hiki kinajulikana kupinga utawala wa Uturuki.

Kama kawaida, kulaani na kuheshimiwa kwa ubwana wa nchi kuliibuliwa na serikali ya Iraq (isio na utashi), Umoja wa Mataifa, Amerika, Uingereza, Ufaransa na zenginezo.

Kwa kuongezea, eneo karibu na Ukanda madhubuti wa Kijani katikati mwa Baghdad pia lilikumbwa na shambulizi kiasi la kombora siku ya Jumatano, na makombora matatu. Na kombora moja lilianguka pambizoni mwa bunge la Iraq wakati kikao cha uchaguzi wa naibu spika wa kwanza wa bunge kilikuwa kikifanyika ambapo mrithi wa Hakim al-Zamili aliyejiuzulu kutoka vuguvugu la Sadri, atachaguliwa.

Mwandishi habari wa Shirika la Habari la Shafak alisema kuwa wabunge kadhaa walitoka nje ya ukumbi wa Bunge mara tu baada ya shambulizi hilo la bomu, hali iliyoashiria kuwa maafisa wanne wa idara ya usalama walijeruhiwa kiasi na idadi kadhaa ya magari kuharibiwa kutokana na kuanguka kwa kombora. Makombora hayo yalitua karibu na Eneo la Kijani.

Pamoja na machafuko hayo yote, tunaona jinsi sakata ya miungano ya kisiasa inavyodhamiria kufanya kikao cha bunge na kuunda serikali, bila kujua kinachoendelea, kana kwamba matukio haya yanatokea kwenye sayari nyingine! Hawajali nchi wala watu wake, na wameyafanya maslahi yao makubwa kuwa ni kuunda serikali na kugawanya nyadhifa za mawaziri, ambazo kupitia hizo nchi inaibiwa, haswa baada ya Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Iraq, Ammar Khalaf kutangaza mnamo Agosti 21 kuhusu kuwepo kwa ziada ya akiba ya fedha za kigeni ambapo nchi ilizidi dolari bilioni 80, na inatarajiwa kufikia bilioni 90 mwishoni mwa mwaka. Khalaf aliongeza, kwa Shirika rasmi la Habari la Iraq, kwamba akiba ya dhahabu ya benki hiyo iliongezeka kwa tani 30 na kurekodi zaidi ya tani 131 kwa jumla.

Miungano hii ya kisiasa inasisitiza kufanyika kwa kikao cha bunge na kuunda baraza la mawaziri, pamoja na kulishawishi vuguvugu la Sadri, linataka kuvunjwa kwa Bunge lenye wizara kadhaa, kwa muda wa mwaka mmoja na nusu, na baada ya hapo uchaguzi wa mapema ufanywe.

Kutokana na yote yaliyosemwa, ni wazi kwa wote jinsi utawala huu wa kisiasa unavyo puuza damu na maisha ya watu wa Iraq, utawala huu ulioundwa na mvamizi Amerika tangu kuikalia kwake kwa mabavu Iraq mwaka 2003 hadi sasa, ambapo waliahidi Iraq mpya, na hii ni kweli, tumeona Iraq mpya katika machafuko, ambapo uhalifu na madawa ya kulevya yameenea, wezi na wahalifu wanastawi ndani yake, na hili linatarajiwa kutoka kwa mvamizi ambaye hana bidhaa nyingine isipokuwa uovu.

Maisha yenye staha, na usalama, na kuenea kwa maadili mema, haviwezekani isipokuwa kupitia mfumo ambao Muumba aliuwekea sheria kwa ajili ya waja wake, na heshima na utukufu vinaweza tu kupatikana kupitia kuyatekeleza yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake (saw),

[لَقَدْ أَنْزَلْنَا إِلَيْكُمْ كِتَاباً فِيهِ ذِكْرُكُمْ أَفَلا تَعْقِلُونَ]

“Na hakika tumekuteremshieni Kitabu ambacho ndani yake yamo makumbusho yenu. Je! Hamzingatii?”. [Al-Anbiya’]. Ummah wa Kiislamu chini yake iko kheri yote, katika Dini yake na katika Shariah ya Mwenyezi Mungu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Iraq

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Iraq
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu