Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh

H.  4 Rajab 1441 Na: 1441 H / 013
M.  Ijumaa, 28 Februari 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh Imefanikiwa Kuandaa Kongamano la Mtandaoni kwa kichwa: “Kielelezo cha Katiba ya Dola ya Khilafah”

Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh, leo Ijumaa, 28 Februari 2020, Imefanikiwa Kuandaa Kongamano la Mtandaoni kwa kichwa: “Kielelezo cha Katiba ya Dola ya Khilafah”. Lengo la kongamano hilo ni kuwasilisha kwa Ummah wa Kiislamu, na haswa watu wa nchi hii, kuwa Hizb ut Tahrir imeandaa Kielelezo cha katiba ya Dola ya Khilafah inayojumuisha vipengee 191 kwa msingi wa Qur’an na Sunnah, ambavyo chama hicho kimejiandaa kikamilifu kusimamia mambo ya Khilafah ya Uongofu ya pili. Ilijadiliwa katika kongamano hilo jinsi gani Dola ya Khilafah tukufu kwa kutekeleza vipengee vyake vinavyohusiana na katiba hii vitasuluhisha majanga msingi ya hivi sasa ya nchi hii, kama vile: kupata haki msingi za watu (chakula-nguo-malazi, usalama-afya-elimu), kuhakikisha kiwango cha juu cha maisha ya watu na kukuza miundombinu ya nchi.

Serikali ya sasa ya kisekula, katika utawala wake wa miomgo mingi, imeshindwa kutimiza haki msingi za watu, achilia mbali kuhakikisha kiwango cha juu cha maisha. Watu wanaendelea na harakati zao katika barabara dhidi ya serikali kudai haki zao za kimsingi, na serikali inawakandamiza watu kikatili, na kuamua kutumia zana za ubunifu katika ukatili wake. Kwa jina la maendeleo, serikali inafanya miradi mikubwa, yote inajulikana kwa deni kubwa na ufisadi mkubwa, na ambayo hainufaishi watu, lakini badala yake ni mzigo wa madeni makubwa na kodi ya kufadhili miradi hiyo inaangukia watu. Juu ya watu inatozwa VAT inayoongezeka daima na kodi, na kuongezeka kwa bei ya gesi, maji na umeme. Haya ndiyo matokeo ya nidhamu ya kisekula ya kirasilimali iliopo, ambapo watawala wana nguvu ya kutunga sheria juu ya maslahi yao wenyewe, na vile vile matamanio yao na tamaa zao. Ambapo, Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[إِنِ الْحُكْمُ إِلَّا لِلَّهِ] “Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu” [Yusuf: 40]. Kwa kweli, kwa upande mmoja watawala wa hivi sasa wanatumia nguvu ya madaraka haya kupata maslahi yao, maslahi ya warasilimali wachache na maslahi ya mabwana zao – makafiri wakoloni, na kwa upande mwingine wanatekeleza dhulma (ukandamizaji) kwa watu wengi. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[وَمَنْ لَمْ يَحْكُمْ بِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ فَأُولَئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ]

“Na wasio hukumu kwa yale aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio madhaalimu” [al-Maidah: 45]. Njia pekee ya kutoka katika hili ni kuisimamisha tena Khilafah ya Uongofu kwa kuiondoa nidhamu ya kisekula ya kirasilimali na serikali inayotawala hivi sasa. Katika muktadha huu, Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh iliandaa kongamano hili la mtandaoni.

Katika kongamano hili, wazungumzaji wameangazia: (1) Jinsi gani Katiba ya Dola ya Khilafah itakavyo hakikisha haki msingi za watu; (2) Jinsi gani Katiba ya Dola ya Khilafah itakavyo hakikisha kiwango cha juu cha maisha ya watu na kujenga miundombinu iliyoendelea katika nchi; na (3) Khilafah iko karibu na vipi hivi karibuni Khilafah itaunganisha Ummah wa Waislamu.

Kwa kushiriki katika kongamano hilo, wanaharakati wa Hizb ut Tahrir wamefanya maingiliano makubwa na watu ambao wameunda muitikio mkubwa. Watu wameshiriki katika kongamano la mtandaoni kwa shauku.

Tunawashukuru wote, Mwenyezi Mungu awajaze kila la kheri, ambao wamefanya kazi bila kuchoka kufanikisha kongamano hili. Tunamalizia kwa dua kwa Mwenyezi Mungu (swt) kuwa harakati ya kusimamisha tena Khilafah ya Uongofu ifikie sehemu inayolenga chini ya uongozi wa Amiri wa Hizb ut Tahrir, Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah, kwamba Yeye (swt) aturuhusu sisi kuisimamisha tena Khilafah ya Uongofu hivi karibuni kwa msaada na ushiriki mchangamfu wa Ummah wa Waislamu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Bangladesh

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Bangladesh
Address & Website
Tel: ‎+88 01798 367 640‎
www.ht-bangladesh.info
E-Mail: contact@ht-bangladesh.info, htmedia.bd@outlook.com Skype: htmedia.bd

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu